Ziwa Victoria limewahi kukauka maji yote mara tatu

Ziwa Victoria limewahi kukauka maji yote mara tatu

Ain't nothing like that, for what extent unaweza ku verify hiyo statement yako ya kuwa lilikauka miaka 17,300. Toa evidence au reference ya kitabu hata kimoja kusapoti hii point yako. Ujue hata km ni zaman, lkn history never dies, tungejua tuu... Hasa sis wana bukoba
Acha ubishi ndugu

Japo umesema jambo la maana kuhusu umuhimu wa ushahidi wa kihistoria. Madai kuhusu kukauka kwa Ziwa Victoria miaka 17,300 iliyopita yanatokana na tafiti za kisayansi za kijiolojia na siyo kumbukumbu za kihistoria zinazopatikana moja kwa moja kwenye vitabu vya historia au mila na tamaduni za watu wanaoishi karibu na ziwa hilo, kama watu wa Bukoba. Kwa sababu masuala haya yanahusu mabadiliko ya kijiolojia ya zamani sana kipindi ambacho huenda kulikuwa pia hakuna wakazi kando ya ziwa hili, ils fahamu kuwa tafiti hufanyika kwa kutumia mbinu maalum za kisayansi.

1. Tafiti za Kijiolojia na Mabadiliko ya Hali ya Hewa Ushahidi unaotumika mara nyingi unatokana na tafiti za mchanga wa ziwa (lake sediments), uchambuzi wa vidimbwi vya kale (paleohydrology), na utafiti wa kimaabara wa rekodi za mabadiliko ya hali ya hewa (paleoclimate records). Kwa mfano, utafiti wa Johnson et al., (1996) na Stager & Johnson (2008) walichunguza uchambuzi wa mchanga kwenye kina cha Ziwa Victoria na wakapata dalili kuwa kipindi cha mwisho wa Enzi ya Barafu (Ice Age) kiliathiri sana maziwa mengi makubwa duniani, yakiwemo Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, na Ziwa Malawi. Tafiti hizi zilionesha kuwa kuna vipindi ambavyo mito na maziwa haya yalikuwa na kiwango cha maji chini sana au hata kukauka kabisa, jambo linalowezekana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

2. Ushahidi Kutokana na Sampuli za Mchanga Katika utafiti mwingine, sampuli za kijiolojia za mchanga na viumbe vidogo vya zamani vilivyohifadhiwa katika udongo wa kina cha Ziwa Victoria vimeonesha kuwa mabadiliko makubwa ya kiwango cha maji yalitokea kipindi cha miaka 15,000 hadi 17,000 iliyopita. Hii inalingana na kile kinachojulikana kama "African Humid Period," ambapo maeneo mengi ya Afrika yalikuwa kwenye hali ya ukame mkali au mvua nyingi. Matokeo haya yalitokana na tafiti za watafiti kama Talbot & Delibrias (1977) waliotumia vipimo vya kaboni na oksijeni kwenye vipande vya mchanga kuchunguza mabadiliko ya maji.

3. Vyanzo vya Kitaalamu na Utafiti wa Karibuni Ili kuelewa zaidi, unaweza kutafuta makala za kisayansi zenye uhakika zinazopatikana katika majarida ya kitaalamu kama Quaternary Research, Paleolimnology, na Journal of African Earth Sciences. Haya majarida yana mfululizo wa makala kuhusu mabadiliko ya hali ya maji kwenye maziwa ya Afrika Mashariki.

Rejea za Kitafiti

1. Johnson, T.C., et al. (1996). "Late Pleistocene Desiccation of Lake Victoria and Rapid Evolution of Cichlid Fishes." Science.

2. Stager, J.C., & Johnson, T.C. (2008). "A 12,400 14C yr Offshore Diatom Record from East Africa." Quaternary Research.

3. Talbot, M.R., & Delibrias, G. (1977). "Holocene Variations in the Level of Lake Bosumtwi, Ghana." Nature.
 
Uongo.hakuna kitu kama hicho.kwanza Kwa miaka hiyo hapa kuwa na uharibifu wa mazingira ambao ungepelekea kukauka Kwa vyanzo vya maji maana idadi ya watu walikuwa wachache sana.Hawa wanajiografia wanapenda kutaja miaka mingi ya mamilioni ili kuhalalisha uongo wao.
Husikariri kuwa uharibifu wa mazingira unaosababishwa na binadamu tu.

