Uchaguzi 2020 Zitto: Mgombea atakuwa mmoja kati ya CHADEMA na ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Zitto: Mgombea atakuwa mmoja kati ya CHADEMA na ACT Wazalendo

Hili taifa lina 50+ years toka lipate uhuru watu aina ya lissu na wenzake walikuwepo toka enzi hizo na walishindwa kufanikiwa na agenda zao za hovyo hovyo na mwaka huu 2020 wataisoma namba kisawasawa
Ushauri wetu kwenu mataga mjiandae mapema kisaikolojia kuwa chama cha upinzani na ndugu zenu kina TLP na CUF ya lipumba
 
Toka mfumo wa vyama vingi uanze, mwaka huu ndo ccm inakwenda kukabiliana na wagombea wa upinzani yaani lissu & mwalimu maana hawana historia ya ukada wa ccm katika maisha ya siasa. Hivyo kama ni kuiondoa basi ni mwaka huu tofauti na hapo hakuna. Kwanza zanzibar kule ACT wako vizuri na watashinda kwa kishindo kikuu maana aliyepitishwa upande wa pili siyo chaguo lao kiuhalisia.
Zanzibar huko ccm ashanawishwa mapema hata kabla ya kumwaga zege lenyewe
 
ACT hawana impact yoyote Tanzania bara, waachwe wapige mechi yao kivyao.
 
Hatutaki kupiga kura siku moja kabla, yale yale ya 2015 ya kuelekezwa tuandike namba zetu za vitambulisho vya kupigia kura, siku ya kupiga kura unaenda kupiga kura unaambiwa tayari ulishapiga.

Kwa wingi wetu polisi na jeshi la wananchi tunasema Sasa hivi hatutaki maelekezo, tunasimamia sheria, kanuni na taratibu za kazi!

Hatuwezi kuwadhulumu ndugu zetu watanzania kisa kulinda maslahi ya watawala, watanzania ni ndugu zetu, tupo nao pamoja!

Hata 2015 tulisimamia uchaguzi na bado kura tulipiga(kwa wale tuliokaidi maelekezo ya kuandika namba za vitambulisho), sasa mwaka huu kimebadilika nini hadi tupige kura siku moja kabla?

Elfu 60 za kusimamia tutazichukua, Watanzania watapiga kura, hakuna figisu itakayotokea vituoni, nyeusi itaitwa nyeusi, nyeupe itaitwa nyeupe,

#MAAGIZOKUTOKAJUUSASABASI!!
Mgambo katika ubora wako [emoji16][emoji16][emoji16]
Lakini kumbuka kazi yako ni kukamata mkaa, hii kazi nyingine utachoka sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jipeni matumaini chama cha mjini wakati wapiga kura wako vijijini, sana sana mtaishia kufanya vurugu mnakutana na mkono wa dola ulio madhubuti.
Huko vijijini watu wame chukia mbaya, bei ya mazao hakuna mbaazi ilikuwaTshs 250,000/= sasa hivi ni Tshs 50,000/= korosho hoi, kahawa hoi!!
Nani ataendekeza huo ujinga, MaCCM hawana pa kushika!!
Ahadi ya Tshs 50,000,000/=
kila kijiji ni hewa, ujinga utaisha safari hii!!
 
Sheria na kanuni za kampeni zinakataza lugha zisizo za kiustaarabu wala staha, lugha zisizo na heshima kwa wagombea wenzako wala kwa mamlaka halali za nchi, lugha za matusi, za uwongo, za kuchochea vurugu, za ukali, lugha zilizo kinyume na maadili mema ya mtanzania ambazo watoto na vijana hawapaswi kuzisikia toka kwa watu wazima.

Tundu Lissu ukimuzuia kuongea lugha hizo atakuwa bubu kwani ndizo lugha pekee anazozijua.

Wananchi wanachotaka kusikia kutoka kwa mgombea urais ni vitu ambavyo mgombea atawafanyia wananchi na taifa kwa ujumla wakimuchagua kuwa rais wao ili kipata maendeleo. Na mambo haya ayaseme kwa lugha ya staha yenye kuwashawishi waamini anasema kweli na wakimuangalia macho yake waamini anasema ukweli.

