Zitto: Umeme wa Gesi ungezalisha MW 3,500 zaidi ya wa Maji


Hii clip kama ipo naiomba aisee
The guy was a clown
 

Hii clip kama ipo naiomba aisee
The guy was a clown
 
Hayo yote yanategemea au yanaweza kubadilika kulingana na mkataba na kama hujui mkataba, ni bora kuweka akiba ya maneno.
 
Kwani wewe usichojua kuhusu utawala wa Kikwete ni kipi? Awamu ya nne nchi ilikuwa inaongozwa toka Washington. Jamaa walimuweka mfukoni mwao kiasi kwamba hata ungekuwa kwenye baraza la mawaziri, na kuwa na mapenzi mema na nchi yako, Rais wa nchi alishabanwa akabanika na mafisi wa kitaifa na kimataifa.

Kelele zote ninazosikia kuhusu umeme wa gesi ni mafisi hao hao kupata upenyo baada ya kifo cha JPM ili warudi kwa nguvu mpya. Kitu pekee kitakachookoa taifa hili kutoka kwa mafisi hao ni wimbi kubwa la raia wa kawaida waliofunguka macho kupitia utawala wa JPM njama za hawa matapeli. Huku mtaani karibu watu wote ikiwemo watu wa kawaida ambao huwezi kuwadhania watakwambia wazi wazi kwamba wanaiona miradi ya kimkakati ya JPM ikiwemo na bwawa la umeme kama hatua kubwa katika uchumi wa nchi, na ni pride ya taifa.
 
Jamani umeme wa Gesi haufai pale kinyerezi kila Mwezi kufanya matengenezo ya mitambo ya MW 300+ ni bilioni Nne, na hiyo ni kila Mwezi, bado wanauziwa Gesi na TPDC ambao nao wanauziwa na mabeberu wanomiliki mitambo ya kuchimba mtwara na ndo wanaipanga Bei , mpaka sasa serikali Haina control na Bei ya umeme kwakuwa Bei ya gesi wanapanga mabeberu.

Stiglers itakuwa Mali ya tanesco yaani serikali. Sasa watu washapewa pesa wapigie debe Gesi Ili mabeberu wauze Gesi nyingi wapate faidi nyingi, umeme wa Gesi ni utoko
 
Inasemekana bwawa linajengwa kwa kutumia utafiti uliofanyika mwaka 70 siunajua mazingira yanabadilika? likileta maafa pia muendelee kupongeza wanaolalamika huo mradi sidhani kama hawataki umeme

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Huo uthubutu ungefata katiba ungefanyika kwa ufasaha na haya yasingemkuta
 
Sasa hivi unauziwa unit sh ngapi?
Swala si uwingi wa MW pekee, ni kuangalia maisha ya huo mradi, na uendeshaji wake, je ikiwa ni 10000 MW na mwananchi akauziwa 2000 kwa unit, ukombozi kwa mwananchi utakuwa wapi?
 
Kwa nini tulikopa Trillion za pesa kujenga bomba la gesi halafu tukalitelekeza??
Huoni hiyo ni hali fulani ya kuchanganyikiwa na kutojua tunataka nini kama taifa?
 
Bomba la gesi lifanyiwe kazi gani??
 
KUTOKA MAKTABA YETU :

MKATABA WA GESI MTWARA WAVUJA


NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MKATABA wa mgawanyo wa mapato yanayotokana na uzalishaji wa gesi asilia kati ya Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC) na Kampuni ya Mafuta ya StatOil ya Norway, umevujishwa.

Mkataba huo ambao unadaiwa utaipotezea Tanzania Sh trilioni 1.6 kwa mwaka, umevuja na kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kuzua mijadala kutokana na mgawanyo wake kutoeleweka wazi.

Kwa mujibu wa makala yaliyoandikwa na jarida la mtandaoni la African Arguments, Tanzania itapoteza zaidi ya Sh trilioni 1.6 kila mwaka kulingana na viwango vya uzalishaji wa gesi asilia katika kitalu namba mbili.

Kitalu hicho kinamilikiwa na Kampuni ya StatOil na Kampuni ya ExxonMobil ya Marekani.

Pamoja na mambo mengine, mgawanyo huo pia unadaiwa kuwa ni sehemu ya Norway kujilipa fedha zake za misaada mbalimbali waliyoitoa nchini kupitia mkataba huo.

“Tangu Tanzania ipate uhuru, Norway imetoa misaada ya thamani ya Dola za Marekani bilioni 2.5 wakati kwa mkataba huu na Kampuni ya StatOil ambayo inamilikiwa na Serikali ya Norway kwa miaka 15 watapata dola bilioni 5.6.

