Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

a

Acha uchochezi, hujaonyesha chanzo cha ramani hizo mbili ulizotuwekea. pia practicability ya mpaka ni shughuli za kiuchumi za nchi. practice haionyeshi kuwa we are restricted that much beyond as you have just shown. acha uchochezi.
Kumbe mmelala mnasubiria kuona shughuli za kiuchumi ndipo mjue mmeingiliwa?
 
Tunaporwa nchi huku mwendazake alikuwa bize kupambana na Chadema & Kenya!
 
Wewe unaamua tu kubisha shughuli zinaendelea kila siku watu na naenda zaidi ya km 20 kufanya shughuli za uvuvi meli zinasafiri unatuletea habari ya km 20 mgogoro bado haujapatiwa ufumbuzi ndio maana hata shughuli za kuvuna gas na mafuta hazijaanza.Hakuna muwekezaji anatia pesa sehemu yenye mgogoro.
 
Awamu ya Tano ilijikita kudhibiti wapinzani bila kujali yaliyokuwa yakijiri mipakani mwetu. Itatugarimu pakubwa kuirejesha sehemu ya ziwa letu iliyotekwa kiulaini.
 
Yaliyoisibu malawi dhidi ya TZ ni kama vile Zanzibar dhidi ya Tanganyika
Kisiwa cha Fungu Mbara ni mali ya Zanzibar zama na zama na kuna Mafuta na Gesi nyingi,Bara wanadai ni kisiwa chao baada ya kugunduliwa uwepo wa Mafuta na gesi pale. Sisi wenyewe Hapa TZ tuna mgogoro wa kuikalia Zanzibar kimabavu isiendelee ki uuchumi kwa zaidi ya miaka 50 sasa kwa kisingizio cha Muungano Feki.

Sisi ni wa Dwazi nchi hii kwa kulala na Siasa kuweka mbele na kudharau uchumi na rasilimali .Wacha Malawiwatupe somo.

Leo Uganda wanachimba mafuta , Wakati zanzibar ilianza Exploration tangia miaka ya 50s.
Lakini Tanganyika wametuwekea kauzibe .
Hadi leo imebaki makabrasha tuu, etu hatuwezi kuchimba kwa vile hatuna sovereghnity.
To Hell,
 
Zanzibar ni tanzania na Tanzania ni zanzibar.

Hakuna mjadala kuhusu hili
 
Umetembelea hilo eneo kwa kutumia Google map? Au Google map kwako unaona haina nguvu yoyote katika hili?

Unasikitisha sana!
Unaonyesha ulivyo mjinga kung'ang'ania Google maps! Hizo ramani siyo za leo wala jana! Kwa taarifa yako ramani hizo zimekuwa zikichorwa tangu 1970! Malawi wamekuwa wakichora ramani kuonyesha ziwa lote liko kwao na sisi tumekuwa tukichora mpaka katikati ya ziwa. Aidha Malawi wamekuwa wakiliita Ziwa Malawi, Tanzania tukiliita Ziwa Nyasa na Mozambique wakiliita Ziwa Niassa.

Hivyo usibabaishwe na na Google maps!
 
Hapana, siyo jambo dogo hata kidogo; lakini ni jambo linalojulikana toka miaka na miaka, hata wakati wa Mwalimu Nyerere na Kamuzu Banda, jambo hilo lilijulikana hivyo, na michoro hiyo ilikuwepo hivyo hivyo unavyoisemea hapa.
 
Mkataba wa heligoland wa mwaka 1890 uliwapa ziwa lote malawi shida inaanzia hapo. Uingereza wanajua hivyo, wajerumani nao wanajua hivyo,
 

Ndio yale yale ya mayahudi kuvamia na kwendelea kumega ardhi ya wapalestina. Sasa yanahamia kwetu.
 
Sio kweli mkuu.

Kilichofanya nikaanzisha hii mada ni mabadiliko ya ramani kupitia Google earth
Wewe Labda mgeni. Kuna ramani nyingi tofauti kutegemea na upande.

hataramanu ya mkoloni ilikuwa inaonyesha hivyo. Nafikiri tokea 1890 iliwekwa hivyo
 
Ta
Ni ujinga wamalawi kutaka ziwa lote liwe lao. Ni kutafuta migogoro ya kipuuzi tu isiyo na kichwa wala miguu. Ni tamaa na kutumika tu
Tatizo ni mali asili iliyopo humo ziwani, hebu fikiria miaka mingi tumeishi kwa kutumia ziwa bila vikwazo kwa kuzingatia mpaka upo katikati lakini sasa ni hayo yanaibuka
 
Mkuu hivi kulikuwa na mkataba wa pili wa kugawanywa ziwa kweli? Ni onavyo Mimi Kama ulikuwepo basi ni wa msumbiji chini ya wareno na Malawi chini ya waingereza na sio tanganyika. Nakumbuka Bernard membe alikuwa anauelezea huu mgogoro kipindi kile cha jk hakuelezea uwepo wa mkataba wa pili zaidi ya kulaumu huo mkataba wa mwanzo ulivyowanyima haki watanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…