Sumti
JF-Expert Member
- Jan 30, 2016
- 2,342
- 2,193
MzaireYuda iskariote, Zito Kabwe anaongea sasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MzaireYuda iskariote, Zito Kabwe anaongea sasa
kazikwe nae rondoMagufuli atakufa tena huko aliko
Unajua JPM alipanda chuki ekari nyingi sana. Sasa ni ngumu kuachwa salama. Kikubwa wengine wajifunzeAmeongea upuuzi mtupu! Ameingiza siasa kwenye shughuli ya msiba. Huyu bila kumzungumzia JPM nadhani siki yake haiendi vizuri, Kila speech analazimisha kumchomekea, Alaaniwe.
Hivi nyongo huwa inatemwa mara ngapi?? Mbona huwa anaitema kila wakati? Ina maana hata kwenye msiba wa WAZURI HAWAFI unaokuja soon, atatema nyongo pia?? PATHETIC!!Nafuatilia kuaga mwili wa Hayati Bernard Membe kwenye runinga. Nimeipenda hotuba ya Zitto Kabwe maana hajamng'unya maneno katema nyongo kwa kusema ukweli. Tuwe wakweli kwa kusema ukweli na siyo kurembaremba hata pale ambapo mambo hayakwenda vizuri.
Alipanda chuki Kwa Nani na Kwa namna gani lazima muishe kwa Sababu ya laana ya kumcheka marehemu.Unajua JPM alipanda chuki ekari nyingi sana. Sasa ni ngumu kuachwa salama. Kikubwa wengine wajifunze
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023
Saa 4:00 Asubuhi
Viongozi Mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wameanza kuwasili
Saa 5:45 Asubuhi
Mwili wa Marehemu Bernard Membe umewasili Karimjee ukiwa umebebwa kwenye gari Maalum la kubebea Maiti.
Saa 6:00 Mchana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan anawasili.
Rais Samia amekwenda moja kwa moja kusaini kitabu cha Maombolezo kilichoandaliwa, kisha kusalimia na kuwapa pole wafiwa.
Saa 6:05 Mchana
Dua na Sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini kisha salamu za viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wamekaribishwa kutoa salamu zao.
Zitto Kabwe anazungumza; Amemuelezea Bernard Membe kama Mwanasiasa mkomavu aliyepambana kulinda heshima yake dhidi ya watu waoga walioshindwa kumkabili kwa hoja, ambapo baadhi ya viongozi na Watu wenye Mamkala walitumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao.
Amesema Ushindi wake katika kesi ile utazika utamaduni huu mbaya wa kushambulia na kuchafua watu.
“Wewe sio tu ulizuia na kukemea upuuzi ule, bali ulihakikisha unatoa mfano kwa mpuuzi aliyebebeshwa upuuzi ule ili kuwa funzo kwa wapuuzi wengine wote”
Amesema kuwa anataraji wale wote waliohusika na mambo yale watamuomba radhi akiwa kwenye umauti.
View attachment 2621369
Zitto KabweAidha, amemsifu kwa kusimama imara katika nyakati ngumu ambazo taifa lilipitia, nyakati ambazo watu wengi waliogopa kuisimamia kweli.
Amemshukuru kwa kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo aliwapa mafunzo na kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii.
“Umetimiza wajibu, upumzike pema Membe… Tangulia BM, umeacha simanzi kubwa kwa watanzania. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Upumzike pema mzee wangu Membe” Zitto Kabwe
Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) anazungumza; Amesema Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa Masikitiko na Mshituko mkubwa kifo chake.
View attachment 2621375
Daniel Chongolo, Katibu Mkuu CCM
Amesema CCM imepoteza kada wake mkubwa, na amewaomba watanzania na wana CCM kuenzi mema yake kwa kusimamia maslahi ya watanzania ndani na nje ya nchi.
Stergomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anazungumza; Ametoa pole kwa mjane wa Marehemu pamoja na watoto kwa kuondokewa mpendwa wao.
Amesema wakati wa uhai wake alitekeleza kazi zake kwa weledi mkubwa hasa katika kukuza uhusiano mwema kati ya Tanzania na mataifa mengine ambao nchi imenufaika sana na kazi zake.
View attachment 2621403
Stergomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MasharikiAlichangia katika kujenga mipango mizuri kwenye sera za nje.
Amemshukuru Membe kwa kumtia Moyo wakati alipoteuliwa kugombea ngazi ya kimataifa ambapo alikuwa nae bega kwa bega kuanzia hatua za mwanzo na muda wote wa kazi.