Mgombea anapaswa kuyaelewa matatizo makuu ya msingi ya taifa letu yanayokwamisha maendeleo ambayo ni:
1. Neocolonism (Ubeberu). Maliasili na utajiri wetu zimeendelea kuporwa kwa wingi kwenda kiendeleza mataifa ya Ulaya, Asia na Amerika. Waporaji hawa (mabeberu) tumekuwa tukiwaita wawekezaji wamekuwa wakitupoza kwa tu misaada midogo midogo.
2. Rushwa
3. Utegemezi
4. Kutojiamini kuwa tunaweza

Huyu jamaa kwa kuwa hakuwapo nchini kwa miaka mitatu hajui hata mambo ambayo tayari yameshafanyika. Hususani jana kwenye sikukuu ya wakulima alizungumzia usumbufu wa kodi na mambo mengine mbali mbali waliyokuwa wakiyapata wakulima njiani wakisafirisha mazao yao. Hajui kwamba kodi hizo na usumbufu huo wa njiani JPM alisha ukomesha zamani. Itamchukua si chini ya miezi 6 kuyajua yote yaliyotendeka katika kipindi hicho cha miaka 3 alichokuwa hayupo maana mengi sana.

Jamaa huyu anapinga ujenzi wa bwawa kubwa kuliko yote Afrika la kuzalisha umeme la Nyerere (Stiegler's) kwa kuwa tayari tunayo mabwawa ya Mtera na Nyumba ya Mungu. Hivyo anaungana na hao mabeberu waliokuwa wakipinga kwa nguvu zote ujenzi wa bwawa hilo. Ikatulazimu tulijenge kwa pesa zetu wenyewe.

Jamaa anafikiri kuwa nchi kuwa na deni la mikopo kubwa kwake ni tatizo. Hajui kuwa hayo ndiyo maendeleo. Nchi jajiri ndizo zinazoongoza kwa ukubwa wa madeni ya mikopo. Hata watu majiri wana madeni makubwa ya mikopo. Masikini huwezi kuwa na madeni makubwa, kwanza hakuna atakayekukopesha kwani anajua hutaweza kurudisha mkopo. Masikini hakopesheki. Tajiri ndiye anakopesheka. Dunia imetutambua sisi ni matajiri wa kiwango cha middle income country. Hivyo madeni ya mikopo lazima yakuwe.
Unaonekana wewe ni mtu wa Ikulu uko kwenye keyboard yaliyoko field huyajui!!
Nenda Makuyuni au kwenye vituo ya mizani uone watu wanavyo nyanyaswa ba kodi za ajabu!!
Hujui kinacho endelea!!
 
Kila kitu kinawezekana iwe baada au kabla, MMOJA kati yao anaweza kuachia ngazi muda wowote akasema anajitoa katika kinyang'anyiro cha urais na kuunganisha nguvu kumpigia kampeni MMOJA.
Kwa utaratibu hilo linawezekana lakini KIUHALISIA kwa vile kila mmoja kati yao wanavyoutaka huo urais ni vigumu sana kwani kuna maslahi binafsi ya wagombea na maslahi ya wapiga ngoma wao kutoka nje hasa hasa wale wanao wafadhili. Hiyo ndio hali ilivyo utake usitake.
 
Lowasa si ni kweli alikuwa mgonjwa wakati wa kampeni za 2015? Hakukuwa na uwongo kwenye hilo. Wapiga kura ilikuwa ni haki yao kulijua hilo kabla ya kutoa maamuzi ya raisi wamtakaye. Na Lissu pia anapaswa ajiandae kwa hizo ndogo ndogo za ukweli kuhusu afya yake physically and mentally kutoka kwa wapiga debe wa mpinzani wake. Ni dosari ambazo wananchi wanapaswa kuzijua kuhusu rais wanayetaka kumchagua. Ni lazima wajue kuwa huyo rais wao ana ulemavu wa kudumu wa miguu na mikono yake. Mguu wake wa kulia na mkono (hand) wake wa kulia hawezi kuukunja. Wananchi wanatakiwa kujua kuwa huyo rais wao hataweza kumudu mikiki mikiki ya kazi hiyo ya urais ikiwemo ya kuweza ku escape matukio hatarishi na kadhalika.

Wananchi wanapaswa kujua kuwa rais huyo watakayemchagua ana some permanent damage to some parts of his brain ganglias iliyosababishwa majeruhi aliyoyapata kwenye hilo shambulio la risasi 36 huko Dodoma 2017. Madhara haya ya anoxic permanent suprantentorial brain damage akiwa rais yanaweza kuathiri maamuzi yake katika baadhi ya maamuzi yake muhimu kwenye mambo ya uendeshaji wa nchi yetu. Haya ni mambo ambayo wapiga debe wa mpinzani wake wanapaswa kuwataarifu wananchi kwa lugha ya nyepesi nyepesi yenye ustaarabu ili wachague kitu wanachokijua.

