Zitto Kabwe: Mwambieni Waziri Mkuu "Watu wake hawawezi kumpenda kama wana hofu ya kupigwa na kutekwa"

Mugambo wanaruka na kukanyagana....ccm ya sasa ni bora kuliko ile ya akina Bashiru na Polepole.
Hata ile iliyomfia JK mkononi 2015 na watu wakawa hawavai nguo za ccm mtaani ilikuwa kama hii tu.
 
Zitto ni kijana ? Uwiii[emoji43][emoji43][emoji43][emoji43]
Kwenye siasa kijana anaishia 55yrs, kwenyw mpira 35yrs ni mzee. Ujana/uzee unategemea na career yako.
 
Kwani hajaona tatizo la vitu kupanda bei,umeme kukatika maji hakuna ila bili unaletewa ipo juu yeye kaona majaliwa tu ndo tatizo
 
Kwamba mabaya yanayotokea ni Waziri Mkuu wala Sio Rais ? Samia !!!

Ila kipindi kile Mabaya yote ni Rais wala sio Makamu !!!!

Huyu Jamaa yupo sawa kweli ?, au anadhani akili zetu tumemkabidhi ili atufikirie ?

Kwanini hizi sifa na lawama tunazigawa kwa mafungu mafungu na sio kuzipeleka moja kwa moja ? (Kama Waziri mkuu anafanya hayo na Rais yupo hakemei basi she is involved by turning a blind eye)
 
Majariwa alipora uchaguzi wa ruangwa wazi wazi..hawa ndio viongozi wa nchi ambao ni wezi..walaghai na wauaji.

Kazi ipo.

#MaendeleoHayanaChama
Majaliwa hana sifa kabisa ya kuwa kiongozi katika jamii iliyostaarabika, ni corrupt, mwongo, mchafu na kiongozi mwenye hila na uonevu.

Alimbambikia kesi yule mgomvea wa CHADEMA, akakamatwa ili yeye apite bila kupingwa. Ni wakala wa shetani. Ana tabia zote chafu.
 
Kwahiyo watu wasiojulikana sahizi ni kosa la waziri mkuu sio rais tena kama mlivyokua mnaaminisha umma 2021 kurudi nyuma? Mna nini na Majaliwa? Anakwamisha mambo yenu yepi? Mnadhani mnammudu?
Majaliwa anawateka wanawakomoa anaowahisi kuwa wanampenga yeye binafsi, siyo Serikali.

Kumbuka huyu Majaliwa ndiye aliyemteka mgombea wa CHADEMA wakati wa kipindi cha uchaguzi 2020, kisha alimbambikia kesi mgombea wa CHADEMA, yeye akatangazwa amepita bila kupingwa. Jamaa ni mchafu sana.
 
[emoji1787][emoji1787] Hapo kwenye ndege [emoji113][emoji113]

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Mchafu kwasababu unasema wewe? Una ushahidi wa aina yoyote wa hizo porojo zako? Wa kimandishi, picha, video au hata wa kimatukio tu? Una list ya watu wangapi 'waliompinga yeye binafsi' akawateka? Shea na sisi tuone
 
Kama yapi?
Wewe unaishi wapi?

Nani aliyemteka mgombea wa CHADEMA, kisha kumbambikia kesi, na kisha mkurugenzi wa Halmashauri kumtangaza Majaliwa amepita bila kupingwa?

Mwulize Majaliwa, yule mfanyabiashara aliyemhengea nyumba ya ghorofa kule Dodoma, ni fadhila ya nini?

Mwulize Majaliwa, kwa nini wakati Marehemu Magufuli akiwa katika kipindi cha mwisho cha kupigania uhai wake, yeye akawadanganya Watanzania kuwa Magufuli yupo ofisini anachapa kazi? Mtu mwongo anastahili kuaminiwa kwa lolote?
 
MAJALIWA anakula na waarabu wa OBC huku watanzania wakila nyasi
 
Kuna kipindi nyerere aliwahi kuwaita wanasiasa wa aina hii kuwa ni Malaya. Huyu ndumilakuwili ni wa kupuuzwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…