Zitto: Umeme wa Gesi ungezalisha MW 3,500 zaidi ya wa Maji

JIWE hataki ushauri, naona Mama anauchinjia baharini tunarudi kupanda miti yetu pale tuendelee na gesoi na nyuklia.
 
Ni kampuni gani hiyo ambayo ndiyo inamiliki gas ya tanzania na itakuwa inaiuzia tanesco ili iuze umeme kwa bei ghali hivyo kupandisha gharama za maisha .?
 
Bomba la gesi lifanyiwe kazi gani??
Ngoja nikupe elimu ndogo ya power plants

Kwenye power systems kuna aina mbili za load.

1. Base load
2. Peak load

Naanza kwenye peak load.

Peak load-
Hapa matumizi ya nishati ni makubwa sana, huu ni muda ambao viwanda vikubwa kwa vidogo, vinafanya kazi, na shughuli nyingi za uzalishaji zinafanyika, na inatokea kwa kipindi cha muda fulani kwa kila siku za kazi.

kwenye peak load gharama za kuzalisha umeme zinaongezeka kwasababu mahitaji ni makubwa, matumizi yanapoongezeka maana yake inabidi mitambo ya akiba iwashwe kuzalisha umeme.

Kiuchumi mitambo inayoshauriwa kutumika kipindi cha mahitaji yakiwa makubwa ni gas turbine na diesel power plant, kwanini wamezichagua hizo kwasababu ni nzuri kimahitaji na kiuchumi kwa utumizi wa muda mfupi.

Base load
Haya ni matumizi ya kawaida yasiyozidi kiwango kikubwa cha mahitaji kwa muda fulani wa siku, muda viwanda vikubwa na vidogo na shughuli zote kubwa zinazotumia umeme mwingi zinaposimamishwa. hapa kwenye base load vyanzo vya umeme vizuri ni Hydro electric power na thermal power plants.


Kupitia hizo chambuzi ndogo kwa ufupi umeshapata logic ya kwann CAG Assad kwenye report yake alisema Tanesco wanauziwa unit 500 wanakuja kuuza 250 (hizo figure sio exactly alizosema ila ziakaribiana)

Unit zinauzwa 500 kwasababu gharama ni kubwa ya uzalishaji umeme wa gas.

Gas inatumika kuzalisha hadi umeme wa mahitaji ya base load wakati efficiently ulitakiwa utumike during peak load.

Nadhani nimekujibu kuhusu bomba la gas, swali jingine.
 
Mbona project zote sasa za awamu ya tano zinapingwa. Kulikoni? Hivi tumelogwa kwa kupingana na Ilani ya Uchaguzi. Au ndiyo kumchukia mtu na mavazi yake yote.Haiwezekani
 
Halafu kila siku mgao wa umeme hauishi. Utaskia mara kunguru wanalaumiwa kwa kusababisha umeme kukatika.

Wakati madeni ya taifa yanazidi kuongezeka. Na Raia tukapigwa marufuku kuhoji wala kuuliza chochote.View attachment 1749265
Halafu kila siku mgao wa umeme hauishi. Utaskia mara kunguru wanalaumiwa kwa kusababisha umeme kukatika.

Wakati madeni ya taifa yanazidi kuongezeka. Na Raia tukapigwa marufuku kuhoji wala kuuliza chochote.View attachment 1749265
Hizo USD bilioni 15 za mwaka 2015 ilipofika mwaka 2020 riba yake na hiyo princioal jumla ilikuwa Dola ngapi ngapi? hilo deni la ndani sh triliini 8 ilipofika 2020 riba pamoja na principal ilikuwa dh ngapi?
ukishapata hiyo hesabu ndipo sasa utoe deni lililopo vinginevyo ni unafiki kumlzumu JPM kwa madeni ya watangulizi wake.
 
Muhongo alisema umeme wa maji umeshaapitwa na wakati umeme wa kisasa ni wa gesi

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Hiyo gesi anamiliki nani, na bei ya huo umeme ingekuwa kiasi gani?

Gas ni ya watanzania, bei ya umeme haieleweki hapa Tanzania mpaka wakati wa uzalishaji. Hao wanaosema bei umeme wa maji itakuwa ndogo ni utapeli. Bei itakuwaje ndogo wakati ni hela za mkopo? Kama wanaweza kushusha bei ya umeme, kipi kimewashinda kushusha bei ya mafuta ya kula na sukari?
 
Kama mradi una feasibility studies ya miaka 70s, je bwawa linaendana kama fasheni za nguo? Kama bwawa linaendana kifasheni kwanini tunaendelea kutumia KIDATU?

Lete ufanisi wa KIDATU.
 
Je, ungeuzwa kiasi gani?
 
Bwana mdogo, akili yako ni finyu. Bei ya umeme inategemea ufisadi kiasi gani umetumika. Bila ufisadi wa JK katika umeme wa gesi, umeme wa gesi ungekuwa rahisi sana. Maamuzi ya kutumia wa maji ulikuwa ni kukwepa ufisadi wa akina muhongo, ndugai etc katika ule mradi. Tanua akili uone jinsi SGR ya kenya ilivyo
 
Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara, umeme wa gas tumekopa 3.2t, kisha huyu naye kakopa 6.5t, hiyo ni 10t tayari. Huo wa maji nao tayari una mizengwe ndani. Sasa kama tayari tuna deni la 10t, hapo tumekwepa gharama gani? Au unadhani huo ufisadi wa kina JK unakwepwa kwa kuhamia mradi mwingine wa mkopo?
 
Ja
Hii kwa kweli inauma sana hasa ukizingatia mradi wa gesi ya Mtwara ulipigiwa promo sana na tuliambiwa ukikamilika tutakuwa tumemaliza tatizo la umeme na kwamba umeme huo ni wa kuaminika ukilinganisha na umeme wa maji.

Kutelekeza huo mradi na huku tukiwa tumeukopea pesa kwakweli huo ni ubadhirifu mkubwa sana wa pesa za walala hoi wa nchi hii.

Sababu ya kuutekeleza hatujaambiwa badala yake tumerukia mradi mwingine unaogharimu pesa kibao kwa jasho la walala hoi.

Hii inatupa picha kwamba tumeamua kuanzisha miradi mipya kwa malengo fiche.
 
Baada ya kujenga Mtambo wa gesi utabidi kila siku ununue gesi,

Hivi hawa akina zitto wanafikiriaga mata**k
Huyo jamaa ni mpuuzi na hawa ndio walikuwa wamepigwa pini hasa sababu ya siasa zao za kuchumia tumbo! Ataongea na kupinga mengi kelele nyingi ila akipewa bakshishi anatulia!
**** kama hawa sio wa kuchekewa kabisa!
 
Mi nadhani kuna ukweli hapa.

Kelele hizi, tena haraka kiasi hiki haziwezi kuwa ni za bure.

Pamoja na kwamba Samia hawezi kuuzima mradi wa maji kwa sasa, lakini inaonekana hawa watu watampa 'pressure' kubwa sana aachie gesi.
 
Ni kiasi gani cha pesa kilikopwa mkuu 'Achanakia'.

Pesa hiyo iliyokopwa ilipelekwa wapi, au imeliwa? AAaaah, ni lile bomba lililojengwa au sio?

Sasa hilo bomba litaoza, au wenyewe wachina watalichukua tena?

Kwa hiyo wewe unapendekeza iwe vipi, tusitishe huu mradi wa umeme wa maji hapo ulipofikia, ili tuurudie ule wa gesi?

Hebu eleza maoni yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…