Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Dah! Kwahiyo suluhisho ni nini mkuu?
 
Safi sana! mleta mada tusaidie kujua!
Hoja hapa ni mpaka kuonesha ziwa lote lipo Malawi!
Miaka michache nyuma waliweka alama nyekundu katikati ya ziwa kuonesha ziwa hilo bado linazozaniwa na mataifa mawili... Leo ile alama nyekundu haipo na mpaka umesogezwa kwa kumega zaidi ya kilomita 20 za nchi yetu.

Umeelewa?
 
Mrejesho ndio huo ramani imebadilishwa kwa kukwapua kilomita 20 ndani ya nchi yetu
 
Tena serikali ya Malawi imeshaanza mazungumzo na kampuni la Uingereza kuja kuchimba hizo rasilimali
 
Natamani vita ije ili mshindi akabidhiwr ziwa nyasa.......,
 
Achana na google maps, kwani ile meli iliyopona ajali hivi karibuni ilikuwa inafanya safari kwenye ziwa gani? Jiulize unaweza kufanya safari kwenye ziwa ambalo huna umiliki nalo?
 
huo ote ni udhaifu wa mwendazake.
anahangaika na kuiba hela za wafanyabiasha na kununua wapinzani kwa kuogopa kunyang'anywa madalaka huku wenzake wanabadirisha ramani.
dipromasia zimemshinda na kila kitu hovyo.
 
Ni ujinga wamalawi kutaka ziwa lote liwe lao. Ni kutafuta migogoro ya kipuuzi tu isiyo na kichwa wala miguu. Ni tamaa na kutumika tu
 
Sasa inakuwaje kuhusu gesi, labda mabeberu wamegundua hatuna mbinu mpya,kwa uzoefi wa gesi ilivyoporwa na uchina,defense unit wako wapi?
 
Ramani iko hivo miaka mingi kabla hata ya Google earth. Kuna siku kwenye ofisi ya ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania ilionekana ramani yenye kuonesha ziwa lote liko Malawi. Ramani za kimataifa zinaliita ziwa Malawi badala ya Nyasa, ni kama uamue kuliita ziwa Nyanza utaliita mwenyewe wengine wataendelea kuliita Victoria.

Malawi wakileta ushahidi wao lazima tutumie akili kuupinga. Sio kukariri resolution ya UN iliyo generalized. UN hawakugawa hizi nchi, waliogawana Tz na Malawi ni Wajerumani waliokuwa German East Africa (ikiwemo Tanganyika) na Waingereza waliokuwa Malawi. Ukitazama Heligoland treaties mbili ndio mpaka ule umewekwa. Sheria za mipaka ya Afrika zinaheshimu mgawanyo wa wakoloni bila kuubadilisha. Sasa Malawi wana treaty ya kwanza inayoonesha ziwa lote ni lao. Treaty ya pili inayoonesha ziwa linagawanywa tulitakiwa tuwe nayo sisi. Hatuna

Angalizo: Nimetumia memories za zamani nilivyoelewa hili suala. Sina uhakika sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…