Itakua wote wameamua kumuunga mkono Lisu.
Tuna bahati kumpata mgombea mashuhuri dunia nzima. Sio vijijini sio mijini.
Lisu aje tu na Sera bora za Elimu, afya, uchumi,kilimo , Elimu, ajira na miundo mbinu lakini pia namna bora ya kutumia vyombo vyetu vya dola kwenye kusimamia amani ya nchi na kuimarisha uzalishaji kwa kutumia majeshi yetu wakati wa amani.
Vipi Lisu atatoa amri kama amiri jeshi mkuu bila kuathiri vyombo hivyo kujipendekeza kwa wanasiasa lakini pia kwa wakubwa zao ambao nao wanateuzi za ndani kwa ndani?
Katiba iliyopo ikitumiwa kisawasawa inatengeneza udikteta; Vipi Lisu ataitumia katiba ilitopo kufanya mabadiliko bila kuwa dikteta kwa kiasi Fulani?
Je, Lisu akiingia madarakani octoba ,halafu CCM wakajaa barabarani kupinga matokeo yake kwa maandamano makubwa atawaruhusu kufanya hivyo kwa sababu ya Uhuru wa kuandamana?
Bila shaka wapinzani wajipange kwa hoja kampeni zikianza mana wananchi wamesharidhika na hali iliyopo na wanaona ni sawa na hakuna hali bora kuliko hii na wanaamini hata wale wanaogawa mapesa barabarani nao pia wana maisha magumu kama wao na ni haki yao kuwagawia wale wanaowataka bila kufanya kazi lakini wengine wanaambiwa hakuna kula bila kazi.
Je, watanzania shida yao kubwa ni Uhuru tu wa mikutano ya kisiasa na kuandamana??