misasa
JF-Expert Member
- Feb 5, 2014
- 14,244
- 10,073
Hujui au? Au tumefukia kule kwasababu tunaenda kwa fasheni?Lete ufanisi wa KIDATU.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hujui au? Au tumefukia kule kwasababu tunaenda kwa fasheni?Lete ufanisi wa KIDATU.
Si wameamua kujenga H.E.P hapo rufijiYaani Tanzania karibu miaka ishirini yote nasikia tu mradi wa umeme mradi wa umeme yaani hakuna anaefanikiwa akija huyu na mwingine anakuja na wake utadhani wanajenga nyumba tofauti...sema yule jamaa katupeleka chaka mno
Msidhani wazungu wanatupenda sana. Gesi sawa lakini umeme wa maji namba moja. Tusiendekeze siasa.Gas hapana, labda kama ingekuwa serikali ndo wanachimba wenyewe!
Nitapinga wote wanaopiga kelele za umeme wa gas! Sababu kubwa ikiwa gas inachimbwaa na makampuni binafsi tena ya nje! Wao ndo wanapanga bei gani wauzie Tanesco! Tanesco hawatakuwa na control na huu umeme kwa hiyo wananchi tutauziwa kwa bei ya juu sana.
Hii itasababisha maisha kuwa ya gharama zaidi!
Afadhali HEP ambayo less costly, na unazalishwa na serikali ambayo watakuwa na direct control. So mwananchi hataumia sana.
Tunampinga Magufuli kwa mambo mengi ila kwa hili la Bwawa la Nyerere tupige kelele kwa kila mmoja mradi uendelee kwa 100%.
Hii project iendelee
Shida ya nchi hii hatuna consistent policies na progrs. Ilani za uchaguzi zaCCM zinabadilika kila kipindi cha uchaguzi.Ja
Hii kwa kweli inauma sana hasa ukizingatia mradi wa gesi ya Mtwara ulipigiwa promo sana na tuliambiwa ukikamilika tutakuwa tumemaliza tatizo la umeme na kwamba umeme huo ni wa kuaminika ukilinganisha na umeme wa maji.
Kutelekeza huo mradi na huku tukiwa tumeukopea pesa kwakweli huo ni ubadhirifu mkubwa sana wa pesa za walala hoi wa nchi hii.
Sababu ya kuutekeleza hatujaambiwa badala yake tumerukia mradi mwingine unaogharimu pesa kibao kwa jasho la walala hoi.
Hii inatupa picha kwamba tumeamua kuanzisha miradi mipya kwa malengo fiche.
Unajua ufisadi wewe kinda! Kalale kwanza maana hujui unalosemaUza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara, umeme wa gas tumekopa 3.2t, kisha huyu naye kakopa 6.5t, hiyo ni 10t tayari. Huo wa maji nao tayari una mizengwe ndani. Sasa kama tayari tuna deni la 10t, hapo tumekwepa gharama gani? Au unadhani huo ufisadi wa kina JK unakwepwa kwa kuhamia mradi mwingine wa mkopo?
Madalali ndio walikuwa wanachukua kamisheni kwenye kampuni za kusupply mafuta ili mgao wa umeme uendeleeYaani sekta binafsi ndio ipewe swala la umeme??
Wewe Zito in kibaraka wamabeberu! Unazungumzia gesi IPI? Hii ya kwetu ulishiriki kuiuza kwa hati ya dharula bungeni! Wakikupandishia bei utafanyaje wakati gesi ni yao maana mliwauzia? Au wakigoma kukuuzia utafanyaje? Wakiamua tu kukuhujumu utafanyaje? Hatutaki tena uchumi tegemezi.Uchambuzi wa ripoti ya CAG ulofanywa na chama cha ACT WAZALENDO inasema tulidharau na kuutupa mradi wa umeme wa gesi ambao tulishakopa fedha China wenye wenye uwezo wa kuzalisha MW 3500 tukakimbilia mradi mpya wa umeme wa Maji wenye kutoa MW 2110 kwa gharama ya Tillioni 6 matokeo yake tumekopa madeni mara mbili kwenye lengo moja.
Wewe kafie mbali huko, mnapambana na maiti na bado anawapiga knockout, tunataka Stigler gorge, fullstopNa Hayati alitoa hela zake mwenyewe kujenga Stigler? Je zile hela za rambirambi alizoiba kwanini asifukuliwe azirudishe?
