Zitto Kabwe: Sitagombea tena Uongozi ndani ya ACT WAZALENDO, najikita kwenye Ubunge. Malengo yangu ni kuwa Rais wa Tanzania

Yani ukisikia kinyonga mbadilika rangi ndio huyu. Katika watu wanafiki Tanzania huyu naye top 10 hakosekani. Lina tamaa mbaya sana. Useless kabisa
 
Ndio maana nikasema ninaamini. Kwa sababu huyo Zito na kundi lake lote waliohamia CCM akina Kitila, mwigamba, Mkumbo, mgwira nk. Waliposhindwa kuiangusha CHADEMA wakakimbilia CCM kupewa teuzi. Leo utaniamisha vipi kwamba ACT ni wapinzani?

..ACT wazalendo upande wa ZNZ wako vizuri, huku Tanganyika wako too weak.

..Waliohamia CCM walikata tamaa mapema kwa kumuogopa Magufuli.

..Magufuli angeendelea kuishi Tanzania ingerudi kwenye mfumo wa chama kimoja kimabavu.
 
au kurudi kwenye chama chako pendwa usichikitaja
 
1. ACT hawajapata walichotegemea kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

2. CDM hawajapata walichokitegemea kupitia mazungumzo ya maridhiano.

3. Wote wajipange upya na kuja na mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu.

1. Ni kawaida kupata matokeo yawe uliyotarajia au vinginevyo.

2. Labda hata sisi ni hivyo kwenye maridhiano katika degree tofauti.

3. Hapo #1 ipo kwenye mada kama #5:

Malalamiko yao kwenye "serikali yao ya nusu mkate Zanzibar" karidhika na alipofikia na yaliyopo ya nini kitafuata.

4. Wana malalamiko, ila hawajuti walipo. Tatizo letu Nini?

5. Hapo #4 huoni hizo ni pilipili tusizo zila?

6. Amesema:

"Hata hivyo anatambua siasa zake ni tofauti na za wengine, ambalo hilo ni suala binafsi."

Hudhani tungejikita zaidi kwenye kusaka yanayo tuunganisha badala ya kujikita kwenye yanayo tufarakanisha? Pa kuanzia pakikiwa: adui yetu ni mmoja?
 
Wewe ndiye humjui vizuri huyo zito. Ndimi ya kuwili mwenye macho ya tamaa ndiyo asili yake. He is a sweet talker and strategically conning.
 
CCM kawafanyia kazi nzuri, hivyo wameshamuahidi kumzawadia jimbo huko Kigoma kutokana na utii wake kwa mabwana zake.
Ndio maana hata Uraia hagombei 2025 usije kumuudhi mama, anapelekwa bungeni Kwa mbeleko ya CCM na mama iwe isiwe lazima atangazwe mshindi.
 
Ufukara wa mawazo ni kutokujikita kwenye mada na kuanza kushambulia watu. Akisema Nyerere, heri ufukara wa mali.

Tukianzia kwenu mnapenda kutudanganya kwenye siasa uchwara wakati malengo ni kula bila kutoa jasho.
 

..hapo kwenye " siasa tofauti " ndipo panapofarakanisha vyama vya siasa.

..Ccm inatumia " siasa tofauti " za vyama vya upinzani kuchelewesha mabadiliko tunayoyataka.
 
Mtu yupo hatua kumi mbele na ahead of time na chama kimemshinda kukisimamisha anataka kwenda kutetea tumbo lake na ubunge?

Ndio mtu gani huyo?

Acha kutudanganya wewe
 
Zitto namfahamu tangu anasaidiwa na Mbowe kwa kulishwa kutokana na umasikini akiwa Chuo kikuu na kuingizwa katika siasa kulelewa hadi kufanya maasi kutaka kumpindua Mbowe na hadi sasa.

Ninazifahamu sana na kuzishuhudia siasa za nchi hii kwa macho na akili yangu tangu Nyerere akiwa madarakani pengine wewe kibaraka wa Zitto haujazaliwa..
 
Na hapa bila shaka ndipo ule mwiba mchungu ulipo. Si Kwa makasiriko haya.

Al Watani, Bams, Mshana Jr
Zitto siyo centre ya siasa za Tanzania na hatakuja kuwa hivyo kiufupi he is a mere busybody.

Hata serikali haiwezi kujisumubua na ACT ambayo msingi wake unatiliwa mashaka na kila mtu hata Zitto mwenyewe.

Kuachia ngazi kwake au kubaki hakubadilishi chochote kwenye siasa za nchi.

Zitto siyo mwanzilishi wa ACT labda kama mnataka kusema alikianzisha akiwa bado yuko CDM kama alifanya hivyo ni mtu asiye na maadili na msimamo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…