Zitto Kabwe: Sitagombea tena Uongozi ndani ya ACT WAZALENDO, najikita kwenye Ubunge. Malengo yangu ni kuwa Rais wa Tanzania

Zitto Kabwe: Sitagombea tena Uongozi ndani ya ACT WAZALENDO, najikita kwenye Ubunge. Malengo yangu ni kuwa Rais wa Tanzania

Akiongea na redio hiyo ya kimataifa jana mchana, mwanasiasa huyo amefunguka:

View attachment 2933149

Kwamba:

1. Ameamua kunga'atuka kwa mujibu wa katiba akikiacha chama kikiwa katika hali bora zaidi kuliko wakati wowote.
2. Hatarejea kwenye uongozi wa chama hicho kama katiba inavyotaka, kwani muda wake umekwisha; bali atasalia kuwa mwanachama.
3. Anayo imani kubwa na waliochukua hatamu za uongozi na kuwa hana shaka, chama kipo katika mikono salama.
4. Mzee Duni kujitoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi, hakukuwa na shinikizo lolote.
5. Malalamiko yao kwenye "serikali yao ya nusu mkate Zanzibar" karidhika na alipofikia na yaliyopo ya nini kitafuata.
6. Kuwa anapanga kurejea bungeni agombee 2025.
7. Chama kikimhitaji kwa ushauri au kushiriki vikao yuko radhi.
8. Anazo ndoto za urais wakati wake ukifika, na hasa 2030 na huko mbele lakini si 2025.
9. Anaamini kwenye siasa za kuleta mabadiliko; kuwa hizo ziko bungeni.
10. Anatambua mbunge aliyepo Kigoma ni aliyetangazwa tu, lakini siyo aliyeshinda.
11. Kuhusu uchaguzi 2025 kuwa huru na haki; anaamini mazingira yatakuwa bora zaidi 2025, kwani 2020 yalikuwa mabaya mno na kuwa heri tungerejea hata kwa yaliyokuwa 2015.
12. Mabadiliko yaliyopo sasa kuwa hakuna kupita bila kupingwa, wenyeviti na makamu watapatikana tokea kwenye mchakato wenye usaili wa waombaji, nk yanatia moyo.
13. Kuhusu madai ya u CCM B wake; hajawahi kuwa CCM, amekuwa upinzani muda wote, hajawahi kuunga mkono juhudi. Hata hivyo anatambua siasa zake ni tofauti na za wengine, ambalo hilo ni suala binafsi.

Maneno kuntu kabisa kutoka kwake Zitto Zuberi Kabwe.

Kwa hakika kama asemavyo Prof. Lwaitama adui yetu ni mmoja:

Lwaitama: Kwenye maslahi ya nchi, adui yetu ni CCM
Haaminiki kama Lipumba
 
..hapo kwenye " siasa tofauti " ndipo panapofarakanisha vyama vya siasa.

..Ccm inatumia " siasa tofauti " za vyama vya upinzani kuchelewesha mabadiliko tunayoyataka.

1. Hatuwezi kuwa sawa kama watoto mapacha ndiyo maana hata kwenye maridhiano tulikuwa na maoni tofauti:

2. Hapo namba #1 Mandela alitembea na Buthelezi. Wala hatujishangai sisi tunakwama wapi?

3. Kwenye hili wakulaumiwa ni sisi wenyewe, CCM tutamsingizia bure.

4. Hapo #3, kwani Mbeya ya zama zile ilikuwaje?

5. Kitulacho kinguoni mwetu tuko kama tunadhani kuna ustaa kwenye ukombozi:

6. Hapo #5 huku kutojua umoja ni nguvu kunayapa ma CCM jeuri ya kuendelea kutung'ong'a hadharani ikiwamo matamshi yao ya kutawala milele.

7. Tuko kama tumerogwa, siyo bure!
 
Ndiyo msingi wa chama chake

1. Misingi ya chama chochote cha siasa Iko kwenye katiba yao ambayo huwasilishwa kwa msajili Kwa uhakiki kabla ya usajili.

2. Wenye chama chao hawajasema popote kuwa chama chao ni cha kidini.

3. Mandela alitembea na kina Buthelezi wakachukua nchi.

4. Ajabu na kweli haijulikani tunataka kuichukua nchi na mawazo kama haya.

5. Prof Lwaitama huwa tunamwelewa kweli?
 
Zitto siyo centre ya siasa za Tanzania na hatakuja kuwa hivyo kiufupi he is a mere busybody.

Hata serikali haiwezi kujisumubua na ACT ambayo msingi wake unatiliwa mashaka na kila mtu hata Zitto mwenyewe.

Kuachia ngazi kwake au kubaki hakubadilishi chochote kwenye siasa za nchi.

Zitto siyo mwanzilishi wa ACT labda kama mnataka kusema alikianzisha akiwa bado yuko CDM kama alifanya hivyo ni mtu asiye na maadili na msimamo.