Mabadiliko ya tabianchi (tabia za nchi) na uharibifu wa mazingira unayotokea duniani yanaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, ambayo ni pamoja na:

1. Mabadiliko ya Asili

Mzunguko wa Jua: Mabadiliko katika mzunguko wa jua na kiwango cha joto linalotolewa na jua huathiri hali ya hewa na tabianchi. Mzunguko huu unaweza kuathiri mvua, joto, na hali ya hewa kwa ujumla. Mfano kipindi fulani huko kale kulitokea kioindi cha Ice Age, au kipindi cha baridi kali, ni kipindi ambacho kimekuwa kikitokea mara kadhaa katika historia ya dunia na kilisababisha maziwa mengi kukauka. Hapa kuna mambo kama Mabadiliko ya umbo la mzunguko wa Dunia kuzunguka jua kutoka kwa mzunguko wa mduara hadi kwa mzunguko wa mduara wa oval. Soma mizunguko ya jua kama Milankovitch cycles, Eccentricity, Axial Tilt, na Precession ambayo inaweza kubadilisha tabia za mazingira na hali ya hewa ya Dunia.

Mabadiliko ya Kijiolojia na miamba: Mabadiliko ya tectonic, kama vile uhamaji wa mabamba ya ardhi (sahani za Miamba), yanaweza kuathiri hali ya hewa kwa mamilioni ya miaka. Mifano ni vilevile mabadiliko ya milima na bonde, ambayo yanaweza kubadilisha mwelekeo wa upepo na mvua.

Vikosi vya Maji (Water Currents): Maji ya baharini au kwenye maziwa yanaweza kuathiri hali ya hewa, kama vile mabadiliko katika mifumo ya mvua kutokana na joto la bahari (El Niño na La Niña). Wote tunakumbuka mvua za El Niño za mwaka 1996 jinsi zilivyo sababisha majanga kwenye mazingira
 
Uongo.hakuna kitu kama hicho.kwanza Kwa miaka hiyo hapa kuwa na uharibifu wa mazingira ambao ungepelekea kukauka Kwa vyanzo vya maji maana idadi ya watu walikuwa wachache sana.Hawa wanajiografia wanapenda kutaja miaka mingi ya mamilioni ili kuhalalisha uongo wao.
Unakubaliana na historia? Je kumewahi kuwepo na ghalika?
 
Ain't nothing like that, for what extent unaweza ku verify hiyo statement yako ya kuwa lilikauka miaka 17,300. Toa evidence au reference ya kitabu hata kimoja kusapoti hii point yako. Ujue hata km ni zaman, lkn history never dies, tungejua tuu... Hasa sis wana bukoba
Hakuna watu wasiojari historia na vitu vingine vya kwao kama Wahaya. Kwenye hili kaa kushoto lete utetezi mwingine
 
Vizazi hurithishana matukio makubwa kama hayo.

Babu ➡️ Babu ➡️ Babu ➡️ sisi
Kuna sababu mbalimbali zinaziweza kupelekea historia hii ya ziwa kukauka kutokujulikana kwa wakazi. Mfano

1. Kutokuwepo kwa wakazi wakati ziwa linakauka: kwa sababu tumesema mara ya mwisho tangu ziwa likauke ni miaka 17,300 maana yake ni miaka mingi, kimaandiko hata Yesu hakuwepo, hii inamaana yesu ana miaka 2,000 tu tangu aondoke. Hivyo uenda kanda ya ziwa hapakuwepo watu au kama walikuwepo walitoweka, na kama hawakutoweka hakutilia maanani kwenye simulizi.

2 . Kukosa Kuwepo kwa Kumbukumbu: Mambo mengi ya kihistoria yanategemea kumbukumbu za watu, maandiko, na ushahidi wa kimazingira. Ikiwa hakuna mtu aliyeandika au kuhifadhi historia, matukio hayo yanaweza kupotea. Mfano Babu au Bibi aliyekuwepo akafariki bila kuandika au kusimulia historia hiyo basi vizazi vijavyo havitaweza kujua chochote.

