Roho ya uchawi...Ila kuna watu wanafiki sana na zito ni mmoja wao... hivi JPM akipatwa na mabaya wewe utafaidikaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Roho ya uchawi...Ila kuna watu wanafiki sana na zito ni mmoja wao... hivi JPM akipatwa na mabaya wewe utafaidikaje?
Bahati nzuri zaidi ni kwamba tangu uvumi huu umeanza hadi hii leo, niliamua kiwa kimya kabisa na kuto comment jambo lolote kwenye mtandao wowote ule wa kijamii.
Kuhusu kututimia mitandao kufanya yenye tija ujue tu kwamba mtandaoni yapo mengi nimesha yafanya na naendelea kuyafanya
Jiwe walilolikataa waashi limekua jiwe kuu la pembeni, nikupongeze kwa kuomba radhi ni jambo la hekima na kwa nia ileile usisite kumuomba radhi mweshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli.Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:
Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.
Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.
Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.
Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.
Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.
Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
Kweri mwambieZitto ni mnafiki yeye naye ndio alikuwa ana eneza uvumi huo na uzushi hahahaha koma acha unafiki bora uendelee kuwa mchawi kuliko kuwa mnafiki!
Sema mawakala wa shetani na mafisadi wanaoipata joto ya jiwe!Vizuri, aache sasa roho mbaya na visasi. Nadhani amejifunza ni namna gani Wananchi wake wengi wanavyomtakia mabaya (kifo), na wapo tayari kufanya sherehe muda wowote iwapo mauti yatamfika. Akiendeleza kiburi shauli yake.