Hatutaki kupiga kura siku moja kabla, yale yale ya 2015 ya kuelekezwa tuandike namba zetu za vitambulisho vya kupigia kura, siku ya kupiga kura unaenda kupiga kura unaambiwa tayari ulishapiga.
Kwa wingi wetu polisi na jeshi la wananchi tunasema Sasa hivi hatutaki maelekezo, tunasimamia sheria, kanuni na taratibu za kazi!
Hatuwezi kuwadhulumu ndugu zetu watanzania kisa kulinda maslahi ya watawala, watanzania ni ndugu zetu, tupo nao pamoja!
Hata 2015 tulisimamia uchaguzi na bado kura tulipiga(kwa wale tuliokaidi maelekezo ya kuandika namba za vitambulisho), sasa mwaka huu kimebadilika nini hadi tupige kura siku moja kabla?
Elfu 60 za kusimamia tutazichukua, Watanzania watapiga kura, hakuna figisu itakayotokea vituoni, nyeusi itaitwa nyeusi, nyeupe itaitwa nyeupe,
#MAAGIZOKUTOKAJUUSASABASI!!