Zitto: Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema...

Status
Not open for further replies.

Yaani hapa ni kama unafua nguo na maji ya chooni kisha unaenda kusuuza na maji ya tope. Hapa naona furushi la maneno ya mihemko na kujipendekeza juu.
 
Kwahiyo kumzushia mkuu kifo ni moja ya kukosoa?
 
Kwahiyo kumzushia mkuu kifo ni moja ya kukosoa?

Mangapi yamekosolowe na kushauriwa na hayajafanyiwa kazi? Huko kumzushia ni uzushi kama uzushi mwingine, unaweza kuupuza maana sio issue sana. Kuna ya msingi zaidi ya uzushi wa mitandaoni tungeweza kujadili. Suala la msingi katika huo uvumi, ni kuwa kuna baadhi ya watu wameonyesha kuwa hawatendei sawa watu wa itikadi tofauti na yeye, na chini ya utawala wake box la kura limezidi kutoheshimiwa. Ni suala simple, sioni kama kuna jipya kwenye huo mjadala ambao dhahiri ni uzushi.

Ungejikita kwenye ule mkataba wa Tanzania na Barrick kuhusu Tanzania kupata 16% na sio 50/50, wangalau ningeona unajadili jambo la maana. Unakwama wapi Misuli?
 
A picture speaks a thousand words!
 
Mbna umekuwa mtetezi wa Zitto sana tindo, kunani?
 
Mbna umekuwa mtetezi wa Zitto sana tindo, kunani?

Mkuu nitendee haki sina sababu ya kumtetea Zitto, kwasababu mimi sio sehemu ya watu walioamini huo uzushi wa kigogo maana namfahamu. Ninachosema Zitto ameomba msamaha ili iwe nini? Kila siku si wanafanyiwa ukatili wa wazi na vyombo vya dola tena kwa maagizo ya wanasiasa walio madarakani, mbona wao hawamuombi msamaha? Labda unionyeshe sehemu yoyote niliyomtetea sana Zitto.

Mimi kwangu nimesema huu uvumi kuhusu rais, ilikuwa ni sehemu sahihi ya sisi wengine kuonyesha hisia zetu kwamba rais anatumia madaraka yake kukandamiza wasio wa itikadi yake, na anahujumu box la kura kwa faida ya chama chake. Hivyo kwa sababu hiyo anapokuwa kwenye matatizo sio rahisi wanaohisi kutotendewa sawa kuwa upande wake. Utaratibu kama huu kwa jamii yetu hutumika sana, kama huishi na watu vizuri, siku ukifiwa au kuandaa sherehe watu hawajitokezi, na hata watakaojitokeza wanaweza wasile chakula ulichoandaa kama sehemu ya kukuonyesha kuwa hutendi sawa. Sioni tatizo kwenye hili, na wala hapo hamna utetezi wowote kwa Zitto kuhusu maoni yangu.
 
nimekusoma mkuu, niwie radhi, nilidhani umesimama naye, hoja yako nimeshaielewa.
 
Mkuu yani katika huu uzi wewe ndio mwenye post nyingi kuliko mchangiaji yeyote yule.

Hivi huoni aibu, si bora ungeanza kujadili hata mambo basi yatakayo wapa ushindi kwenye chaguzi zijazo?
 
Wacha unafiki. Na wewe uliweka picha ya mwanamke akikagua gard ya heshima. Unakumbuka uliandika Nini?.
 
Natamani nimtukane. Lakini naogopa kufungiwa. Nikidhani Zitto NI mwanasiasa mwenye akili na upendi kumbe ni hafadhali ya Iddi Amini aka Nduli
 
Mkuu yani katika huu uzi wewe ndio mwenye post nyingi kuliko mchangiaji yeyote yule.

Hivi huoni aibu, si bora ungeanza kujadili hata mambo basi yatakayo wapa ushindi kwenye chaguzi zijazo?

Una ushauri mzuri sana iwapo kungekuwa na uchaguzi, lakini hakuna uchaguzi bali kuna zoezi la kuwahalalisha wanaccm. Huyo niliyemjibu nimemjibu kama yeye maana naukubali uwezo wake. Lakini nguruwe pori kama ww ndio wanachangia niwe na post nyingi kwenye huu uzi. Huoni kwenye ule uzi wako kule nimekupa ukweli wako, ukatoka kule kwa hasira mpaka umekuja huku kuhesabu post zangu?
 
Mkuu yani katika huu uzi wewe ndio mwenye post nyingi kuliko mchangiaji yeyote yule.

Hivi huoni aibu, si bora ungeanza kujadili hata mambo basi yatakayo wapa ushindi kwenye chaguzi zijazo?
Huyu jamaa itakuwa analipwa kuishambulia serikali. Anajuhudi sana kwenye hilo.
 



Msitunge maneno ya Uzushi ili mjibiwe!
 
Natamani nimtukane. Lakini naogopa kufungiwa. Nikidhani Zitto NI mwanasiasa mwenye akili na upendi kumbe ni hafadhali ya Iddi Amini aka Nduli
Zitto anasukumwa na ubinafsi, sio mtu wa kumuamini huyu.
 
Huyu Zitto atakuwa karithishwa uchawi na marehemu mama yake
 
Zitto ni mnafiki yeye naye ndio alikuwa ana eneza uvumi huo na uzushi hahahaha koma acha unafiki bora uendelee kuwa mchawi kuliko kuwa mnafiki!
Usipaniki brother fahamu kama mficha uchi hazai kama ni mnafiki au siyo mnafiki tunapenda tujue ukweli ukowapi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…