Zitto: Umeme wa Gesi ungezalisha MW 3,500 zaidi ya wa Maji

Mkuu hata mimi naungana na wewe kwamba umeme wa maji unatufaa sana sisi kuliko huo umeme wa gesi nk,

Ila kuna aina mbili za umeme wa maji, ule wa maporomoko na ule wa kujenga bwawa, pale kidatu sio Bwawa bali ni maporomoko ya maji kutoka mlimani na hapo ndipo mashine zimetegwa na maji yanapoporomoka kutoka mlimani ndipo huendesha hizo generators kuzalisha umeme. Kuna ( falls na Dams). Linalotaka kujengwa huko stiegler ni Bwawa ambalo litahifadhi maji kisha zinawewa njia kwenye barrier (Dyke) ambapo katika hizo njia wataweka Generators na maji yanapopita kwa msukumo ndipo huendesha hizo generators.
 
Ukipata pesa ukaamua kujenga nyumba ya kisasa ni lazima ubomoe ya zamani? Tulijenga uwanja wa Mkapa hapo pembeni ya wa taifa, mbona hatukuuvunja? Umeishiwa na hoja nini dogo.
 
mkuu uwe unaacha ujinga hata mara moja moja basi.

mbona siasa zinawaharibu hivi!!mnafanya haya kwa maslahi ya taifa kweli??

Umeshaishiwa na hoja, sasa pembeni wenye uwezo wa hoja waongee.
 
Zito ni mzigo na si riziki!

Zito no zigo zito na si riziki, iko hivi:
Zito alishiriki kuuza gesi yetu yote kwa hati ya dharula. Na sasa gesi ina mwenyewe japokuwa anaichimbia Tanzania!! Hatuna maamuzi nayo! Tukiitaka lazima tuinunue kwa bei atakayotaka mwenye nayo. Ukweli huu wote zito anaujua. Baada ya kuiuza gesi Leo anataka tuwekeze kwa kutegemea gesi isiyo yetu! Kwa mfano bei ya gesi ikipandishwa tutalazimika kununua hivyo hivyo! Wakiamua kutuhujumu hatuwezi kuwa na ujanja!! Lakini gesi INA ukomo Wa uhakika ila maji hayana uko Wa uhakika! Zito tunakujua, unataka kutufanya watumwa Wa gesi yetu waliyoiuza.
 
Halafu baada ya kumtumbua, nafasi yake inachukuliwa na mwingine, THEN KESI MAHAKAMANI... WAKATI HUO NAFASI HIYO MOJA WANALIPWA WATU WAWILI KWA MWAKA MZIMA.. MTUMBULIWA NA MTEULIWA MPYA... gharama hizo hazisemwi
 
Ukipata pesa ukaamua kujenga nyumba ya kisasa ni lazima ubomoe ya zamani? Tulijenga uwanja wa Mkapa hapo pembeni ya wa taifa, mbona hatukuuvunja? Umeishiwa na hoja nini dogo.
Utakuwa juha! Ukipata pesa halafu unajenga nyumba ya kisasa kwenye kiwanja ambacho tayari ulishakiuza utakuwa juha!! Maana utaendelea kulipia pango la ardhi milele yote! Akikutishia kupandisha kodi ya ardhi unalazimika kumwabudu ili ubembeleze!
Iko hivi gesi yetu ilishauzwa!! Sasa tunaambiwa tujenge mitambo ya kuzalisha umeme Wa gesi, nani ajuaye gesi itauzwaje? Akikukatalia kununua kiasi cha gesi unachotaka utafanyaje? Akikupa sharti la kuruhusu usenge wakati nchi yote inategemea umeme wa gesi utafanyaje? Hivi inaingia akilini kuwekeza matrilioni kwenye rasilimali ambayo huna miliki nayo?
 
Je hii Stigler serikali inachimba yenyewe??
Anachimba na kujenga mkandarasi lakini bwawa na mitambo yote itamilikiwa na Tanzania. Lakini gesi wameshamilikishwa wageni sisi tumegeuka kuwa wateja! Hatuna kauli nayo!
 
Wawekezaje wa huo umeme ni "thithi" kwa Mgongo wa wawekezaji wa "China" na hata huo wa Bandari ya Bagamoyo wawekezaji ni "thithi" mtaji fedha za sandarusi:
 
Anachimba na kujenga mkandarasi lakini bwawa na mitambo yote itamilikiwa na Tanzania. Lakini gesi wameshamilikishwa wageni sisi tumegeuka kuwa wateja! Hatuna kauli nayo!
Mbona mnapenda kujifariji na KUKERA?
 
Wapiga debe wa mabeberu wanaolilia umeme wa gesi na bandari ya bagamoyo tuwaorozeshe hapa! 1. Propesa Muongo 2. Ziiitoooo Kerbbwe 3. Spuka Nndungayyi 4. Mzee wa Msoga (nyuma ya pazia). tuendeleze orodha hapa!
 
Kuna maamuzi lazima uyachukue immediately na hadharani ili watu wajifunze. Ndio maana mwizi anaiba sirini lakini anaadhibiwa hadharani. Marekani walionyonga Sadam Hussein na kusambaza hadharani video, same same kwa Gadafi.
 
Achana na maneno ya uchochoroni, feasibility study ya mwaka 70s ni ipi na ya 2000s ni ipi? Kikubwa ni umeme uzalishwe. Waziri mkuu juzi amehakikishia uma kua mradi utakamilika kwa wakati
 
Achana na maneno ya uchochoroni, feasibility study ya mwaka 70s ni ipi na ya 2000s ni ipi? Kikubwa ni umeme uzalishwe. Waziri mkuu juzi amehakikishia uma kua mradi utakamilika kwa wakati
Maneno ya uchochoroni=Waziri mkuu

"Muheshimiwa yuko anachapa kazi ana mafaili mengi sana"- Msikitini, Njombe

Ni bora nimuamini CAG kuliko Mwalimu Majaliwa

Ila cha muhimu umeme uzalishwe tu ndio tunachotaka. Kwa hilo uko sahihi
 
Ukipata pesa ukaamua kujenga nyumba ya kisasa ni lazima ubomoe ya zamani? Tulijenga uwanja wa Mkapa hapo pembeni ya wa taifa, mbona hatukuuvunja? Umeishiwa na hoja nini dogo.
Ujamsikia POROFESA MUONGO dogo?
 
Zitto anaweza kuwa na hoja lakini shida yake ni ukigeugeu wake ndiyo unatufanya wakati mwingine tusimwamini hata kwa mambo yenye ukweli ...hatabiriki
 
Maneno ya uchochoroni=Waziri mkuu

"Muheshimiwa yuko anachapa kazi ana mafaili mengi sana"- Msikitini, Njombe

Ni bora nimuamini CAG kuliko Mwalimu Majaliwa

Ila cha muhimu umeme uzalishwe tu ndio tunachotaka. Kwa hilo uko sahihi
Katika watu niliowapa credit na kuwaamini ni Majaliwa, lakini nimeshapoteza imani naye, hakuwa na sababu kulisemea jambo ambalo waumini hawakumuuliza swali
 
Je, Zitto amezingatia na masuala ya climate change na mitigation zake kwenye hoja yake? Labda kama kuna teknolojia ya clean natural gas!
 
Hiyo gesi faida yake yote si tulishanyang'anywa huyu zito nae ni puppet nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…