Uchaguzi 2020 Zitto: Wagombea wote 18 wa ACT-Wazalendo kisiwani Pemba wameenguliwa

Uchaguzi 2020 Zitto: Wagombea wote 18 wa ACT-Wazalendo kisiwani Pemba wameenguliwa

Pemba wagombea wengi wa upinzani hawajasoma elimu wengi ni madrasa
Miaka mingine walikuwa wanajaza vipi, ila pia Sheria za uchaguzi zinahitaji kufanyiwa marekebisho, mtia nia akikosea kujaza fomu anapaswa apewe fomu nyingine au kurekebisha alipokosea na siyo kumtoa kwenye kinyang'anyiro
 
kama hujafuata sheria za uchaguzi unategemea usikatwe kweli? wengine walikuwa hawajiamini wakaamua kufanya makosa ili waenguliwe tu
 
kama hujafuata sheria za uchaguzi unategemea usikatwe kweli? wengine walikuwa hawajiamini wakaamua kufanya makosa ili waenguliwe tu
Kwanini kukosea kunatokea kwa wapinzani tu?ni uhuni was chama tawala baada ya kulewa madaraka
 
Mambo ni mazito kidogo.

Zitto kasema kuwa Pemba hakuna mgombea wa ACT aliyeachwa . Wote 18 wameliwa vichwa.

View attachment 1549864

Aidha Zitto pia amesema jumla ya wagombea ubunge 44 wa ACT-Wazalendo Tanzania nzima wameenguliwa.

Hii ni hatari tupu.

View attachment 1549869
CCM mnaaka kuleta Vita Huko Pemba, faida itakuwa ya Nani? Kuna kila dalili kuvhocuea vurugu . Kuna kila dalili hiki Chama kuondolewa madarakani na jumuia za kimataifa. Ninafanya watanzania kuwa wajinga wakisingizia demokrasia na muungano.
 
Weyani tv inapatikana king'amuzi gani?? Haijafungiwa tu??
27 Aug 2020

ACT Wazalendo watowa kauli nzito pingamizi za Pemba, wasema liwalo sasa naliwe



Chama cha ACT Wazalendo kimesema sasa hakitakubaliana na hujuma yoyote dhidi ya wagombea wake kwenye uchaguzi wa Oktoba 2020 na kwamba watachukuwa hatua kali kukabiliana nazo.

Source : Weyani TV
 
Haaa haaa daah, siasa mmefanya peke yenu miaka mitano. huu woga unatokea wapi
Swali jingine Je baada ya kupora uchaguzi SM kwanini wauogope uchaguzi huu ilhali wenyeviti wote ni wao?
Kizuri si wote baina yao wanaofurahia kinachoendelea...
Dunia inazunguuka "...wamepita wengi na walisifiwa sana ila mwishowe walikuwa na anguko baya"
TUJISAHIHISHE...
 
Kinachoshangaza ni upinzani tu wanakiuka taratibu na unakuta wasomi wazuri wanaojua kujaza fomu vizuri kuliko hata wale wa chama tawala. Ingetokea wa chama tawala hata mmoja kaenguliwa kwa kosa hilo watu wangeona kuna usawa kwenye utendaji kazi wa tume. Tume imekuwa ikifanya kazi kibaguzi sana.

Uzuri wa zanzibar ni tofauti na bara huwa hawakubali kuendeshwa kibubusa.
Tuombe mungu machafuko yasitokee ila haki itendeke.
 
Zanzibar ni tofauti na Bara. Wataleta machafuko.
 
Back
Top Bottom