1. Kuzungumza center wa siasa, labda unazungmzia u Messi, Ronaldo nk. Yaani ustaa.

2. Au unamaana kumbe center wa siasa za Tanzania siyo mwananchi?

3. Tuweke egoism pembeni hii nchi tulipaswa kuichukua tokea 1995 huko.

4. Ubinafsi umetufikisha wapi?

5. Tungeacha hii ya kuwa mahakimu, mashahidi na ma prosecutor wenyewe.
 
Kwanza hawa watu ni wajinga wa Kiswahili. Kiongozi anayemaliza muda wake wa uongozi kikatiba, hang'atuki bali amemaliza kipindi chake cha uongozi. Hawa watu wamejaa unafiki.

Nyerere kuachia uongozi ilikuwa issue ya kuongelewa sana kwa sababu aling'atuka. Mwinyi kuachia uongozi ilikuwa kawaida, kwa sababu alimaliza kipindi chake cha uongozi kikatiba.
Yaani Nyerere kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 ndo asifiwe eti aling'atuka!
Tena baada ya nchi kumshinda!!
 
Sisi tusio Zito wala Lipumba

1. Si unaujua ule msemo pendwa kuwa nyani haoni kundule?

2. Kwa mujibu wa nani au kipimio gani, haKuna.

3. Ila tu kwa kuwa wewe ndiwe jaji, prosecutor na shahidi na kuwa hukumu yako ndiyo tuikubali tu?

4. Kuwa wala hujishangai?
 
Mtu yupo hatua kumi mbele na ahead of time na chama kimemshinda kukisimamisha anataka kwenda kutetea tumbo lake na ubunge?

Ndio mtu gani huyo?

Acha kutudanganya wewe

Kwa hiyo angekomaa kitini ndiyo ingekuwa sawa?
 
Akiongea na redio hiyo ya kimataifa jana mchana, mwanasiasa huyo amefunguka:

View attachment 2933149

Kwamba:

1. Ameamua kunga'atuka kwa mujibu wa katiba akikiacha chama kikiwa katika hali bora zaidi kuliko wakati wowote.
2. Hatarejea kwenye uongozi wa chama hicho kama katiba inavyotaka, kwani muda wake umekwisha; bali atasalia kuwa mwanachama.
3. Anayo imani kubwa na waliochukua hatamu za uongozi na kuwa hana shaka, chama kipo katika mikono salama.
4. Mzee Duni kujitoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi, hakukuwa na shinikizo lolote.
5. Malalamiko yao kwenye "serikali yao ya nusu mkate Zanzibar" karidhika na alipofikia na yaliyopo ya nini kitafuata.
6. Kuwa anapanga kurejea bungeni agombee 2025.
7. Chama kikimhitaji kwa ushauri au kushiriki vikao yuko radhi.
8. Anazo ndoto za urais wakati wake ukifika, na hasa 2030 na huko mbele lakini si 2025.
9. Anaamini kwenye siasa za kuleta mabadiliko; kuwa hizo ziko bungeni.
10. Anatambua mbunge aliyepo Kigoma ni aliyetangazwa tu, lakini siyo aliyeshinda.
11. Kuhusu uchaguzi 2025 kuwa huru na haki; anaamini mazingira yatakuwa bora zaidi 2025, kwani 2020 yalikuwa mabaya mno na kuwa heri tungerejea hata kwa yaliyokuwa 2015.
12. Mabadiliko yaliyopo sasa kuwa hakuna kupita bila kupingwa, wenyeviti na makamu watapatikana tokea kwenye mchakato wenye usaili wa waombaji, nk yanatia moyo.
13. Kuhusu madai ya u CCM B wake; hajawahi kuwa CCM, amekuwa upinzani muda wote, hajawahi kuunga mkono juhudi. Hata hivyo anatambua siasa zake ni tofauti na za wengine, ambalo hilo ni suala binafsi.

Maneno kuntu kabisa kutoka kwake Zitto Zuberi Kabwe.

Kwa hakika kama asemavyo Prof. Lwaitama adui yetu ni mmoja:

Lwaitama: Kwenye maslahi ya nchi, adui yetu ni CCM
Ameshafanyiwa lobbying ya Ubunge jimboni kwake !
Kura zitatosha tu iwe jua iwe mvua !
Zisipotosha zitatosheshwa ! 🙏🙏😅😅 !
 
Yani ukisikia kinyonga mbadilika rangi ndio huyu. Katika watu wanafiki Tanzania huyu naye top 10 hakosekani. Lina tamaa mbaya sana. Useless kabisa

Nguli Prof. Lwaitama hakubaluani nawe:

Ninakusoma kwa msisitizo huu bila shaka mada imekugusa negatively. Ajabu na kweli. Ninadhani ni muhimu kutafakari ni kwa nini hasa?
Ambacho kimefanya nikupe Kongole, pamoja na kuweka Video lakini bado ukatuandikia kwa ufupi yale Zitto aliongea. ..

Hongera tena.
 
Back
Top Bottom