Nimepokea hivi karibuni voice note kutoka kwa Mtanzania anayeishi Afrika Kusini. Sauti hiyo ya Dudula Master ambaye ni mhamasishaji mkubwa wa Xhenophobia ametoa onyo dhidi ya wageni wote kuondoka Afrika ya Kusini kuanzia tarehe 02 Septemba 2022 hadi Machi 2023.
Nchi zetu hususan Tanzania zinapaswa kuhakikisha usalama kwa raia wao wanaoishi kule kihalali na ikiwezekana kuweka utaratibu wa kuwaondoa raia wake Afrika ya Kusini.
Matishio haya yamekuwa yakifanyika bila hatua zozote kuchukuliwa, hivyo inawezekana baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola vya Afrika ya Kusini ni wahusika wa hizi operesheni dhidi ya wageni.
Hatulipi ubaya kwa ubaya bali kumtenga mtu mbaya ni sehemu ya kumpa fundisho dhidi ya mtenda ubaya. Ni wakati sasa wa Nchi...