Zoezi la Vyeti Feki Kenya: Rutto Asiingie Mtego wa Magufuli

Zoezi la Vyeti Feki Kenya: Rutto Asiingie Mtego wa Magufuli

Usichague cha kusoma, bali soma na kuelewa. Hatutetei wagushi vyeti bali tunasema zoezi la kuondoa wagushi vyeti lilikuwa la ubaguzi. Kuna sekta hazikuguswa. Mbona liko wazi tu.

Kweli unamtoa dreva aliyegushi cheti cha Form IV na unamuacha Daudi Bashite anayetumia cheti na majina ya Paul Makonda awe RC Dar?

Naomba Lyetu uni jibu hilo kwa utulivu
Leta uthibitisho hapa, sichangii fununu au umbea.
 
Magufuli alifanya hili zoezi la vyeti feki kwa Tanzania lakini alikuwa selective. Magufuli hakugusa TPDF, Bunge na Wakuu wa mikoa. Hata Polisi na TISS nao hawakuguswa. Halafu alidhulumu mafao ambayo ni jasho lao.

Nashauri tu kuwa kama William Rutto anataka lifanikiwe alifanye across-the-board kwa sekta zote, asiwe selective

View attachment 2969921
Hujui kitu kuhusu hii issue. Au ulikuwa mhanga?
 
Hujui kitu kuhusu hii issue. Au ulikuwa mhanga?
Wewe pimbi mimi nina vyeti vyote halali vya kusomea elimu ya Tanzania kasoro PhD.

Ila siwezi kuunga mkono DOUBLE STANDARDS katika mchakato wa kuwatoa. Elewa neno Double Standards. Kama huelewi uliza, siyo mnaunga mkono tu kama kuku wasiokuwa na vichwa
 
Lyetu ndilo jina langu halisi, leta ushahidi Makonda alitumia cheti cha mtu mwingine.
Ushahidi ni kwamba jina halisi la RC Arusha ni Daud Albert Bashite. Soma Jamhuri la tarehe 21 Machi, 2017

Au kiambatisho hiki Uchunguzi wa Bashite | JAMHURI MEDIA
Screenshot_20240527_124241_Google.jpg
 
TPDF hakuna vyeti feki kwa vile TPDF huto elimu bure wa askari wake. Zamani walikuwa wanatoa elimu ya sekondari yotre kuanzia form 1 hadi vyuo (Nadhani unaijua sekondari ya TPDF Makongo), siku hizi nadhani wanaanzia form 5 hadi vyuo.
Vyeti feki ni elimu au kutumia jina la mtu? Hao vyeti feki sio kwamba walifoji vyeti ila walitumia majina ya mtu mwingine kuendelea na masomo elimu ya juu.

Kwahiyo jeshini wapo wengi tu walifeli la saba wakarudia kwa jina la mtu mwingine.
 
Acha ujinga wewe kwahiyo unataka kusema Magufuli aliwaogopa hao .. 😂 yaani apambane na watu wakubwa na mataifa makubwa afu awaogope TPDF, wakuu wa mikoa n.k wewe nawe ni unapenda kuzusha mambo usioyajua

Magufuli alifahamu anacho kifanya, sio kila kazi serikalini ni lazima uwe na cheti, alikuwa anaangalia uwezo wa mtu kufanya kazi na kuendana na matarajio yake, lakini kuna hizi kazi zilizo kuwa zina hitaji utaalamu wa hali ya juu kama ualimu, udaktari n.k
watu walikuwa wanachukua hela za serikali lakini hakuna walilikuwa wanalifanya zaidi zaidi kuendelea kuharibu taifa na kusababisha majanga kutokana na wao wenyewe kukosa utaalamu kwenye nafasi zao
Mkuu kwa Tpdf ata askari akiwa na vyeti feki siyo mbaya wao wanakuwa walinzi wa gatin na kufyeka tu makambini, tofauti na sekta ya Afya, Elimu, Mahakama, na Tamisemi
 
Nimesoma comments za baadhi ya wajinga, nimechafukwa hadi nimeshindwa kumalizia biriani langu.

Tumefika huku kwenye kutetea wagushi nyaraka? Tunataka wagushi nyaraka waachwe? Tunataka wagushi nyaraka walipwe?

Ama kweli Africa ni bara la wajinga.
Pole mkuu,kama tuliwahi kuwa na Rais kama Jiwe sasa unategemea nin
 
TPDF hakuna vyeti feki kwa vile TPDF huto elimu bure wa askari wake. Zamani walikuwa wanatoa elimu ya sekondari yotre kuanzia form 1 hadi vyuo (Nadhani unaijua sekondari ya TPDF Makongo), siku hizi nadhani wanaanzia form 5 hadi vyuo.
Kichuguu mkongwe akiwa kazini JF.
 
Back
Top Bottom