Naam, UncleKwangu Mimi swala sio wingi wa MW wala gharama atakayouziwa mwananchi, Mimi najiuliza tu ni kina nani wapitisha mradi wa gesi? Walikuwa waburundi? Waliokuja kuuweka pending je wanatoka nchi gani? Sio watanzania?
Magufuri alikuwepo kwenye baraza la Mawaziri lililopitisha mradi wa gesi, amekuja kuwa Rais akaja na bwawa la Nyerere! Wataalum hao hao waliopitisha gesi ndo hao hao walipigia chapuo bwawa la Nyerere
Shida yangu kubwa iko kwa aina ya viongozi na wataalum tulionao sijui wakoje
Watu makini hawawezi kupitisha vitu kwa kukurupuka! Kama nchi lazima iwe na plan ambayo hata aje nani atalazimika kuitekeleza. Hapa tutatofautiana speed tu!
Haiwezekani eti nchi ina wataalum wanakaa vikao wanajadili na kukubaliana kwamba "Tanzania tunahamia kwenye umeme wa gesi" halafu miaka kadhaa mbele wanasema " Hapana, turudi kwenye bwawa"
Miradi mikubwa Kama hii haitakiwi kuamuliwa kwa mihemuko wala mashindano!
Sina shida na mradi upi ni Bora, shida yangu kwanini wataalum hawako stable kufanya maamuzi
Pia maintenance ya mitambo ya kufua umeme kwa gesi ni gharama sana kuliko mitambo HEP. Kwasa babu HEP hakuna joto linalozalishwa katika kufua umeme wakati umeme wa gas joto linahitaji service ya mitambo mara kwa lakini pia mitambo huchakaa mapema.Baada ya kujenga Mtambo wa gesi utabidi kila siku ununue gesi,
Hivi hawa akina zitto wanafikiriaga mata**k
Kama mradi una feasibility studies ya miaka 70s, je bwawa linaendana kama fasheni za nguo? Kama bwawa linaendana kifasheni kwanini tunaendelea kutumia KIDATU?
Gas ni ya watanzania, bei ya umeme haieleweki hapa Tanzania mpaka wakati wa uzalishaji. Hao wanaosema bei umeme wa maji itakuwa ndogo ni utapeli. Bei itakuwaje ndogo wakati ni hela za mkopo? Kama wanaweza kushusha bei ya umeme, kipi kimewashinda kushusha bei ya mafuta ya kula na sukari?
Kwaiyo yanaitwa maporomoko ya kidatu?Kidatu sio bwawa ni maporomoko, tofautisha kati ya Bwawa na Maporomoko Dam and falls), Bwawa linajengwa kuzuia maji ili yatiririke kwa utaratibu fulani kuendesha mitambo ya kuzalishia umeme, Maporomoko mara nyingi huwa ni tukio la asili ambapo Maji yanayoporomoka hutegwa sehemu fulani na yanapoporomoka huendesha mashine ya kuzalisha umeme.
Gas ilishauzwa na mikataba michafu wakati wa JK na serikali haikuwa na jinsi zaidi ya kuanza mradi wa HEP.. Gas yetu ingekuwa Tanesco inauziwa na kampuni za kigeni hivyo bei ya umeme ingekuwa hatuna control nayo, ni hatari sana, kheri mara 100% umeme wa maji. Zitto afunge domo lake tu.
Tulikabidhi nchi kwa limbukeni.Tukubali jambo moja, tulikuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa kukurupuka.
Uliona wapi kiongozi anamfukuza mfanyakazi mwenye mkataba wa kazi kwa kuwauliza watu waliopo kwenye mkutano, 'Nimtumbue sasa hivi au nimwache?; Wananzengo nao wanajibu, "tumbua"; halafu mfalme anasema, "Kabwe, nimekwishakutumbua". Kweli unaamini huyo ni kiongozi anayeweza kutafakari kabla ya maamuzi?
So sad!Tukubali jambo moja, tulikuwa na kiongozi anayefanya maamuzi kwa kukurupuka.
Uliona wapi kiongozi anamfukuza mfanyakazi mwenye mkataba wa kazi kwa kuwauliza watu waliopo kwenye mkutano, 'Nimtumbue sasa hivi au nimwache?; Wananzengo nao wanajibu, "tumbua"; halafu mfalme anasema, "Kabwe, nimekwishakutumbua". Kweli unaamini huyo ni kiongozi anayeweza kutafakari kabla ya maamuzi?