3. Mabadiliko ya Jamii na Utamaduni: Mabadiliko katika jamii, kama vile uhamaji wa watu, kupotea kwa lugha, au mabadiliko ya dini, yanaweza kuathiri jinsi watu wanavyokumbuka na kuwasilisha historia.

4. Mizizi ya Uelewa wa Kihistoria: Wakati mwingine, watu hujenga uelewa wa kihistoria kulingana na uzoefu wao wa kibinafsi na matukio yanayowazunguka, na hivyo kusababisha kutofautiana kati ya hadithi za jamii tofauti. Kupelekea simulizi kupindishwa.

5. Ukosefu wa Uthibitisho: Watu wanaweza kukosa ukweli wa kihistoria kama hawana ushahidi wa moja kwa moja au simulizi kutoka kwa wazee wao. Watu wanaweza kuona unawadanganya kama vile unavyoona kwenye andiko hili

6. Uhamasishaji Imara: Watu wanaweza kukataa ukweli wa kihistoria kama unapingana na imani zao au maadili ya jamii yao. Hii inaweza kupelekea kutokukubali ukweli wa kisayansi, kama vile kukauka kwa Ziwa Victoria.
 
I'm a native from Bukoba region, sio kuona tu, bali sjawahi kuskia something of that nature, eti ziwa letu limewahi kukauka, never, mababu na mababu hawajawai narrate such a historical disaster. However, it'll never even happen, coz that will then be a cataclysmic impoderabilia at its peak.
Acha ubishi bwenga, vipi Mlimani City ulikuwepo?
 
Hii ina ukweli gani wakuu?​
dailytalkz_'s profile picture's profile picture

ZIWA VICTORIA LIMEWAHI KUKAUKA MAJI YOTE MARA TATU

Ziwa Victoria ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani baada ya Ziwa kuu la Kaskazini nchini Marekani.

Ziwa hili ambalo lina kina cha mita 83 ni moja ya maziwa machanga katika historia ya dunia kwa maana hayana miaka zaidi ya milioni moja toka yafanyike. Ziwa Victoria lilitokea takribani 400,000 iliyopita.

Ziwa Victoria lina historia ya kipekee kijiografia duniani likiwa ni moja ya ziwa kuu ambalo limekutwa na tukio la kukausha maji yake yote mara tatu.

Zaidi ya miaka 17,300 iliyopita ziwa hili ambalo ni chanzo kikuu cha mto Nile (white Nile ) ingawa chanzo halisi ni mto Kagera ,

lilikauka kabisa na kusababisha ukame mkubwa eneo lote la Victoria basin na nchi zote ambazo mto Nile unapita lakini athari kubwa ikiwa nchini Misri.

Ziwa hili lilijaa tena maji miaka 14,700 iliyopita hii ina maana kuna...miaka 2700 , ziwa hili lilikuwa kavu kabisa na flow pekee ya maji kiasi sana katika bonde la mto Nile, ilitegemea chanzo pekee cha Ziwa Tana ambalo halikuweza kuyasukuma maji kufika Misri!.
View attachment 3140744
Watu wanabisha ila inaweza kuwa ni kweli maana kipindi hiko sidhani kama kulikuwa na kiumbe binadamu anaishi kanda ya ziwa isee.

Ila kupitia hadithi za vitabu vya dini tunaambiwa misri ilikubwa na ukame mkubwa sana kipindi waziri mkuu yusuph na pia baadae ikafuata neema kubwa sana hapo misri hadi kupelekea mataifa jirani kukimbilia hapo.

Sasa huu ni unaweza kutumika kama ushahidi maana misri inategemea mto nile wenye chanzo chake kutoka ziwa Victoria Tanzania
 
Aiseee hapana,mimi ndugu zangu wangu kisiwan ukerewe sijawah sikia wakisema waliwah kwenda mwanza kwa mguu

Toka 1990 hili ziwa naliona sana sana huwa maji yanapungua tu sio kuisha yote
Anaongelea miaka milioni iliyopita au hujui kusoma
 
Back
Top Bottom