Zuchu bado ana safari ndefu sana kimuziki ,bado hajapata fan base ya kwake yeye kama yeye bila kumtegemea Simba

Zuchu bado ana safari ndefu sana kimuziki ,bado hajapata fan base ya kwake yeye kama yeye bila kumtegemea Simba

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Ukweli usemwe tu, Zuchu ni msanii mzuri na msanii mkubwa ila bado hajafika viwango vya kumuweka kama msanii mkubwa hapa nchini ukimlinganisha na wasanii wa kike wakubwa wa kizazi chochote kike, kilichopo na kilichopita.

Kwa kizazi kilichopo ,Zuchu hamfikii hata kidogo Nandy , Nandy anaweza kusimama yeye kama yeye Zuchu bado hawezi kusimama akiwa mbali na Diamond Platinums

Kwa kizazi kilichopita huko Zuchu hagusi kabisaaaa wala tusimdanganye .

Akiendelea kukaza tutamuweka kwenye kundi la wasanii wa kike bora wa muda wote kama ilivyo kwa Lady Jaydee.
 
Kwahiyo unatakaje?

Ukimsapoti Nandy sio lazima ung'ang'anie na Zuchu atoke wasafi ndo umsapoti, unaweza achana naye km huwezi msapoti akiwa usafini na kuamua kumsapoti hata Maua Sama. Kuna wasanii wengi sana nje ya Wasafi lakini bado mmewakomalia wa usafini ili wajiengue.

Kwani ili uitwe msanii mkubwa inabidi uwe unajitegemea? Hebu ngoja nikamwangalie Nicki Minaj huwenda anajisimamia
 
Na ni mwanaume kaposti hii TAKATAKA?? Tunasafari ndefu kama Taifa.

Yaani msanii wa kwanza wakike kwa Tanzania nzima kama sio East Africa, kufikisha idadi ya watazamaji wa Video ya wimbo Mmoja kwa miaka 3 pekee, zaidi ya watazamaji million 100, na ukumbuke hiyo si Colabo kwamba useme wimbo ulipewa Busta.. na ukumbuke huyo ni mwanadamu wa pili baada ya bosi wake diamond, kufikisha views zaid ya mil100, na pia ndiye mwanamke pekee wa Tanzania na East Africa nzima kufanya maajabu hayo, then uje kumcampare na hao wasanii wenu ambao, hawamfikii kwa lolote kuanzia number of viewers, hitting songs, mpaka madili.

Acheni ushabiki wa kitoto nyie haters
 

Attachments

  • Screenshot_2024-12-05-22-57-02-09_f9ee0578fe1cc94de7482bd41accb329.jpg
    Screenshot_2024-12-05-22-57-02-09_f9ee0578fe1cc94de7482bd41accb329.jpg
    334.4 KB · Views: 4
Back
Top Bottom