ZITTO: Sitopokea posho ya 300,000 kwenye mbunge la Katiba

ZITTO: Sitopokea posho ya 300,000 kwenye mbunge la Katiba

Status
Not open for further replies.
Posho-Za-Vikao-Mhe-Zitto-Kabwe-II.jpg



Zitto akilejea barua yake ya 2011 akiwa anaongea na mwandishi wa gazeti la majira amesema hatapokea posho yoyote kwenye hili bunge la katiba. Zitto amesema ametumwa na wanakigoma kuja kuandika katiba wala sio kipokea posho.
Zitto ameongezea kuwa kuwa huu ni wizi kwa wananchi yaani mwalimu analipwa kati ya 200000 mpaka 300000 kwa mwezi wakati wabunge wanapokea kwa siku

Anafanya kampeni akijua kundi kubwa ni la walimunchini ambao kama waki muunga mkono uhakika wa kura nyingi anao 2015. Sasa jeanagombea kwa tiketi ya chama gani? Tafakari!!
 
Wewe badala ya kuuliza kama wabunge wako wa CCM watachukua au wataacha unazungumzia Lema hivi haujioni kama ni Mp.um.bavu

tunajua kwamba maccm ni majizi hivyo hatuna haja ya kurudia kujiuliza ktk hilo - ukiondoa upofu na mahaba ya kijinga, hawa makamanda wetu wanatofauti gani na ccm?!
 
Heshima mbele wakubwa,


Msidanganyike jaani, barua ya Juni, 2011 hiyo. Wasitudanganye kabisa, wamwambie aandike nyingine...
 
Kwanza alitakiwa hata hili Bunge la Katiba asingie ila Mahakama tu imemchelewasha ungekuta na yeye anaangalia kupitia TBC1 kama sisi. Duh, siasa mbaya sana.. will never dare...
 
Hongera sana Zitto, wewe ni mfano wa kuigwa kwa vitendo si kwa maneno.

Tu ajua watanzania wengi walilalamikiq sana kunusu hii posho na wewe umefanya kwa vitendo si maneno kuikataa.

Watanzania na Wapenda maendeleo wanatakiwa kuungana na kumpongeza na hikiwezekana wabunge wengine hasa wakile chama cha wanaojiita wazalendo waungane nao nae kuikataa posho kwa vitendo maana hata wao walisema ni kubwa hivyo ni vyema kuikataa kwa vitendo..

Watanzania na watu wote wanatakiwa kufahamu kuwa zitto hajamlazimisha mtu kukataa posho ame hamua mwenyewe na wala hamlazimishi mtu kutichukua posho hivyo ni vyema wasiopenda kuziacha posho wanyamaze na waendelee kuzichukua na wala tusimchukie mtu kisa hafanyi tunayo yafanya.

Nitawashangaa watakaoo anza kumkashifu huyu mzalendo wakati kila mmoja wetu amekuwa akipinga hizi poshona sasa tumepata yule wakuzipinga kwa vitendo na si maneno.

Nchii hii hinahitaji watu kama hawa wasio na maneno mengi bali vitendo.

salamu hizi zimfikie kamanda Godbless J Lema na msaidizi wake Mungi na hikiwezekana tuungane kumpongeza kijana mzalendo wa vitendo.

Tusibaki kuandika makala tuu bali tuoneshe uzalendo kwa vitendo kama huyu kijana.

Mungu azidi kukulinda mh Zitto.

ana.
Wewe ni miongoni mwa wajinga wasiojua nini wanachoandika au kuongea wewe inasema wabunge wa CDM ambao hawafiki hata 50 waungane na Zitto kukataa posho ya 300,000/- huku ukiwaacha wa CCM ambao ni zaidi ya 200 hivi haujioni kama ni mp.umb.avu
 
Last edited by a moderator:
Wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya muungano wasichukue posho hizi.......hizi wachukue wakina Mtikila na Peter Mziray tu ambao hawajawahi kuzionja....KUDOS Zitto.
 
Kuna maali ambapo hizo posho zake zitapitishwa na kumfikia, huku sisi tukiamini kuwa hapokei posho. Mbona kwenye vikao vya kamati hawakatai posho na wanaweza wakavuta hatazaidi ya hizo 300k

sijui anawazaje zitto.. Ni janga lingine.. SI ANGECHUKUA AKAWAWEKEE BODA BODA WALE VIJANA WA MWANDIGA,, AU HATA AKAWABORESHEE WAVUVI WA DAGAA NETS...
ANA SHIDA KUBWA.
 
Sasa atotoa wapi hela za kuishi hoteli, kula na hata malipo ya taxi? Jamani tuache unafiki, labda atuambie amepata wapi hela za kutumia mbadala na hizo?
 
Watu bana, hivi mbona hata yale mambo rahisi mnashindwa kuyatekeleza??? Yeye anasimamia msimamo wake kuwa analipwa mshahara kwa kazi za kibunge na hivyo hawezi kupokea posho pale anapotimiza wajibu wake. Cha ajabu Chadema wenzangu ambao tunajipambanua kuwa wazalendo tunambeza. hivi hii tabia ya kubeza kila jema kwa kuwa limefanywa na mtu tusiyemkubali inatoka wapi?? kwani tunajenga nchi ya Zitto??

Nonsense kabisa!!! eti tutachikuwa kumkomoa Zitto!!!
 
Kwanini asipokee afu atupe mchanganuo wa hiyo hela kwenye madawati au madawa?

Umesema kweli, anavyoziacha bado haziwasaidii watu wa Kigoma. Kwasababu anajua kwamba zinatumiwa vibaya basi ni bora angezichukua na kuzitumia vizuri kwa kuwanunulia wanakigoma madawati. Ninaamini zipo shule nyingi Kigoma zina uhaba wa madawati na vitabu.
 
Sasa atotoa wapi hela za kuishi hoteli, kula na hata malipo ya taxi? Jamani tuache unafiki, labda atuambie amepata wapi hela za kutumia mbadala na hizo?

Mwalimu anatoa wapi hela za kuishi na kulipia nyumba yake??? Mshahara unamtosha na kama kuna allowance ya malazi anapokuwa nje ya kituo cha kazi (Bungeni) hapo sawa.
 
Nyie mnaomsema vibaya Zitto hamuogopi kumalizwa hata panya kwenu hatosalia.
Back to the topic.
Kama kukataa posho kumetoka ndani ya moyo wake, basi angezichukua tu najua Kigoma kuna matatizo mengi sana.
Ingesaidia hata kidogo, kuliko kutaka sifa ya kuikataa kabisa.
 
Posho-Za-Vikao-Mhe-Zitto-Kabwe-II.jpg



Zitto akilejea barua yake ya 2011 akiwa anaongea na mwandishi wa gazeti la majira amesema hatapokea posho yoyote kwenye hili bunge la katiba. Zitto amesema ametumwa na wanakigoma kuja kuandika katiba wala sio kipokea posho.
Zitto ameongezea kuwa kuwa huu ni wizi kwa wananchi yaani mwalimu analipwa kati ya 200000 mpaka 300000 kwa mwezi wakati wabunge wanapokea kwa siku

ZITTO ni jembe la ukweli
 
nakukubali kwa uzalendo zitto,namjua lema atakuja hapa kulalama akikuita mnafiki,safi zitto huo ndo uzalendo kamanda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom