Zitto Kabwe: Ndoto yangu ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mwamsheni bwana Mwandiga jamani aache kuota asije akakojoa kitandani!!
 
Ule mkoa ulisahaulika sana! JPM kama alitaka kuukumbuka, lakini mtu kama Zitto anamponda?
 
Huyu atakuwa rais kama Mungu anao mpango wa kuliadhibu taifa hili la Tanzania. Wala hatapakwa mafuta atakuwa kama walivyokuwa wakina nebukaridezar au dario.

 
Zitto anasema ana uzoefu? Uzoefu gani? Ukimsikiliza vizuri utagundua anatamani madaraka ... ile hali ya kutukuzwa na siyo kubadilisha maisha ya Watanzania. Kama nchi tuna tatizo, maana kijana mdogo kama Zitto hajawahi kufanya kazi zaidi ya utalii wa kisiasa.
 
Ataambulia kura za akina Kuga, Spunda,Muttamwega na Dovutwa labda agombee kupitia ushirika wa vyama vyote vya upinzani.
 
Lini kama ni 2025 haiwezekani kwani chama chake kilisema kitafanya kazi na mama kwa miaka 9
 
AYATOLLAH ZITTO ZUBERI KABWE
Hapana mm ndo natatizo dogo,ila zitto iq yake ni njema ila msijali tunakajenga kaache ukigoma na kufake ,ila naapa Zitto is a deal,ngoja tukazungushe kagrow huyu anafaa
 
Sema kipenzi Chako,
Aliekwambia kwamba watu wote walimkubali mwendazake ni nani?
Binafsi hakupata kura yangu usitujumuishe
 
Reactions: Qwy
Mb
Mbona alisema atagombea 2015 akiwa CHADEMA? Huyo huwa anaangalia upepo. Kwa Sasa hata aligombea hawezi kushinda kwa sababu mvuto kwa watu umeisha.
 
Ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania anayejiona ana uwezo wa kutosha kiakili, kiafya na kiushawishi na aliyejiandaa vya kutosha kutamani kuwa Rais wa nchi siku moja.

Zitto Kabwe ni mtanzania na anaonekana kujipanga kwa lengo hilo tangu zamani.

Baada ya kuona amegundulika mapema mpango wake wa kufanya mapinduzi ya ndani ya CHADEMA ili awe na uwezo wa kujiamulia mambo mwenyewe kushindikana, akakimbilia kuanzisha chama chake.

Sasa njia ipo wazi kugombea atakavyo bila kuwa na mtu yeyote wa kumzuia ndani ya chama chake alichokiita ACT.

Aendelee na harakati zake japo wengi tunaona kuwa bado hajaweza kuwa na ushawishi wa kutosha kumfanya awe Rais wa nchi.
 
Kama anamchukia alokuwa Rais wetu kipenzi cha watanzania alotangulia mbele za haki Jemedari, Jembe, Jeshi (JPM), labda awe Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB)
Zito anakubalika sana huku kusini Lindi na Mtwara mtaji wa kuanzia anao haswaa na si wengine Bali ni sisi Wana korosho wa Kusini, tuna commonality flani Kati yetu wanakusini na Wanakigoma, kiufupi tuna historia ya kutengwa kwenye mikakati ya maendeleo kwenye hii nchi tangu ukoloni hadi uhuru.
 
Yupi aliyedai kuwa COVID 19 haukuwepo Tanzania? Huwa unafuatilia mambo kweli wewe? Kuna wakati ni bora kukaa kimya!
Sasa unataka tubishane juu ya hili pia? Muda huo huwezi kuutumia kufanya jambo jingine la maana?

Kwa hiyo wewe unajiona ni mfuatiliaji wa mambo, na kuelewa hayo unayofuatilia, au unaona maluweluwe ya kupoteza akili yako kwa kuwa chizi wa kutetea mtu mwingine bila hata kufikiri?
 
Hakuna mahali magufuli aliwahi sema corona haipo.

Alichokua anapingana nacho ni njia za kupambana nayo. Ambayo alikua sahihi.

Ambapo baada ya muda zimekuja kutumika na wengine.
Mkuu, hakuwahi kuwa "sahih"i kwa lolote.
Ni shukrani tu kwa Mwenyezi Mungu, katuepusha na janga. Hakuna ajuaye hadi sasa ilikuwaje nchi nyingi za kiafrika tuliponea chupuchupu. Huenda kuna siku tutajua, baada ya tafiti kufanyika.
Usitafute kumpa sifa ambazo hakuwa nazo kabisa, na zaidi ya yote, kiburi chake ndicho kikawa mwisho wake.

Bila COVID-19, leo hii akina Mbowe wangekuwa katika hali ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…