ichumu lya
JF-Expert Member
- Aug 11, 2016
- 2,651
- 2,790
Hii ina ukweli gani wakuu?
ZIWA VICTORIA LIMEWAHI KUKAUKA MAJI YOTE MARA TATUZiwa Victoria ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani baada ya Ziwa kuu la Kaskazini nchini Marekani.
Ziwa hili ambalo lina kina cha mita 83 ni moja ya maziwa machanga katika historia ya dunia kwa maana hayana miaka zaidi ya milioni moja toka yafanyike. Ziwa Victoria lilitokea takribani 400,000 iliyopita.
Ziwa Victoria lina historia ya kipekee kijiografia duniani likiwa ni moja ya ziwa kuu ambalo limekutwa na tukio la kukausha maji yake yote mara tatu.
Zaidi ya miaka 17,300 iliyopita ziwa hili ambalo ni chanzo kikuu cha mto Nile (white Nile ) ingawa chanzo halisi ni mto Kagera ,
lilikauka kabisa na kusababisha ukame mkubwa eneo lote la Victoria basin na nchi zote ambazo mto Nile unapita lakini athari kubwa ikiwa nchini Misri.
Ziwa hili lilijaa tena maji miaka 14,700 iliyopita hii ina maana kuna...miaka 2700 , ziwa hili lilikuwa kavu kabisa na flow pekee ya maji kiasi sana katika bonde la mto Nile, ilitegemea chanzo pekee cha Ziwa Tana ambalo halikuweza kuyasukuma maji kufika Misri!.