Kwa vyovyote vile itakuwa, kwa mazingira yeyote yale yatakuwa, ni muhimu na lazima Vyama makini vya Upinzani kuweka Mgombea mmoja wa Urais wa Muungano, Urais wa Zanzibar, Kila Jimbo la Uchaguzi la Ubunge na Uwakilishi na kila Kata ya Udiwani. Nimezunguka Vijijini, CCM INANG’OKEKA-Zitto Kabwe on twitter.
Maweee.......eti CCM inang'okeka....
ZZK anaendeleza porojo zake KONGWE.......
Lengo lake si URAIS.....
Lengo lao si URAIS......
Hawana lengo la kupata urais BARA.....
LENGO LILILO KUU ni kujaribu Tena ile bahati ya CDM baada ya Lowassa kwenda kuwaongezea IDADI YA WABUNGE kupitia idadi ya kura alizopata mgombea wa UKAWA.
Chambilecho ZITTO KABWE "kwa vyovyote vile kwa MAZINGIRA yoyote Yale" anatahadharisha ile HOFU KUU ALIYONAYO.....
HOFU GANI?
ZZK anajua ya kwamba mgombea wao mh.Membe ni GALASA...........
Mh.Membe hana hata SUDUSI ya kaliba aliyokuwa nayo mh.Lowassa kipindi KILE cha "MAFURIKO KOKO na "ULIPO TUPO".
ZZK anajua kuwa pamoja na CV za mh.Membe na KUJIMWAMBAFAI kuwa YEYE NI Vladimir Putin wa TZ na kiungo MNOGESHAJI Uchaguzi,bado hana PLATFORM kubwa ya KISIASA....
Mh.BCM hakuwahi kuwa na platform kubwa ya KISIASA ndani ya CCM sembuse nje yake?!!!
Mh.BCM alijizolea umaarufu wa KISIASA kwa sababu ALIKUWA anatembelea NYOTA YA JAHA ya mh.Kikwete,kwa hiyo basi si CANDIDATE atakayemsumbua mh.Magufuli kwa wananchi hasa Kura za walalahoi wa nchi hii......
Mh.Magufuli atabaki na kumbukumbu isiyofutika,kuwa ni Mh.Lowassa pekee aliyewahi kumsumbua kutoka upinzani,na katika hili simuoni mh.Tundu Lissu Wala mh.Membe akiuvunja Mwiko huo.
Muuza Al Kasus
Tandale