“Kwa hiyo kwa miaka saba tu Norway itakuwa imerudisha misaada yake yote mara mbili zaidi,” ilisema sehemu ya makala hayo katika mtandao wa African Arguments.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) amesema katika taarifa yake kwamba, kuvuja kwa mkataba huo kumesaidia kuona ukweli wa matamko ya viongozi kuhusu ni namna gani Tanzania itafaidika na utajiri wake wa gesi.

Alisema kama mkataba huo mmoja taifa litapoteza matrilioni ya fedha, hali ikoje katika mikataba mingine 29.

Kwa mujibu wa Zitto, hivi sasa ugunduzi wa gesi asilia nchini ni lita za ujazo trilioni 51 ambazo ni sawa na mapipa bilioni 10 ya mafuta.

“Katika gesi asilia iliyopatikana nchini, StatOil peke yao wana jumla ya lita za ujazo trilioni 20, sawa na mapipa ya mafuta bilioni 4 ambazo ni zaidi ya mafuta yaliyogunduliwa nchini Uganda na Ghana kwa pamoja.

“Hata hivyo, utajiri wote huu utainufaisha zaidi Norway na Marekani kupitia kampuni zao kuliko watu wa Tanzania, Watanzania watabaki kupewa misaada ya vyandarua na mataifa haya ilhali wanafaidi gesi asilia yetu.

“Natoa wito kwa Wizara ya Nishati na Madini kutoa tamko kuhusu mkataba huu kati ya TPDC na StatOil, vile vile Kampuni hii ya StatOil kutoka nchi rafiki mkubwa wa Tanzania ina wajibu wa kutoa maelezo ya kina.

“Serikali ieleze ni hatua gani inachukua kurekebisha mkataba huu na StatOil nao waeleze watachukua hatua gani kuhakikisha wanaacha unyonyaji huu mkubwa na wa aibu kwa taifa la Norway,” alisema Zitto.

Alisema ni wakati muafaka kwa Watanzania kuona mikataba yote ya gesi na mafuta ambayo Serikali imeingia na wawekezaji.

Zitto alisema mkataba huu wa StatOil uliovujishwa uwe ni chachu ya kulazimisha Serikali na kampuni kuweka mikataba yao wazi kwa kuanza mashinikizo hayo sasa kwa faida ya vizazi vijavyo.

“Mwanzoni wengi wetu tulidhani kuwa tatizo la mkataba huu ni eneo la umiliki wa kampuni tu kulingana na namna ulivyowasilishwa, kumbe mgawanyo mzima wa mapato unakwenda kinyume na maelezo ya Serikali na TPDC kwa umma.

“Mkataba uliovuja unaonyesha kwamba, makubaliano ambayo Serikali imeingia na wawekezaji hawa wa Norway yanakwenda kinyume na mfano wa mkataba unaotakiwa kusainiwa (Model PSA).

“Uchambuzi nilioufanya kulingana na viwango vya mgawo wa mapato kati ya PSA na mkataba huu unaonyesha kwamba, Tanzania itapata mgawo kiduchu sana na kinyume na mgawo unavyopaswa kuwa,” alisema.

Kwa mujibu wa sheria mkataba wa mgawanyo wa mapato unaopaswa kutumiwa na TPDC katika mikataba na wawekezaji inatakiwa kilo 0-249.999 katika viwango vya uzalishaji kila siku, TPDC wapate asilimia 50 na mwekezaji asilimia 50.

Kilo 250 hadi 499, TPDC wapate asilimia 55 na mwekezaji asilimia 45 na kilo 1,500 na kuendelea TPDC wapate asilimia 80 na mwekezaji asilimia 20.

“Tofauti na mkataba huu, katika kilo 0- 299.999 za gesi ya viwango vya uzalishaji kila siku, TPDC inapata asilimia 30 na StatOil asilimia 70, kilo 300-599.999 TPDC asilimia 35 na mwekezaji asilimia 65 na kilo 1,500 na kuendelea ndiyo wote wanapata asilimia 50 kwa 50,” alisema.

Kwa mgawanyo huo wa mapato alisema utaifaidisha zaidi Kampuni ya StatOil ambayo ni kinyume na mkataba unavyopaswa kuwa.

“Wakati mgawo wa nusu kwa nusu upo katika uzalishaji wa chini kabisa kwenye ‘model PSA’, kwenye mkataba wa StatOil mgawo huo upo kwenye uzalishaji wa juu kabisa.

