Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

Zitto Kabwe: Mahindi ya Tanzania ni salama

Magufuli sio kiongozi ni mtawala wala haishangazi kutozingatia diplomasia inasemaje
Kwani dipromasia ni kuwa unyanyaswe kila mara kisha ujibebeshe kwa udhaifu ndio dipromasia?
Kila upande unatakiwa kutumia hiyo dipromasia,
Kama wakenya ni bingwa wa dipromasia wasingezuia mahindi kihuni bali wangewasiliana na viongozi wenzao wa nchi yatokayo hayo mazao.
 
Niliposema Zito Kabwe awe mshauri wa Mheshimiwa kuhusu uchumi hamkunielewa, sasa bado pia hamtaelewa eti eeh.
 
Jamaa wanapenda kweli kutuchokoza.....
ukiona mgogoro wa K na T ujue Kenya ndio mchokozi....
badala ya kufuta utaratibu kupitia jumui ya Africa Mashariki wao wana tu surprise....
wanashtukiza wakati maloli yapo mipakani noma sana.....
 
Chadema hoja zao ni tume huru, kuibiwa kura, corona yani upumbavu mtupu. Ukiwaambia wafanye siasa ya kutoa solution kwa matatizo ya wananchi unaambulia matusi. Wenyewe kila siku ni maslahi binafsi ya chama tu halafu wanategemea wachaguliwe. 2020 wamevuna walichopanda wananchi hawakuwa na sababu ya kuwashika na kuwach
Nchi yoote hadi mende na nzi wa chooni ni kijani, CHADEMA bado haiishi midomoni mwenu mna shida gani?

1.Je, chadema ndio Walifunga mipaka mwaka Jana na wakulima wakashindwa kuuza mahindi hadi kilo moja ilifika tsh 100/= na walipolalamika wakaambiwa walishe mifugo?

2. Je, chadema ndio Waliwapiga marufuku wafanyabiashara wa mahindi kwa kuwapa amri ya ghafla ya kusaga na ku-pack wauze unga?

3.Je, chadema ndio walimlazimisha tajiri Summry aliekuwa na zaidi ya magunia elfu hamsini ayauze humu ndani kitu kilichopelekea kupata hasara kubwa maana alilazimika kuuza debe kwa tsh 2000//=?

4. Je, chadema ndio waliovamia soko la korosho kwa mtutu wa bunduki na kutoa ahadi hewa ya ununuzi wa korosho kwa bei ya juu tena kwa kishindo cha awamu ya tano na mwishowe korosho haikununuliwa na kuwaachia wakulima umasikini ambao duniani haujawahi kuwepo, mwisho wakaokota kampuni feki la kununua korosho kutoka Kenya nalo likapotea kusiko julikana.

5.Je, Chadema ndiyo iliharibu soko la mbaazi na mazao jamii ya mikunde mfano eneo niliko kilo ya mbaazi ilifika tsh. 2500/= lakini baadaye ilipelekea bei kushuka na kufikia kilo ya mbaazi tsh 100/= na wateja walikosekana?

6. Zitto kaonesha namna ambavyo serikali ilifeli ktk kutatua changamoto za masoko ambapo hata yale masoko yanayosuasua yakaishia kufa kifo cha mende badala kuishauri kutokana na makosa hayo jitu linakurupuka na kuivamia Chadema, huku ni kutumia kichwa kama kama pamba na fuko la kuhifadhi meno.
 
Siasa kila kitu, Kenya wamesema na kuweka kinachowafanya wayakatae mazao ya TZ. Jibu ni kuwa prove wrong kwa kuomba vipimo vifanyike kwa kutumia neutral lab na wote wahudhurie kama witness. Sio kukimbilia kufunga mipaka, kuzuia ndege nk. Scietific allegations hujibiwa kisayansi pia sio kisiasa.
 
Wakati mnachoma vifaranga wao mliwapa taarifa?
 
Siasa kila kitu, Kenya wamesema na kuweka kinachowafanya wayakatae mazao ya TZ. Jibu ni kuwa prove wrong kwa kuomba vipimo vifanyike kwa kutumia neutral lab na wote wahudhurie kama witness. Sio kukimbilia kufunga mipaka, kuzuia ndege nk. Scietific allegations hujibiwa kisayansi pia sio kisiasa.
Hayo si ndio ilibidi yafanywe na Kenya kabla ya kutoa katazo?
 
Chadema mnajiona wanyonge mbele ya kila mtu!

Sisi tulifikiri ni kwa wazungu tu kumbe hata kwa wakenya? Au kwa vile wanaongea sana Kingereza?
mtu/watu wowote against serikali hii dhalimu ni rafiki yetu, haiwezekani mtufanyie uhuni kwenye uchafuzi (uchaguzi) mkuu halafu tuwapende...simpo tu, adui yenu sisi ni rafiki kipenzi.
yaani kwangu ingetokea hata alshabab wamewafanyia yao kwenye yale mamikutano yenu sijui ya halmashauri kuu sijui kamati ya takataka gani mnapokutanaga Dodoma ningefurahi kinoma!
 
Back
Top Bottom