Zitto Kabwe: Membe alitupigania dhidi ya tabia Mbaya ya Watu wenye Mamkala kutumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao

Zitto Kabwe: Membe alitupigania dhidi ya tabia Mbaya ya Watu wenye Mamkala kutumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023



Saa 4:00 Asubuhi
Viongozi Mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wameanza kuwasili

Saa 5:45 Asubuhi
Mwili wa Marehemu Bernard Membe umewasili Karimjee ukiwa umebebwa kwenye gari Maalum la kubebea Maiti.

Saa 6:00 Mchana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan anawasili.

Rais Samia amekwenda moja kwa moja kusaini kitabu cha Maombolezo kilichoandaliwa, kisha kusalimia na kuwapa pole wafiwa.

Saa 6:05 Mchana
Dua na Sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini kisha salamu za viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wamekaribishwa kutoa salamu zao.

Zitto Kabwe anazungumza; Amemuelezea Bernard Membe kama Mwanasiasa mkomavu aliyepambana kulinda heshima yake dhidi ya watu waoga walioshindwa kumkabili kwa hoja, ambapo baadhi ya viongozi na Watu wenye Mamkala walitumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao.

Amesema Ushindi wake katika kesi ile utazika utamaduni huu mbaya wa kushambulia na kuchafua watu.

“Wewe sio tu ulizuia na kukemea upuuzi ule, bali ulihakikisha unatoa mfano kwa mpuuzi aliyebebeshwa upuuzi ule ili kuwa funzo kwa wapuuzi wengine wote”

Amesema kuwa anataraji wale wote waliohusika na mambo yale watamuomba radhi akiwa kwenye umauti.

View attachment 2621369
Zitto Kabwe
Aidha, amemsifu kwa kusimama imara katika nyakati ngumu ambazo taifa lilipitia, nyakati ambazo watu wengi waliogopa kuisimamia kweli.

Amemshukuru kwa kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo aliwapa mafunzo na kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii.

“Umetimiza wajibu, upumzike pema Membe… Tangulia BM, umeacha simanzi kubwa kwa watanzania. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Upumzike pema mzee wangu Membe” Zitto Kabwe

Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) anazungumza; Amesema Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa Masikitiko na Mshituko mkubwa kifo chake.

View attachment 2621375

Daniel Chongolo, Katibu Mkuu CCM

Amesema CCM imepoteza kada wake mkubwa, na amewaomba watanzania na wana CCM kuenzi mema yake kwa kusimamia maslahi ya watanzania ndani na nje ya nchi.

Stergomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anazungumza; Ametoa pole kwa mjane wa Marehemu pamoja na watoto kwa kuondokewa mpendwa wao.

Amesema wakati wa uhai wake alitekeleza kazi zake kwa weledi mkubwa hasa katika kukuza uhusiano mwema kati ya Tanzania na mataifa mengine ambao nchi imenufaika sana na kazi zake.

View attachment 2621403
Stergomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Alichangia katika kujenga mipango mizuri kwenye sera za nje.

Amemshukuru Membe kwa kumtia Moyo wakati alipoteuliwa kugombea ngazi ya kimataifa ambapo alikuwa nae bega kwa bega kuanzia hatua za mwanzo na muda wote wa kazi.

Rais Samia Suhulu Hassan anazungumza; Amesema kifo ni jambo lisiloepulika kwa binadamu, na wote tumepokea kwa huzuni taarifa hizo za kifo cha Membe.

Serikali, Familia ya Rais na watanzania wote tunaungana kwa pamoja kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wanalindi wote kwa kumpoteza mpendwa wao.

View attachment 2621413
Samia Suhulu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais amemsifu kwa kuwa mtu muungwana na kaka wa karibu aliyekuwa tayari kusadia wengine. Amesema maamuzi ya Mungu huwa hayalaumiwi bali hushukuriwa.

Amemalizia kwa kuwaomba watanzania kumuombea Membe roho yake ipumzike kwa amani.

Nape Nnauye anazungumza; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza kwa niaba ya familia amemshukuru Rais Samia kwa kusimama bega kwa bega na familia ya Marehemu katika wakati huu mgumu ambapo gharama nyingi za msiba huu ikiwemo usafiri zimebebwa na Rais mwenyewe.