Ni haki yao wapiga kura kujua kabla kwamba huyo watakayemchagua lazima atatumia kiasi kikubwa cha pesa za walipa kodi na muda mwingi wa kipindi chake cha urais kugharimia kujaribu kukarabati afya yake huko nchini kwa mabeberu. Hivyo miaka kadhaa (kama mitatu) atakuwa Ubelgiji kurekebisha miguu na mikono yake. Hata mwenyewe alishakiri na kusema kwamba madaktari wake walikuwa wamepanga kuuvunja upya huo mfupa wa mguu wake na kuuwekea antenna tena. Akawajibu,'Ngoja kwanza nirudi nyumbani nikagombee urais, nitarudi kuendelea na matibabu nikiwa rais na uwezo zaidi wa kulipia gharama yo yote ya matibabu'.

Ni haki ya wapiga kura kuyajua haya kuhusu wagombea wao wa urais kabla ya kufanya maamuzi kwenye sanduku la kura. Hii ndiyo kazi ya wapiga debe wa mpinzani wake katika kampeni hizo za uchaguzi. Wakina Msukuma na Bajaji wataziongea kwa mafumbo mafumbo yenye staha ya utu wake. Wataongea kwamba huyo jamaa ana mavyuma kibao mwilini mwake ambavyo ndani yake vimepandikizwa vyombo vya mawasiliano po pote alipo na station mbali mbali za mabeberu. Hivyo akiwa rais wa nchi yetu, mabeberu hao wataona na kusikia cho chote ambacho rais wetu atakuwa anasema au anafanya. Yaani hakutakuwa na siri wala salama kwa mabeberu (waporaji) wa nchi yetu. Nchi yetu itakuwa closely monitored na hawa mabeberu.

Hii ndiyo maana ya kampeni. Wagombea wana maximize weakness za mpinzani wao na kuzieleza kwa wapiga kura kwa lugha nyepesi nyepesi zisizokuwa na mauzi wala uwongo wo wote ili kuwashawishi wasimpe kura huyo mpinzani wao. Watawaeleza strengths za mgombea wao vs mpinzani wao ili wampe kura mgombea wao. Ndiyo maana ya kampeni.

Sasa huyu jamaa ku prove brain ganglias damage alizozipata anakuja na weakness za JPM kuwa ni kujenga bwawa la umeme la Mwl. Nyerere,, kununua ndege 11 kwa cash, kutumia matrillion ya pesa kujenga SGR, ma fly overs kila mahali nchini, maviwanja ya ndege kila mkoa hadi mkoa wa Geita huko Chato, Stieglers hydroelectric dam, kupanua bandari ya Dar na Mtwara, kutengeneza meli zaidi ya 20 kwenye ziwa la victoria, nyasa na tanganika, mashule kibao, hospitali na vituo vya afya kibao nk. Eti haya ni weakness za mpinzani wake kwani ni maendeleo ya vitu badala ya watu. Eti yeye atawaletea maendeleo ya watu kuweza kuandamana wakati wo wote na mahali po pote, watu wataweza kuropoka na kuandika au kurusha mtandaoni na kwenye television cho chote wanachojisikia hata kama ni masuala ya ushoga, ngono na kadhalika. Hizi ndizo strength zake.
Hiyo ndio kampeni hata ukimsikiliza huyo wa USA naye huwa anawananga sana wapinzani wake watarajiwa kwenye uchaguzi uliopita na huu ujao. Na hizo ni dalili wazi wazi za KUKOSA HOJA MADHUBUTI. Hivyo njia rahisi ni kukimbilia aidha kwenye VIOJA NA VIHOJA au kupersonalise campaigh na kusema ya binafsi ya mpinzani wako. Huu kwa kifupi ni UANAHARAKATI siyo UANASIASA!
 
Kuota ni haki yako
Narudia, sio chadema wala act au hata waungane wote. Hakuna upinzani wa kuitoa ccm madarakani?. Mara 1000 ingelikua kipindi kile cha mzee lowassa ningeamini kidogo lakini alishindwa.
Ninyi mkipata mbunge hata mmoja mutakua mumejitahidi sana.
 
Back
Top Bottom