mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,916
- 8,630
Ohooo kajamaa kamerudi tena ??Naona precautions za CORONA zimetaradadi hapa, kila muda tunapitishiwa sanitizer.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ohooo kajamaa kamerudi tena ??Naona precautions za CORONA zimetaradadi hapa, kila muda tunapitishiwa sanitizer.
Kuna mtu alikua anachafua watu Kama zitto kipindi cha JK? Umesahau zile nakala zake?[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Great thinkers msituchekeshe bwana, aliyekwambia ana uchungu na membe nani?!!! Mbona ilionekana wazi kuwa anakerekwa na vikaragosi vinavyotumwa kuchafua watu!!!! Au wenzetu mnatumia akili ipi?!!!!! Zitto ni mmoja wa walioathirika na hali hiyo, musiba alimsingizia hadi kuwa anatembea na mke wa marehemu Filikunjombe
Labda atalazwa na mapepo sio peponi kwa mbwa yuleRest in Peace Membe, watanzania tunakulilia, Mungu akulaze mahali pema peponi AMEN
Mtasafirisha lini huo mzigoPole Mama Samia kwa kuondokewa na mtu wa karibu.
Pole JK kwa kuondokewa na rafiki yako.
Pole kwa Watanzania wote
Apumzike salama jasusi mbobevu. Ni safari yetu binadamu wote. Zingine zote mbwembwe tu zetu wanadamu...
Membe domo kulegea haamki tena kenge nyieNi kweli,maana yule wa Chato mwenye kichwa chenye kona kona kama korosho yeye amesimama.
Kuchafuana ndani ya Nji hii hakutakwisha ! Kwa sababu ndio njia ya vilaza kujiliwaza !!Kuna mtu alikua anachafua watu Kama zitto kipindi cha JK? Umesahau zile nakala zake?
Zitto huyu kipindi lowassa ameanza mchakato wa kugombea huko ccm si ndio alikua akitumika sana kwenye magazeti kuandika nakala za kumponda lowassa?
Naomba nae huyu yuda ataftiwe utaratibu wa kumuondoa mafenesi usoni anajifanya ni smart sana mbwa hyuZitto anajuwa ukweli maana pia inasemekana ni team X majasusi bana ujuwe hili tukio lakutisha sana amezima kama mshumaa ni ghafla...
Eti mtu aende kuomba radhi kwenye kabri la kenge kama bm [emoji1787][emoji1787][emoji1787]Acha wajipe faraja kwa kumpoteza muhuni mwenzao
Nani ambaye siye muovu?Alikuwa muovu kuliko shetani
Membe, Kikwete, Samia mzee Mwinyi, mzee Makamba, n.k ni watu wema sana. Lkn jiwe alikuwa shetani na nusuNani ambaye siye muovu?
Wazee watamfufua? Hizi PhD zinawasaidia kweli nyinyi?Dakika ya 90 watamaliza wazee.
Unaumia ukiwa wapiEti watanzania, kwaiyo nimekutuma useme kwa niaba yangu?
Kwa mafanio huo huo. Kile kipindi zotto alipambana na akinachenge na akina rostam azizi kupitia list of shem ya kwaaanika vigogo walificha pesa uswizi kuna tofauti gani na MSIBARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023
Saa 4:00 Asubuhi
Viongozi Mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wameanza kuwasili
Saa 5:45 Asubuhi
Mwili wa Marehemu Bernard Membe umewasili Karimjee ukiwa umebebwa kwenye gari Maalum la kubebea Maiti.
Saa 6:00 Mchana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan anawasili.
Rais Samia amekwenda moja kwa moja kusaini kitabu cha Maombolezo kilichoandaliwa, kisha kusalimia na kuwapa pole wafiwa.
Saa 6:05 Mchana
Dua na Sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini kisha salamu za viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wamekaribishwa kutoa salamu zao.
Zitto Kabwe anazungumza; Amemuelezea Bernard Membe kama Mwanasiasa mkomavu aliyepambana kulinda heshima yake dhidi ya watu waoga walioshindwa kumkabili kwa hoja, ambapo baadhi ya viongozi na Watu wenye Mamkala walitumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao.
Amesema Ushindi wake katika kesi ile utazika utamaduni huu mbaya wa kushambulia na kuchafua watu.
“Wewe sio tu ulizuia na kukemea upuuzi ule, bali ulihakikisha unatoa mfano kwa mpuuzi aliyebebeshwa upuuzi ule ili kuwa funzo kwa wapuuzi wengine wote”
Amesema kuwa anataraji wale wote waliohusika na mambo yale watamuomba radhi akiwa kwenye umauti.
