Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

Kuna ishu za kitoto zinaendelea kati ya hizi nchi mbili na mbaya zaidi zinaathiri maisha ya watu.
 
Wakulima wengi walitumbukia kwenye umasikini wa kutisha, wafanyabiashara walifilisika na msimu uliofuata mavuno yalishuka sana. Sitaki kuona mkulima wa Tanzania akirudi kwenye maumivu yale kwa Serikali kushindwa kutimiza wajibu wake.
Hovyo.

Kama mahindi ya Tanzania hawayataki wakenya kwa sababu zao nyingine, tutawalazimisha wayanunue?
 
Bila shaka yoyote Zitto anatafuta uteuzi kupitia siasa zake za kinafiki. Zitto anafahamu fika kuwa Tanzania ndiyo imekuwa kikwazo katika kuridhia sheria kuhusu sumu kuvu wakati nchi nyingine zote zilikwisha ridhia.

Hatuwezi kulazimisha kuwauzia sumu Wakenya, haikubaliki kimataifa wala kibinadamu.
 
Majibu yatoke wizara ya kilimo kuliko kwa huyo Zitto kabwe.

Kama walivofanya wakenya.

Zitto aache tabia za wanasiasa '"mediocre" kuzungumzia kila kitu. Yes, ni diplomacy, ola angehimiza wizara ya kilimo kupitia wakala wa utafiti wajibu barua ya Kenya kwa facts. Sio kuzungumzia diplomacy kwenye research za wengine.
Barua gani tena?

Hakuna barua iliyotumwa Tanzania.

Labda useme hiyo ya malori yanayorundikana hapo Namanga, kama ndiyo unayaita barua.

Huu ni uhuni wa kipekee wanaofanya Kenya, na niuchokozi wa maksudi kabisa.
 
CHADEMA watabisha!

Eti Kwamba?

Kwamba chadema watabisha kuwa haupo mzozo wa kidemokrasia? Kwamba watabisha kuwa wakulima wa mahindi hawathiriki sasa na kuwa hawakuathirika mno kufuatia agizo lile la kusitisha kuuza nafaka nje lilipopitishwa?

Au watabisha kuwa hapana haja ya kukaa mezani na kutatua matatizo yaliyopo kidiplomasia?

Au watabisha kuwa wakulima wa Tanzania wanazalisha mahindi yenye sumu?

Ama?

Hiiiiii bagosha, basi hao chadema watakuwa ni wenda wazimu kweri kweri.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ni MPUMBAVU tu ambaye anaweza kuziona hoja za Chadema za Wizi wa kura, Corona ambalo ni janga kubwa la dunia na uwepo wa Tume Huru na Katiba mpya ni MASLAHI binafsi ya Chadema. Hizi hoja zinagusa mamambo muhimu sana ya kuhakikisha Watanzania tunakuwa na Viongozi wanaostahili kuitwa viongozi na siyo wahuni, majizi na wauaji.
Chadema hoja zao ni tume huru, kuibiwa kura, corona yani upumbavu mtupu. Ukiwaambia wafanye siasa ya kutoa solution kwa matatizo ya wananchi unaambulia matusi. Wenyewe kila siku ni maslahi binafsi ya chama tu halafu wanategemea wachaguliwe. 2020 wamevuna walichopanda wananchi hawakuwa na sababu ya kuwashika na kuwachagua
 
Bila shaka yo yote Zitto anatafuta uteuzi kupitia siasa zake za kinafiki. Zitto anafahamu fika kuwa Tanzania ndiyo imekuwa kikwazo katika kuridhia sheria kuhusu sumu kuvu wakati nchi nyingine zote zilikwisha ridhia.

Hatuwezi kulazimisha kuwauzia sumu Wakenya, haikubaliki kimataifa wala kibinadamu.
Unahangaika sana kuwatete wakenya
 
Kwa mujibu wa utafiti, Mahindi ya mikoa miwili tu ndio yana kiwango kikubwa cha aflatoxin, Manyara na Dodoma. Mahindi ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Ruvuma, Kigoma etc hayana kabisa aflatoxin. Kenya hawawezi KISHERIA/KIMKATABA kuzuia Mahindi yote ya Tanzania!
Say Whaat ?!!!!

Hapo ni kwamba ameteleza au ? Sasa kuna jitihada zinafanyika ili (sisi watanzania tukae mbali na hayo)?

All in all busara itumike na wote tuendelee kufanya biashara, tulishane huku tukihakikisha hatulishani sumu (elimu itolewe pia kwa hao wakulima wetu wa Manyara na Dodoma)
 
Nina mahindi ambayo hayana dawa yoyote, nimeyahifadhi kwenye mifuko inaitwa PICS. Anayetafuta anicheki. Zipo tani zaidi ya 30.
 
Kila taifa lina mamlaka husika kulinda mipaka na usalama wa raia wake. Anapoibuka mwanasiasa anayetaka kutumia tukio fulani kupata umaarufu wa kisiasa ni upuuzi ambao hauna nafasi kwenye dunia ya leo.

Mamlaka ya Kenya kuangalia usalama wa chakula ina watalaamu wanaofanya kazi kwa weledi na utalaamu. Kuibuka mwanasiasa mnafiki kukosoa na kudai mahindi ni salama bila ushahidi wa kisayansi ni upuuzi.
 
Back
Top Bottom