Lengo kubwa la Magufuri ilikuwa ni kubana matumizi alibana kwa namna nyingi ikiwemo hiyo ya mishahara hewa, daktari, mwalimu, nesi, n.k hawa watu wakigushu vyeti tutakuwa na uhakika gani na taaluma zao?? Kazi zao zinahitaji taaluma ndio maana wamesomea hizo kazi...
Kulikuwa na mambo mengi sana ya hovyo
1. Baadhi ya viongozi walitengeneza majina feki ya wafanya kazi na maanisha kuwa yalikuwa majina tupu
2. Marehemu kuendelea kulipwa
3. Watu kufanya kazi za kitaaluma bila kuwa na taaluma husika
4. Hongo za namna mbalimbali
Njia pekee yakubaini haya yote ilikuwa ni ukaguzi wa vyeti
Ukiwa na cheti feki ukibaki nacho ndani nani atakuuliza kuhusu hilo? Waligushi vyeti feki ili wapate kazi serikalini walipwe fedha za serikali lakini hawakuwa na vigezo vya kufanya kazi hizo za kitaaluma...
Kwahiyo hapa jambo la muhimu alilolifanya magu ni kuzuia fedha za serikali kuibiwa hovyo,, kuhusu vyeti hili halikuwa lengo kuu kwahiyo hao wa malori uliosema hata wangekuwa na vyeti feki wangebaki navyo ndani tu wala wasinge ulizwa na mtu yeyote mtu halipwi fedha kwa kuwa na cheti analipwa kwa kufanya kazi lakini awe na vigezo vya kufanya kazi...
Huu ni wizi uliyo fanywa na viongozi walio kuwepo kipindi hicho lakini wewe bado unashindwa kutambua jitihada hizi, je wewe ungekuwa raisi ungefanya nini kuondoa hii hali ya wizi bila kuwa kagua vyeti vya wafanyakazi wako??? Au cheti kipo kwa ajiri ya nini?? Mambo mengine haya hitaji kuwa mwanachama wa chama fulani au hadi umpende sana mtu fulani ndipo uelewe jitihada zake.. kuendekeza uchama, udini, ukabila n.k huwezi kuwa mtu wa haki wala huwezi kutambua jitihada za mtu mwingine zaidi utafikiria kukosoa tu jitihada za wengine
Hapa hoja yako ilikuwa ni kwamba Magufuri aliogopa baadhi ya watu, lakini unashindwa kutambua kuwa hao wote alio waogopa alikuwa anashirikiana nao kwenye kazi kiasi gani? Ukaleta hoja za udereva kuwa aliwazingua sijui aliwazingua vipi lakini hawa madereva elimu zao ni veta huko nao wana taratibu zao za ukaguzi ndio maana askari wa ukaguzi wapo barabarani muda wote,, mimi hoja yangu ilikuwa ni watu kufanya kazi zinazo hitaji utaalamu wakusomea lakini wao wamelazimisha mambo tu
Ebu punguza matusi uwe unaeleza vizuri ili ueleweke