Ziwa Victoria limewahi kukauka maji yote mara tatu

Akili yangu ikiwa nzuri isiwe nzuri, inakuhusu?

Mimi simwiti mtu kondoo, wenyewe wanaitana kondoo. Wewe kondoo au siyo kondoo?
Mwanakondoo asameheyae dhambi za Ulimwengu ameshinda tumfuate.
 
Aiseee hapana,mimi ndugu zangu wangu kisiwan ukerewe sijawah sikia wakisema waliwah kwenda mwanza kwa mguu

Toka 1990 hili ziwa naliona sana sana huwa maji yanapungua tu sio kuisha yote
Sasa hivi yanazidi nenda Garden kama za kamanga, kishimba, hotel za malaika na yatch club za Mwanza jinsi maji yamejaa.
 
Pprojo
 
Kuna vitu vingine ukivisema tu hata kichaa hawezi kukubali.

Huo ni uongo wa wa zungu wenu ambao Kila kitu wanawatafunia then wanawapa mmeze tu.

Kwa kifupi sisi Ziwa letu Nyanza lililopo mwanza na mikoa jirani halijawahi kukauka. Labda Hilo la wazungu
 
Hadithi za kusadikika
 
Halijakauka ila siku zinavyozidi kwenda maji yanapungua fukwe inarudi ndani
 
Fossil evidence, spectrometer, deposition, sedimentology, umri wa miamba n.k
Wapelekeni watoto shule wakasome tuache kutia aibu ndogondogo.
Usinilazimishe sasa, haya fossil evidence inathibitisha vipi ziwa lilikauka mara 3, umri wa miamba unathibitisha vipi ziwa kukauka? Spectrometer unajua ni kipimo cha nini haya kinapima kukauka kwa ziwa?

Unaweza ukasoma lakini usielimike mkuu.. Nipe proof kwa namna gani waliona ziwa limekauka.. Hayo ni makisio yao tu, kwa sababu hii na ile huenda lilikuwa limekauka lakini sio 100% na sio kila wakisemacho wao mie nipinge, wanasayansi wangapi waliweka jambo hivi likaaminika miaka nenda rudi kisha baadae akatokea mwingine na kusahihisha?

Wewe ni katika wale BINADAMU WA KWANZA ALIKUWA NYANI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…