TANZIA Zuchi Zuchero, mpiga picha na Mwandishi wa Habari afariki kwa ajali

Sina la kusema mkuu, maana kuna wanaotegemea kuishi kwa hizo boda hivyo siwezi kuziita takataka labda sheria zikaziwe, usalama uzingatiwe watozwe faini kali huenda ikapunguza tatizo hali ni mbaya boda zinaua sana barabarani
Mpaka sasa hivi sheria zipo lakini ndiyo hivyo vijana hawataki kuzifuata!
 
Hawa madada nao,siku ingine utasikia kapanda na mtoto bodaboda! Mtoto anasimulia jinsi alivyoinjoi bodaboda. SMH
 
Yaani inashangaza. Ukiacha polisi,je watu wengine hakuna kitu wanaweza kufanya?
Imeniuma Sana......

Mwanadamu ni kiumbe cha thamani sana.... kuanzia kikiwa hai na hata kikiwa hakina Uhai.....ndio maana kuna mazishi na makaburi.........

Yaani binadamu wanaacha maiti ya binadamu mwenzao inadharirika kwenye mvua kwa kauli ya polisi.......

Seriously mwanadamu anazungukwa na binadamu wenzake wanamtazama kama mzoga kwa masaaa zaidi ya sita.......

Watu wanashindwa kwenda kituo cha polisi na kujitolea hata elf 20 ya mafuta kuja kumchukua marehemu....???

Binadamu tumefikia kubaya Sana kwenye matendo ya kibinadamu na utu...............

Dah!!!!
 
Uko sahihi mkuu, Uendeshaji wa bajaj hapa mjini, nao unatia mashaka sana coz wanajichomeka chomeka sana, nayo ni hatari
 
Sina la kusema mkuu, maana kuna wanaotegemea kuishi kwa hizo boda hivyo siwezi kuziita takataka labda sheria zikaziwe, usalama uzingatiwe watozwe faini kali huenda ikapunguza tatizo hali ni mbaya boda zinaua sana barabarani
Nafikiri alaaniwe yulee aliyezilaani kwanza kwa kusema ni kazi ya laana.
 
Mama Samia Hadi awatumie hela ya mafuta Kwenye M-pesa
 
Habari hii haijakamilika kabisa.Haijaeleweka vyema.
Anyway, nawapa pole sana wafiwa.

But all in all, natoa tena angalizo kwa Waandishi wa Habari Tz wanatakiwa kuwa makini sana muda wote kuhusiana na maisha yao kwani wengi wao nyoka wapo majumbani mwao na kwenye ofisi zao wanapofanyia kazi.
 
Kifo chake ni cha kupangwa?
 
Boda Boda ni death trap ila hatuwezi zikwepa kiukweli. Daladala na foleni hizi ni kero mno. Yani hazivumiliki kabisa kama una nauli utalipa boda boda tu ikupeleke. Gari binafsi ndio yale yale maana una ganda for hours kwa safari ya dakika 20 tu.
Hizi siku mbili boda nimepanda mitaa ya kkoo bila kupenda ila risk ndo hizi sasa.. Barabara mbovu na miundombinu inaondoka na roho za watu aisee gari binafsi shida.. usafiri wa umma nao usiseme limebaki kaburi tuu ukipanda ukifika salama unamshukuru Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