View attachment 2621415
Nape Nnauye anazungumza; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Ameishukuru Wizara ya Mambo ya nje kwa kuwabeba, kwa moyo wa upendo walioonesha. Heshima hii hawataisahau.

Amewashukuru viongozi wote wa Serikali na Mkoa, Madaktari wa Hospitali ya Kairuki, majirani, waombolezaji, ndugu, jamaa na marafiki wote kwa umoja walioonesha.

Saa 7:30 Mchana:
Jeneza linafunguliwa ili waombolezaji watoe heshima za mwisho. Rais Samia anawaongoza waombolezaji.

Saa 7:50 Mchana
Zoezi la kuaga limehitimishwa Rasmi.
Zana Za kilimo Mbeya aliwahi kufanywaje na Joseph Pombe Magufuli? Manaake haishi kulalama kila anapopewa mic anabishana na kumshambulia aliyelala ambaye hata hawezi mjibu. Ila alipokua hai alipiga kimya. Coward
 
Huyo Zitto kutoa maneno hayo vepee?? Si aungane nae wakafukiwe wote huko Rondo km ana mkubali sana huyo marehemu.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nilikuwa namwangalia akitoa shombo zake huku uso umevimbiana kwa kubugia asali mpaka umekuwa wa mviringo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
CCM ukweli upo wazi na haupingiki mmemfanya vibaya kwenye historia ya marehemu Benard Membe kipengele cha siasa ,mmeshindwa kuelezea alihama CCM na kugombea Urais kupitia Act wazalendo, hivyo hivyo pia kwa msemaji wa familia

Zitto kabwe umefanya vizuri kuwakumbusha waweke record vizuri ya historia ya marehemu kupitia siasa , lakini kwangu mimi Zitto kabwe atabaki kuwa mwanasiasa mnafiki.
Unafiki ni moja ya tabia kuu kwa Spies..!!!..anaweza kuwa rafiki ili akakugeuka dkk yoyote ile

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Zitto Kabwe amemtaka Cyprian Musiba aombe msamaha, siyo tu atoe rambirambi, kwa sababu alimsakama Membe mpaka Membe akaugua. Ameleta usumbufu kwa Membe na pia kwa familia yake: kwa Cecilia, Richard na Dennis.
Zitto ana chuki nzito dhidi ya Musiba hadi ananunua ugomvi!

Musiba aombe radhi kwa lipi? Kwa sababu ya syndicate zilizopigwa kichinichini dhidi ya Musiba.? Nani alikuambia dhuluma hushinda au haki ya mtu hupotea daima.?

.Zitto amuombe radhi Maalim Seif kwanza kabla hajanyooshea vidole wengine.
 
Yeye Zitto amewahi kuwaomba msamaha wale aliotaka wakazikwe karibu na Magufuli?

Zitto anadai Musiba alimsakama Membe mpaka Membe akaugua?!, si tuliambiwa Membe alienda hospitali kwa "check up" ya kawaida tu, lakini kilichotokea baadae ndio mpaka madaktari wakashangaa!.

Huyu Zitto nilishamuona toka jana, amegeuza huu msiba wa Membe kama uwanja wa kutafuta "kick", japo kwa wengine anaonekana sio mnafiki, kwangu ni mnafiki tu.
 
Zitto ana chuki nzito dhidi ya Musiba hadi ananunua ugomvi!

Musiba aombe radhi kwa lipi? Kwa sababu ya syndicate zilizopigwa kichinichini dhidi ya Musiba.? Nani alikuambia dhuluma hushinda au haki ya mtu hupotea daima.?

.Zitto amuombe radhi Maalim Seif kwanza kabla hajanyooshea vidole wengine.
Zito ni lazima amchukie huyo mropokaji Musiba.

Kumbuka Musiba aliandika kwenye vile vigazeti takataka vyake kuwa Zito na maalim waligombania shoga! Maandishi kama yale nadhani yalikiwa yanadhihirisha kabisa kuwa Musiba alikuwa na uwendawazimu wa aina fulani.

Kama sasa hivi Musiba ana akili timamu, awaombe radhi, siyo familia ya marehemu tu, bali wote aliokuwa anawachafua. Awaambie tu kuwa alikuwa amepagawa na sasa akili yake imerudi.
 
Back
Top Bottom