Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Lazima yupo anayeujuwa ukweli.
Lazima yupo anayejuwa kwa nini ikawa hivyo
Lake Tanganyika na Lake Victoria mipaka ipo katikakati kwa nini Lake Nyasa iwe tofauti...???
Dr. Mwinyi Rais wa ZNZ amekataa kusifiwa sifiwa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ramani ya google earth inaonyesha hivyo tangu zamani. Na wamalawi hilo ziwa huliita malawi sisi tunaliita Nyasa.
Lakini hili swala bado lipo kwenye mazungumzo na marais wa nchi za SADC .
Ninachokiona huko mbeleni, Malawi ikija kujiimarisha kijeshi kuliko Tanzania inalichujua hilo ziwa lote.
Hapo ndipo idara za usalama wa taifa zinatakiwa kufanya kazi kuhakikisha hili halitokei.
 
Sasa inakuwaje kuhusu gesi, labda mabeberu wamegundua hatuna mbinu mpya,kwa uzoefi wa gesi ilivyoporwa na uchina,defense unit wako wapi?
Wakigundua hatuna mbinu mpya ndio waje kumega ardhi yetu?
 
Dah! Kwahiyo tukubali hatuna kitu kwenye ziwa nyasa 🥺
 
Swala la mpaka unaita swala dogo?
 
Asante kwa uzalendo ulionao kwa nchi yako wa hali ya juu..hao wamalawi wanajifurahisha tu. Ni panya wadogo sana. Kuna kampuni za kibeberu zinataka kuchimba mafuta hapo,ndo zinasogeza mpaka.
 
Wandugu,
Toeni taharuki zenu, hiyo ramani iko hivyo hata kabla ya Tanganyika kupata uhuru wake.
Ni ramani ilichorwa na wakoloni. Haiongezi wala kuondoa kitu.

Ila historia inawapiga chenga wengi
Mkuu umekubali tumegwe? Kwenye hii dunia wenye akili wapo tayari hata kupora nchi nzima ila wewe umekubali sehemu ya muhimu kama ile ambayo raia wetu wameitumia miaka na miaka kuchukuliwa kimasihara
 
Kama ipo hivyo siku zote mbona Tanzania tunafanya shughuli zetu kama kawaida kwenye hilo ziwa?

Ingekua uongeayo ni kweli, basi tusingedhubutu kufanya shuguli za kiuchumi kwenye hilo ziwa
 
Asante mkuu wewe unayo akili ya kuwaza mbali
 
Mipaka ilikuwepo ila siyo katika hali ya sasa.

Unataka kusema chief Mkwawa hakuwa na mpaka kwenye eneo lake la utawala ?
Nakubaliana na wewe ila mipaka tuliyokuwa nayo ilikuwa ya kutaja maeneo tu lakini ikitokea tatizo machifu wote walikua kitu kimoja.

Leo hii inaweza kushambuliwa Kenya alafu sisi huku tukabaki kuchekelea
 
Hiyo ramani yako ya pili inaonyesha hujaisoma vizuri. Labda tatizo lako ni English hamna.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Malawi kaamua kucheza kama pele apo inabidi tusimwachie kizembe
 
Mimi naona mihemko unayo wewe.

Ramani ya mwaka 2014 niliona mpaka wa rangi nyeupe ulipita katikati ya ziwa, muda mfupi baadae ramani ikawa iko pale pale lakini imechorwa kwa rangi nyekundu kuashiria kuna mzozo.

Leo katika ramani mpaka umesogezwa kilomita 20 kwa upana na kilomita zaidi ya 220 kwa urefu. Hili ni jambo dogo kwako?
 
Sio kweli mkuu.

Kilichofanya nikaanzisha hii mada ni mabadiliko ya ramani kupitia Google earth
 
Asante kwa uzalendo ulionao kwa nchi yako wa hali ya juu..hao wamalawi wanajifurahisha tu. Ni panya wadogo sana. Kuna kampuni za kibeberu zinataka kuchimba mafuta hapo,ndo zinasogeza mpaka.
Ni kampuni za Uingereza mkuu. Alafu haohao Uingereza ndio waliosababisha huu mgogoro maana Ujerumani wao walisema ikiwa mpaka wa nchi na nchi umepita kwenye maji, basi ni sharti mpaka huo uwe katikati ya maji pande zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…