Katika Kipindi hiki kigumu cha COVID-19, Serikali ulimwenguni zinasaidia wananchi wake. Tanzania kuna wananchi wanyonge na masikini wengi, hawana akiba ya fedha, kwa sababu ya udogo wa kipato.
Mfano, Sekta ya Utalii imepata pigo kubwa, wafanyakazi kupewa likizo bila malipo. Pia kukosekana mapato katika tourism, agriculture consumers imedrop mno, Kilimo kimeathirika, wakulima wameathirika kimapato.
Ni vigumu kugawa pesa kama USA, Serikali ifanye Subsdize katika huduma muhimu kama Unga, Mafuta kupikia, Gesi ya kupikia, Umeme. Serikali ipunguze kodi katika hizi bidhaa ili zipungue bei na wanyonge wasiteseke. Kuna PESA za Mwenge na pesa za maafa ..ziende huko.
Serikali iongee na Bakresa na Mo, na wazalishaji wengine, ili Wapunguze bei za unga na Mafuta, then Serikali ifidie. Na Wasambazaji wa gesi za majumbani, serikali iongee nao, gesi ipungue bei...Pili itaokoa mazingira na kufuta matumizi ya mkaa.
Wabunge wote, na wanaharakati, muishauri serikali.