Bomba la gesi lifanyiwe kazi gani??
Ngoja nikupe elimu ndogo ya power plants
Kwenye power systems kuna aina mbili za load.
1. Base load
2. Peak load
Naanza kwenye peak load.
Peak load-
Hapa matumizi ya nishati ni makubwa sana, huu ni muda ambao viwanda vikubwa kwa vidogo, vinafanya kazi, na shughuli nyingi za uzalishaji zinafanyika, na inatokea kwa kipindi cha muda fulani kwa kila siku za kazi.
kwenye peak load gharama za kuzalisha umeme zinaongezeka kwasababu mahitaji ni makubwa, matumizi yanapoongezeka maana yake inabidi mitambo ya akiba iwashwe kuzalisha umeme.
Kiuchumi mitambo inayoshauriwa kutumika kipindi cha mahitaji yakiwa makubwa ni gas turbine na diesel power plant, kwanini wamezichagua hizo kwasababu ni nzuri kimahitaji na kiuchumi kwa utumizi wa muda mfupi.
Base load
Haya ni matumizi ya kawaida yasiyozidi kiwango kikubwa cha mahitaji kwa muda fulani wa siku, muda viwanda vikubwa na vidogo na shughuli zote kubwa zinazotumia umeme mwingi zinaposimamishwa. hapa kwenye base load vyanzo vya umeme vizuri ni Hydro electric power na thermal power plants.
Kupitia hizo chambuzi ndogo kwa ufupi umeshapata logic ya kwann CAG Assad kwenye report yake alisema Tanesco wanauziwa unit 500 wanakuja kuuza 250 (hizo figure sio exactly alizosema ila ziakaribiana)
Unit zinauzwa 500 kwasababu gharama ni kubwa ya uzalishaji umeme wa gas.
Gas inatumika kuzalisha hadi umeme wa mahitaji ya base load wakati efficiently ulitakiwa utumike during peak load.
Nadhani nimekujibu kuhusu bomba la gas, swali jingine.