Ziwa Victoria limewahi kukauka maji yote mara tatu

Ziwa Victoria limewahi kukauka maji yote mara tatu

Akili yangu ikiwa nzuri isiwe nzuri, inakuhusu?

Mimi simwiti mtu kondoo, wenyewe wanaitana kondoo. Wewe kondoo au siyo kondoo?
Mwanakondoo asameheyae dhambi za Ulimwengu ameshinda tumfuate.
 
Aiseee hapana,mimi ndugu zangu wangu kisiwan ukerewe sijawah sikia wakisema waliwah kwenda mwanza kwa mguu

Toka 1990 hili ziwa naliona sana sana huwa maji yanapungua tu sio kuisha yote
Sasa hivi yanazidi nenda Garden kama za kamanga, kishimba, hotel za malaika na yatch club za Mwanza jinsi maji yamejaa.
 
Ni kweli kuwa Ziwa Victoria limepitia mabadiliko makubwa ya kihistoria, ikiwa ni pamoja na kipindi ambacho lilikaushwa kabisa maji mara kadhaa. Tafiti za kijiolojia zinaonyesha kuwa Ziwa Victoria lilikaushwa angalau mara tatu katika historia yake, hasa wakati wa mabadiliko ya hali ya hewa na kipindi cha baridi kali duniani (ice age). Hii ilitokea kutokana na mabadiliko ya kijiografia na hali ya hewa yaliyosababisha ukosefu wa mvua katika eneo hilo, hivyo kuathiri kiwango cha maji ya ziwa.

Kwa mujibu wa masomo ya kihistoria ya kijiolojia, ziwa hili lina umri wa takriban miaka 400,000 na mara ya mwisho lilikaushwa ilikuwa takriban miaka 17,300 iliyopita. Kipindi hicho kilikuwa na athari kubwa, sio tu kwa ziwa hilo bali pia kwa mito inayotegemea maji yake, kama vile Mto Nile. Kutokuwepo kwa maji ya kutosha kulisababisha ukame mkubwa katika bonde la Ziwa Victoria na maeneo yote ambayo Mto Nile unapita, ikiwa ni pamoja na nchi ya Misri, ambayo ilitegemea Mto Nile kwa kilimo na maisha ya watu.

Baadaye, takriban miaka 14,700 iliyopita, Ziwa Victoria lilianza kujaza maji tena kutokana na kuongezeka kwa mvua katika bonde la Nile, na hivyo kusaidia urejeshaji wa mtiririko wa maji kuelekea Mto Nile. Hata hivyo, kuna kipindi cha miaka 2,700 ambapo ziwa lilibaki kavu, na mtiririko wa maji uliokuwa mdogo sana ulitegemea vyanzo vingine vidogo, kama vile Ziwa Tana, ambavyo havikuwa na uwezo wa kusukuma maji kufika Misri kama ilivyokuwa awali.

Kwa hiyo, historia hii inaonesha jinsi Ziwa Victoria linavyoweza kuathirika na mabadiliko ya hali ya hewa na kijiografia, na umuhimu wake kwa mtiririko wa maji kwenye Bonde la Nile na nchi zinazoizunguka, hasa Misri.
Pprojo
 
Kuna vitu vingine ukivisema tu hata kichaa hawezi kukubali.

Huo ni uongo wa wa zungu wenu ambao Kila kitu wanawatafunia then wanawapa mmeze tu.

Kwa kifupi sisi Ziwa letu Nyanza lililopo mwanza na mikoa jirani halijawahi kukauka. Labda Hilo la wazungu
 
Hii ina ukweli gani wakuu?​
dailytalkz_'s profile picture's profile picture

ZIWA VICTORIA LIMEWAHI KUKAUKA MAJI YOTE MARA TATU

Ziwa Victoria ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani baada ya Ziwa kuu la Kaskazini nchini Marekani.

Ziwa hili ambalo lina kina cha mita 83 ni moja ya maziwa machanga katika historia ya dunia kwa maana hayana miaka zaidi ya milioni moja toka yafanyike. Ziwa Victoria lilitokea takribani 400,000 iliyopita.

Ziwa Victoria lina historia ya kipekee kijiografia duniani likiwa ni moja ya ziwa kuu ambalo limekutwa na tukio la kukausha maji yake yote mara tatu.

Zaidi ya miaka 17,300 iliyopita ziwa hili ambalo ni chanzo kikuu cha mto Nile (white Nile ) ingawa chanzo halisi ni mto Kagera ,

lilikauka kabisa na kusababisha ukame mkubwa eneo lote la Victoria basin na nchi zote ambazo mto Nile unapita lakini athari kubwa ikiwa nchini Misri.

Ziwa hili lilijaa tena maji miaka 14,700 iliyopita hii ina maana kuna...miaka 2700 , ziwa hili lilikuwa kavu kabisa na flow pekee ya maji kiasi sana katika bonde la mto Nile, ilitegemea chanzo pekee cha Ziwa Tana ambalo halikuweza kuyasukuma maji kufika Misri!.
View attachment 3140744
Hadithi za kusadikika
 
Halijakauka ila siku zinavyozidi kwenda maji yanapungua fukwe inarudi ndani
 
Fossil evidence, spectrometer, deposition, sedimentology, umri wa miamba n.k
Wapelekeni watoto shule wakasome tuache kutia aibu ndogondogo.
Usinilazimishe sasa, haya fossil evidence inathibitisha vipi ziwa lilikauka mara 3, umri wa miamba unathibitisha vipi ziwa kukauka? Spectrometer unajua ni kipimo cha nini haya kinapima kukauka kwa ziwa?

Unaweza ukasoma lakini usielimike mkuu.. Nipe proof kwa namna gani waliona ziwa limekauka.. Hayo ni makisio yao tu, kwa sababu hii na ile huenda lilikuwa limekauka lakini sio 100% na sio kila wakisemacho wao mie nipinge, wanasayansi wangapi waliweka jambo hivi likaaminika miaka nenda rudi kisha baadae akatokea mwingine na kusahihisha?

Wewe ni katika wale BINADAMU WA KWANZA ALIKUWA NYANI.
 
Back
Top Bottom