View attachment 2621369
Zitto KabweAidha, amemsifu kwa kusimama imara katika nyakati ngumu ambazo taifa lilipitia, nyakati ambazo watu wengi waliogopa kuisimamia kweli.
Amemshukuru kwa kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo aliwapa mafunzo na kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii.
“Umetimiza wajibu, upumzike pema Membe… Tangulia BM, umeacha simanzi kubwa kwa watanzania. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Upumzike pema mzee wangu Membe” Zitto Kabwe
Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) anazungumza; Amesema Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa Masikitiko na Mshituko mkubwa kifo chake.
View attachment 2621375
Daniel Chongolo, Katibu Mkuu CCM
Amesema CCM imepoteza kada wake mkubwa, na amewaomba watanzania na wana CCM kuenzi mema yake kwa kusimamia maslahi ya watanzania ndani na nje ya nchi.
Stergomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anazungumza; Ametoa pole kwa mjane wa Marehemu pamoja na watoto kwa kuondokewa mpendwa wao.
Amesema wakati wa uhai wake alitekeleza kazi zake kwa weledi mkubwa hasa katika kukuza uhusiano mwema kati ya Tanzania na mataifa mengine ambao nchi imenufaika sana na kazi zake.
View attachment 2621403
Stergomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MasharikiAlichangia katika kujenga mipango mizuri kwenye sera za nje.
Amemshukuru Membe kwa kumtia Moyo wakati alipoteuliwa kugombea ngazi ya kimataifa ambapo alikuwa nae bega kwa bega kuanzia hatua za mwanzo na muda wote wa kazi.
Rais Samia Suhulu Hassan anazungumza; Amesema kifo ni jambo lisiloepulika kwa binadamu, na wote tumepokea kwa huzuni taarifa hizo za kifo cha Membe.
Serikali, Familia ya Rais na watanzania wote tunaungana kwa pamoja kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wanalindi wote kwa kumpoteza mpendwa wao.
View attachment 2621413
Samia Suhulu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaRais amemsifu kwa kuwa mtu muungwana na kaka wa karibu aliyekuwa tayari kusadia wengine. Amesema maamuzi ya Mungu huwa hayalaumiwi bali hushukuriwa.
Amemalizia kwa kuwaomba watanzania kumuombea Membe roho yake ipumzike kwa amani.
Nape Nnauye anazungumza; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza kwa niaba ya familia amemshukuru Rais Samia kwa kusimama bega kwa bega na familia ya Marehemu katika wakati huu mgumu ambapo gharama nyingi za msiba huu ikiwemo usafiri zimebebwa na Rais mwenyewe.
View attachment 2621415
Nape Nnauye anazungumza; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya HabariAmeishukuru Wizara ya Mambo ya nje kwa kuwabeba, kwa moyo wa upendo walioonesha. Heshima hii hawataisahau.
Amewashukuru viongozi wote wa Serikali na Mkoa, Madaktari wa Hospitali ya Kairuki, majirani, waombolezaji, ndugu, jamaa na marafiki wote kwa umoja walioonesha.
Saa 7:30 Mchana:
Jeneza linafunguliwa ili waombolezaji watoe heshima za mwisho. Rais Samia anawaongoza waombolezaji.
Saa 7:50 Mchana
Zoezi la kuaga limehitimishwa Rasmi.
Ile list of shame nayo ifutwe maana zitto mwembe yanga ndo alichafua akina rostam akina Patel kuwa wamefisha pesa uswizi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Great thinkers msituchekeshe bwana, aliyekwambia ana uchungu na membe nani?!!! Mbona ilionekana wazi kuwa anakerekwa na vikaragosi vinavyotumwa kuchafua watu!!!! Au wenzetu mnatumia akili ipi?!!!!! Zitto ni mmoja wa walioathirika na hali hiyo, musiba alimsingizia hadi kuwa anatembea na mke wa marehemu Filikunjombe
DaahHaya ndo madhara ya kuchelewesha kufukia hii mizoga
Nasikia kafika mwishoni kabisa!Hapana, kikwete ndiyo hatohudhuria kwa sababu "Maalumu"
Wwnasiasa ni wwnafiki sana aisee nakumbuka kipindi kile cha list of shameKuna mtu alikua anachafua watu Kama zitto kipindi cha JK? Umesahau zile nakala zake?
Zitto huyu kipindi lowassa ameanza mchakato wa kugombea huko ccm si ndio alikua akitumika sana kwenye magazeti kuandika nakala za kumponda lowassa?
Vipi Le Mutus na yeye alimcheka Magufuli?Alipanda chuki Kwa Nani na Kwa namna gani lazima muishe kwa Sababu ya laana ya kumcheka marehemu.