Zitto Kabwe: Mwambieni Waziri Mkuu "Watu wake hawawezi kumpenda kama wana hofu ya kupigwa na kutekwa"

Zitto Kabwe: Mwambieni Waziri Mkuu "Watu wake hawawezi kumpenda kama wana hofu ya kupigwa na kutekwa"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


“Najua kuna Maafisa wa Usalama wa Taifa hapa kwenye Mkutano wetu Ruangwa, nawatuma wakamwambie Waziri Mkuu kuwa Zitto anasema maliza hofu Ruangwa.

“Watu wako hawawezi kukupenda kama wana hofu ya kupigwa na kutekwa kwa sababu tu wako vyama tofauti na wewe,” - Zitto Kabwe akiwa Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi.

Ameongeza kusema: "Nitamweleza Waziri MKuu Kassim Majaliwa kuwa kiongozi ukitaka kupendwa na kukubalika na watu wako, wasaidie kuwainua hali zao na sio kuwaburuza kwa mabavu na vitisho. Kufanya hivyo, kutakuchora kuwa kiongozi katili, watakuogopa na kukuchukia."
 
Zitto anamaanisha PM bado anaendelea na tabia za utekaji alizotoka nazo kwa mwendazake, anasahau wakati ule hata Samia alikuwa makamu wa Rais hivyo nae alikuwa akihusika, tatizo mahaba yanamfunga akili haoni hilo.

Alishasema hatampinga Samia, sasa atambue haiwezekani usimpinge kiongozi halafu uwapinge wasaidizi wake, huo ni ujinga kabisa, anachofanya hapo ni kumpinga Samia bila kujua, analeta habari za kutekwa ili kutafuta attention tu, halafu akienda kwenye mitandao anasema siku hizi hakuna kutekana, ili kumlinda Samia wake.
 
Haya mambo ya watu wasiojulikana si yaliisha kitambo? Kumbe huko kwingine bado yapo?
 
Ccm B wana lalamika kama wakaazi wa jiji la Dar na kero ya maji ya mgao Kama kipindi Cha ujamaa wa Nyerere bidhaa Kama mafuta, sukari,unga nk vilikuwa vya mgao
 
Katumwa akamchafue majaliwa ruangwa. Baada ya kuwaambia watu kuhusu tatizo la umeme, tozo na ubadhirifu uliokithiri ye anamchafua Majaliwa.

Majaliwa keshaifungua ruangwa. Kuna mahakama nzuri ya wilaya, hospitali mbili kubwa za wilaya, chuo cha veta, ofisi ya takukuru, magereza ya wilaya, duka la msd, ambulensi kila kituo cha afya, vituo vya afya vya kisasa vyenye vyumba vya operasheni kwa ajili ya wazazi, shule nzuri zenye tiles na madirisha ya aluminium, uwanja wa mpira, barabara za lami, taa za barabarani, benki za nmb na crdb.

NMB wana jengo la ghorofa ruangwa na wenyeji wanakuambia hawakutegemea kama ipo siku ruangwa kutakuwa na ghorofa. Na kuna hotel ya ghorofa tatu imejengwa.

Zitto kama ameenda kujenga chama chake ruangwa aachane na majaliwa ila kama kaagizwa na team msoga kwenda kutest mitambo dhidi ya majaliwa basi aendelee kufanya kazi aliyotumwa.
 
[emoji3][emoji3][emoji3] Zitto nadhani huu ni muendelezo wa ile twitter yako juu ya PM majuma yaliyopita, umeona haikufanya kazi umeona uende huko huko Jimboni kwake [emoji3][emoji3] chuki ni mbaya sana, either uwe umetumwa au la… Mwcheni huyu baba wa watu amsaidie Rais Samia kazi, kumvuruga mtendaji mkuu wa serikali ni kumvuruga Rais na mipango ya Serikali,
 
Back
Top Bottom