JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo linalokabili wanaume wengi duniani. Kwa mujibu wa tafiti, tatizo hili linazidi kuwa kubwa miaka ya hivi karibuni tofauti na zamani. Katika kutafuta visababishi vyake, Mdau mmoja wa JamiiForums aliweka chapisho lake lenye utafiti unaotaja sigara kuwa miongoni mwa mambo yanayofanya tatizo hili litokee. Ni kweli kuwa sigara inaweza kusababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume?
Miaka ya 2000s imekumba na mabadiliko mengi ya kiteknolojia ikiwemo uwepo wa safaru za kidigitali ambazo haiziwezi kudhibitiwa na mamlaka za serikali (Benki Kuu). Sarafu za kidigitali zinazotambulika hadi sasa ni pamoja na BitCoins na OneCoin. Sarafu nyingine ya Islamic Coin (ISLM) imeibuka. Hivi karibuni kumeibuka madai kuwa sarafu hiyo imetambuliwa na Fatwa kuwa ni halali kutumika na waislam.
Kipindi cha afya hai ya uzazi wa mwanamke hutawaliwa na mizunguko ya hedhi ya kila mwezi ambayo hukoma baada ya kupata ujauzito, muda mchache baada ya kujifungua na pia baaada ya kufikia umri wa ukomo wa hedhi. Kwa maana rahisi, mwanamke hawezi kupata ujauzito ikiwa hapati hedhi. Hata hivyo, tumesikia mara kadhaa baadhi ya wanawake wakitoa madai kuwa wamepata ujauzito muda mfupi tu baada ya kujifungua, kabla hata hedhi yao ya kwanza haijarudi. Madai haya yana ukweli kiasi gani?
Asali ni chakula kinachotumika kama dawa ya magonjwa mengi. Hutibu vidonda, kikohozi, huondoa sumu mwilini, ni chanzo bora cha nishati pia hutumika kwa kazi nyingi za urembo. Ukipita mtandaoni utaona baadhi ya makala zikiweka marufuku ya kuwapatia watoto wachanga asali. Jambo hili linaleta ukakasi mkubwa wa jamii kwa kuwa asai imekuwepo kwa miaka mingi, na karibia kila jamii huitumia. Katazo hili lina ukweli gani kisayansi?
Kwa mujibu wa mdau mmoja, Disemba 12, 2019 aliona kwenye taarifa ya habari ya chombo kimoja wakitangaza kuwa familia moja imepoteza watoto wao wanne kwa kile kinachodaiwa kuwa walikula mihogo yenye sumu. Aidha, mada hii imekuwa inazungumzwa sana mitaani, huku ikiacha mashaka makubwa kwa kuwa mihogo ni chakula kinachotumika kwa kiasi kikubwa, kama kingekuwa na sumu basi watu wengi wangekuwa wamepoteza maisha. Tuelewe nini kuhusu madai haya? Ni kweli kuwa mihogo huwa na sumu, au ni uzushi tu unaopaswa kupuuzwa?
Madai Shirika la utangazaji la BBC liliripoti kuwa nchi ya China ina mpango wa kufungua vituo vya polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na raia wake wanaoishi katika nchi hizo tatu za Afrika, tovuti inayomilikiwa na mtu binafsi ya Nigeria ya Vanguard imeripoti. Wakiwanukuu watetezi wa Usalama, Vanguard amesema mpangilio wa China unaweza kuonekana kama shambulio dhidi ya uhuru wa eneo husika. Aidha inaelezwa kuwa, [China] imeamua… kushirikiana na United Front linked, mashirika ambayo yako nje ya nchi katika mabara matano, kuanzisha mfumo mbadala wa polisi na mahakama ndani ya nchi tatu, na kuhusisha moja kwa moja mashirika hayo katika mbinu zisizo halali zinazotumiwa kuwasaka...
Mdau wa JamiiForums.com ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa UTI kwa wanawake. Anahoji inakuwaje sababu kubwa inayotajwa kuwa ni uchafu ipate mashiko kwa nyakati hizi, kwani wanawake wa zamani ndio walikuwa wasafi zaidi kuliko hawa wa sasa? Mdau huyu anashauri wataalam wa afya waingie upya maabara kuchunguza nini hasa chanzo halisi cha kuongezeka kwa maambukizi ya UTI. Kwake hoja ya kuwa ugonjwa huu unaweza kusababishwa na uchafu anaona kama haina mashiko. Sayansi inasemaje juu ya hoja hizi za mdau?
Habari zenu wakuu Hivi nmekua nikijiuliza sana ni hali ya hewa ndio inapelekea watu kuumwa sana sasahivi au ni nini?? Maana nmekua nikishuhudia watu wangi wakikohoa sana ambapo hali hii yakukohoa wengi wamekua wakieleza kua huwakuta sana ifikapo mida ya saa 12 jioni ambayo huwafanya hata washindwe kulala kwa kikohozi icho kikali. Je, mabadiliko ya hali ya hewa yana mchango wowote katika kusababisha magonjwa?
Leo, Machi 15, 2021 Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania ameanza ziara mkoani Tanga na akiwa kwenye kiwanda kimojawapo alichozindua kinachoshughulika na matunda wilayani Korogwe, alipata nafasi ya kusalimu wananchi baada ya kuombwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo alianza na salamu kutoka kwa Rais Magufuli "Kabla ya kuwapongeza niwasalimie salam za Rais anawasalimia, anasema tuendelee tuchape kazi, kipindi hiki tushikane tujenge mshikamano, tujenge upendo, tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu" Baada ya salam hizo Mama Samia amewapongeza kwa kuwa na kiwanda kwani ni mkombozi.
Back
Top Bottom