Zitto: Msaidizi wa Maalim Seif alinipigia simu mara 4 kutaka kunijulisha msiba sikupokea ndipo akanipigia Rais Mwinyi nikapokea kwa mujibu wa sheria

Kwani kuna tofauti na wale wanaojiaminisha kwamba tatizo lipo wakati halipo ?

Wanasiasa wote ni walewale, By the way karne hii kiongozi anachohitaji ni Diplomasia, hio ni maradufu ya ubabe....
 
Hivi Kuna sheria inayohusiana na kupokea simu za viongozi?
 
Kuna mtu alimwaga chozi kwenye msiba wa Mkapa pale uwanjani
Kumwaga machozi na kuogopa kupokea sim havifanani
Hata mwenye furaha anaweza kumwaga machozi kama ilivyo kwa mwenye huzuni, hilo ni tendo lisilo la hiari
 
Acha kuleta bla bla hapa,msiba na machozi ya furaha wapi na wapi?
 
Wapi na wapi kuweza kuwa kiongozi na kushtushwa ama kuogopa msiba?

Zitto ni mwanadamu kama wewe na mimi na hata rais wako Magu mara kadhaa ukitokea msiba huandika 'kashtushwa' mana hili ni jambo ingawa ni la haki lakini kuns pazia nene lilopo kutokujua nani na lini na wakati gani atafariki ndio mana mwanadamu akipata taarifa ya fulani kafa hushtuka na kuogopa hasa kwa mtu uliyemfahamu na kumjua zaidi wa karibu yako, Quran tukufu sisi waislamu imekuwa ikituasa mara kadhaa kuogopa mauti na kututaka tutende mema ili tupate msaada wa Mungu siku ya siku.

Ndio mana kabla sikutaka kukujengea hoja kwamba haikuwa matumaini yangu kwa hata hili la muumba hulifahamu wala sikutegemea kwamba ungekuwa hufahamu chochote kuhusu mauti/kufa.
Mbona simu ya Rais Mwinyi aliipokea wakati maudhui ni yale yale?

Ila nimekuelewa sana bwashee!
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema siku maalim Seif alipofariki yeye alikwenda hospitali asubuhi na kuelezwa maendeleo ya mgonjwa.

Anasema ilipofika saa 5 na ushee akiwa katika shughuli za chama alipigiwa simu na msaidizi wa maalim Seif aliyekuwa anashinda pale hospitali na hakuipokea.

Akapiga tena mara tatu zaidi lakini Zitto hakupokea kwa sababu alijawa na uwoga na hakuwa tayari kupokea habari mbaya kwa wakati huo, anaeleza Zitto.

Baadae kidogo nikapigiwa na mh Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ndipo kwa mujibu wa sheria ikanibidi nipokee na akanijulisha habari za msiba na tukakubaliana alitangazie taifa kisha nasi kama chama tukatangaza baada ya tangazo la serikali, amemalizia Zitto Kabwe.

Chanzo: Clouds TV

My take: Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Maendeleo hayana vyama!
Ukimuamini M Mungu unayaelewa kabisa maneno ya Zitto, lakini ukiwa na akili ya kibinaadamu tu ni vigumu kuelewa maelezo yake.

Nakumbuka mtangazaji wa CNN akimhoji mwanasaikolojia maarufu akifanya kazi CIA (shirika la kijasusi marekani). Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwashawishi watekaji wa ndege/watu wabadili mawazo yao na waweke silaha zao chini ili wajisalimishe. Alimuuliza swali moja linalolingana na hilo: " Inakuwaje mnapoteza muda kuwashawishi watekaji ambao wameshadhamiria kufa na wapo tayari kwa lolote wajisalimishe?" Jibu lake alisema: Katika kila dakika mioyo yao inaweza kubadili mawazo na kufikiri pengini siku yangu ya kufa sio leo na wakasubiri kesho yake au siku nyingine.

Ninachotaka kukueleza ni kuwa hata huyo afisa wa CIA akikutwa kisawasawa moyo wake unaweza kuwa mlaini kuliko wako, na ukashangaa hivi aliwezaje kupata nafasi kubwa kama hiyo!

Kifupi mwanadamu yeyote jinsi M Mungu alivyomuumba, moyo wake ni dhaifu kweli kweli kuliko unavyofikiria wewe. Lakini kulifahamu hilo inabidi umjue M Mungu.
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema siku maalim Seif alipofariki yeye alikwenda hospitali asubuhi na kuelezwa maendeleo ya mgonjwa.

Anasema ilipofika saa 5 na ushee akiwa katika shughuli za chama alipigiwa simu na msaidizi wa maalim Seif aliyekuwa anashinda pale hospitali na hakuipokea.

Akapiga tena mara tatu zaidi lakini Zitto hakupokea kwa sababu alijawa na uwoga na hakuwa tayari kupokea habari mbaya kwa wakati huo, anaeleza Zitto.

Baadae kidogo nikapigiwa na mh Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ndipo kwa mujibu wa sheria ikanibidi nipokee na akanijulisha habari za msiba na tukakubaliana alitangazie taifa kisha nasi kama chama tukatangaza baada ya tangazo la serikali, amemalizia Zitto Kabwe.

Chanzo: Clouds TV

My take: Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Maendeleo hayana vyama!
Zitto bado kijana mdogo, msimshambulie sana..
 
Mungu huwa anatuepusha mengi sana,

ile nafasi ya Urais huwa sio kwa kila mtu,

Ni Mungu pekee ndiyo anampa anayeona anafaa,
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema siku maalim Seif alipofariki yeye alikwenda hospitali asubuhi na kuelezwa maendeleo ya mgonjwa.

Anasema ilipofika saa 5 na ushee akiwa katika shughuli za chama alipigiwa simu na msaidizi wa maalim Seif aliyekuwa anashinda pale hospitali na hakuipokea.

Akapiga tena mara tatu zaidi lakini Zitto hakupokea kwa sababu alijawa na uwoga na hakuwa tayari kupokea habari mbaya kwa wakati huo, anaeleza Zitto.

Baadae kidogo nikapigiwa na mh Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ndipo kwa mujibu wa sheria ikanibidi nipokee na akanijulisha habari za msiba na tukakubaliana alitangazie taifa kisha nasi kama chama tukatangaza baada ya tangazo la serikali, amemalizia Zitto Kabwe.

Chanzo: Clouds TV

My take: Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Maendeleo hayana vyama!
Muha kweli muha,kwa kupenda sifa, zamani Waha utawasikia ukiwe kwenye treni usiinite Kalumanzira niite braza K.
 
Kiongozi ambaye hasikilizi wasaidizi🤔🤔🤔🤔
Kutopokea sim ya msaidizi wa maalim seif ni dharau. Sijui kama za wasaidizi wengine na wananchi zinapokelewa
Hapo hajakua raisi.
 
Back
Top Bottom