Rais Samia Suhulu Hassan anazungumza; Amesema kifo ni jambo lisiloepulika kwa binadamu, na wote tumepokea kwa huzuni taarifa hizo za kifo cha Membe.
Serikali, Familia ya Rais na watanzania wote tunaungana kwa pamoja kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wanalindi wote kwa kumpoteza mpendwa wao.
View attachment 2621413
Samia Suhulu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaRais amemsifu kwa kuwa mtu muungwana na kaka wa karibu aliyekuwa tayari kusadia wengine. Amesema maamuzi ya Mungu huwa hayalaumiwi bali hushukuriwa.
Amemalizia kwa kuwaomba watanzania kumuombea Membe roho yake ipumzike kwa amani.
Nape Nnauye anazungumza; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza kwa niaba ya familia amemshukuru Rais Samia kwa kusimama bega kwa bega na familia ya Marehemu katika wakati huu mgumu ambapo gharama nyingi za msiba huu ikiwemo usafiri zimebebwa na Rais mwenyewe.
View attachment 2621415
Nape Nnauye anazungumza; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya HabariAmeishukuru Wizara ya Mambo ya nje kwa kuwabeba, kwa moyo wa upendo walioonesha. Heshima hii hawataisahau.
Amewashukuru viongozi wote wa Serikali na Mkoa, Madaktari wa Hospitali ya Kairuki, majirani, waombolezaji, ndugu, jamaa na marafiki wote kwa umoja walioonesha.
Saa 7:30 Mchana:
Jeneza linafunguliwa ili waombolezaji watoe heshima za mwisho. Rais Samia anawaongoza waombolezaji.
Saa 7:50 Mchana
Zoezi la kuaga limehitimishwa Rasmi.
kazikwe nae rondoWale lialia wa jpm wakazikwe nae tafadhali msituchoshe kutafuta huruma za watu kilasiku. Unapoyosha watu kijinga tu leta clip aliyosema jpm mpumbavu au unataka ukalale pembeni yake pale chato hujakatazwa
Alishaisha yeye na chuki zake aliifanya Tanzania kama Burundi,DRC,Uganda,Rwanda na Sudan.Alipanda chuki Kwa Nani na Kwa namna gani lazima muishe kwa Sababu ya laana ya kumcheka marehemu.
Mna matatizo ya kisaikolojia.Mwamba bado amesimama ndo maana bado kuna watu wanapambana naye
Ngoma droo wamesawazishaUna maana gani mkuu??
Weka evidence Acha kuropokaAlishaisha yeye na chuki zake aliifanya Tanzania kama Burundi,DRC,Uganda,Rwanda na Sudan.
Wema hawafiUko sahihi. Na ndo maana nilimwambia mtu huko juu; maumivu mliyoyapata kwa kupigwa mwereka kwa Jiwe haviwezi kupozwa na kifo cha Membe. Hawa watu hawakuwa na hadhi sawa, na maumivu ya vifo vyao hayawezi kuwa sawa. Joe mshale wa 17 March, 2021 ulikuwa mkali haswaa!
Eti watanzania, kwaiyo nimekutuma useme kwa niaba yangu?Rest in Peace Membe, watanzania tunakulilia, Mungu akulaze mahali pema peponi AMEN
Kama anampenda sana Membe akazikwe naeMnaofatilia msiba wa Membe nafikiri mnamsikiliza sasa Zitto akimuelezea marehemu Membe.
Zitto badala ya kumuongelea Membe anaushambulia utawala wa Magufuli mpaka kumuita JPM mpuuzi.
Na kwanini wenzake wamepewa dakika mbili ila Zitto kapewa dakika zaidi. Zitto anachafua hali ya hewa...
Alikuwa muovu kuliko shetani😂😂😂😂
Kisa cha kufa mara mbili nini?
Kwani imerudi ??!Kuna tetesi wasaidizi wake walimtaka asihudhurie kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi na yeye ameng'ang'ania.
Huenda leo akaja na barakoa.
Tunatakiwa tuishi kwa kuhurumiana sote !!Pole Mama Samia kwa kuondokewa na mtu wa karibu.
Pole JK kwa kuondokewa na rafiki yako.
Pole kwa Watanzania wote
Apumzike salama jasusi mbobevu. Ni safari yetu binadamu wote. Zingine zote mbwembwe tu zetu wanadamu...