“Ukilinganisha mgawanyo huu wa mapato, iwapo kiwango cha ‘model PSA’ kingetumika Tanzania ingepata shilingi trilioni 1.6 zaidi ya kiwango itakachopata kwenye mkataba wa sasa uliovujishwa, hii ni kutokana na bei ambazo Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeweka katika uchambuzi wake kuhusu gesi asilia ya Tanzania,” alisema.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alikataa kuzungumzia kuhusu mkataba huo huku akielekeza watafutwe TPDC na Kampuni ya StatOil huku akihoji ni vipi kuvuja kwa mkataba ndiyo kunafanya Tanzania ipoteze fedha hizo.

Alisema kama mkataba una makosa au umevuja wa kuwaona ni hao waliotajwa.

“Huyo mtu aliyetuma sijui kuandika hayo ninyi wenyewe mmemfanyia uchunguzi ni mtu wa namna gani, maana siku hizi mtu yeyote nchi hii anaweza kuhongwa Dola 200 akaandika au kuzungumza chochote hata bungeni.

“Mimi nina vitu vingi vya kufanya zaidi ya kupitia hayo mambo ya kwenye mitandao, ukiacha kazi niliyopewa nina kazi ya taaluma yangu ya jiolojia ambayo naifanya kila siku,” alisema


CHANNZO: GAZETI MTANZANIA JULY, 7,2014
 
Afu wangetuuzia shilingi ngapi vile ??

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Wengi humu ni sehemu ya mafisadi.gesi inachimbwa na mabepari na lengo lao ni kupata faida na si hasara unadhani ss titauziwa Bei gani.Kama tunataka kujiridhisha Richmond nyingine sawa lkn mm Naona wengi humu huenda wanainterest na hizo projects za kihuni za gesi.ss tunataka Miradi ya serikali ili mtu akimess up tumshughurikie lkn haya makampuni ya mabepari yakiamua mwezi mzima yanazima umeme au yanapandisha Bei ya umeme tutafanyaje?
 
Gesi hii wanasiasa kibao walishakula kamisheni yao...Zitto ni mmoja wao, zipo tetesi kuwa mkataba wa gesi wa Wachina ulifungwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba huwezi kuufanyia figisu yoyote ya kuufumua na hayati JPM alishindwa!(akiwahi kusema sio mara moja) Kuwaonyesha kuwa mkijua "hizi" sisi tunajua "zile" ndio akaona usiwe tabu ngoja twende kwenye vyanzo vya maji...ili mahitaji ya tanesco kununua gesi yawe ni "pale tutakapozididiwa kabisa" gesi akina Kikwete, Muhongo, Zitto, na wengine wengi walishakula mgao wao na sasa wanatafuta namna ya kurudisha fadhila ya kile walichokula!
Wachina wakabebe gesi yao!
 
Zitto huna maarifa hata kidogo ya kuchambua mambo ya umeme waachie wataalamu wa umeme. Usilete siasa kwenye mambo ya msingi kuna wataalamu wake.
 
Kama kweli hiyo hela imekopwa na imeingia katika mfuko wa hazina haiwezi kutumika kwa kazi nyingine mfano kujenga reli? na kama hairuhusiwi si mkopo unarudishwa kwa aliyeutoa. Huo labda ni mkopo hewa na hela yote mmeificha Uswisi ndio maana Zitto anatapatapa kudanganya watu.

Zitto anatafuta namna ya kufiti katika serikali mpya ili anufaike binafsi na ni suala la muda tu, Zitto atatumia mpaka udini.
 
Wasomi wetu na wanasiasa wetu wengi wana elimu lakini hawana maarifa. Kitendo cha serikali kuanzisha ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme ni pigo kubwa sana kwa kampuni zinazoiuzia serikali gesi ya kuzalisha umeme, maana ujenzi wa bwawa utakapo kamilika na kuanza kuzalisha umeme wa bei nafuu hawa wenye makampuni ya gesi hawataweza tena kuiuzia serikali gesi kwa bei kubwa maana itakuwa inajitosheleza kwa umeme wa bei nafuu, hivyo basi itawabidi wapunguze bei ya gesi kulingana na matakwa ya serikali.
Kutokana na hali hiyo haya makampuni yanapambana kwa kila njia kwa kuwatumia baadhi ya wanasiasa na watu maarufau kuwaaminisha wananchi kwamba umeme wa maji ni gharama kuliko wa gesi ili wananchi wapinge ujenzi wa bwawa na wao waendelee kuiuzia serikali gesi ya kuzalisha umeme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…