JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Kama ilivyozoeleka kwenye jamii nyingi kuwa ukiwa Rastafarian basi kwa asilimia kubwa utakuwa unatumia bangi/marijuana na majina mengine lukuki kama inavyojulikana. Leo kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa kuna meme inasambaa ikiwa na ujumbe "Wakati Lucky Dube anaimba "Born to Suffer" me nilidhani ni sababu anavuta bangi" Meme hii ikanikumbusha article niliyowahi kusoma kuwa Lucky Dube alijiepusha na matumizi ya bangi, pombe na sigara ili kuwa mfano mzuri kwenye jamii.
Kuna kijiwe huku Bonyokwa tunapiga stori za kawaida kuhusu nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Sasa kuna jamaa kasema kuwa Rais wa awamu ya pili nchini Kenya, Hayati Daniel Arap Moi wakati anaingia madarakani hakuwa na mahusiano kabisa na hakutaka kujihusisha nayo kabisa. Nguvu kubwa alielekeza katika malezi ya watoto. Jambo hili lilimfanya ahudumu miaka 24 ya urais bila kuwa na mke (First Lady) jambo ambalo halijazoeleka ulimwenguni, kwamba kuwe na mtawala asiye na mwenza. Daniel Toroitich Arap Moi (Google)
Bado nipo njiapanda, nimesikia kuwa mwanamke mjamzito akinywa pombe kwa kiwango kikubwa wakati wa ujauzito basi huweza kusababisha changamoto kubwa sana kwa mtoto. Kuna wajawazito kadhaa nimepata kuwaona wakinywa pombe tena kali sana lakini hizo changamoto kwa watoto wao sijaziona. Baadhi ya changamoto nilizoambiwa ni kuwa na kichwa kidogo isivyo kawaida, uso bapa, macho madogo, pua ndogo nk Naomba kujua hili ili nimkanye mama kijacho kufakamia mipombe asijeleta balaa ndani.
MADAI Mdau wa JamiiForums ametoa mkasa mmoja unaomhusisha mume wa rafiki yake wa kike aliyeanza kuonesha dalili za ujauzito kwenye ujauzito mchanga wa mkewe. Mdau anaeleza kwamba shemeji yake huyu ilikuwa kila asubuhi anatapika njano, na homa za hapa na pale na kila alipoenda hospital Ugonjwa haukuonekana, ilifikia wakati mwanamme akawa hawezi kufanya shughuli zake kwa sababu ya kutapika sana. Baada ya kupima ilikuja kugundulika kuwa mkewe alikuwa na ujauzito. Ikasemekena kwamba kuna nyakati fulani ujauzito anabeba mwanamke Ila mabadiliko na dalili za ujauzito anakuwa nazo mwanaume. Jambo hili ni kweli au uzushi?
Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele. Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria. Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar. Huu Muungano ni wa kishenzi sana.
Wakati napitia pitia mitandaoni kutafuta style mpya kwa ajili ya shangazi yenu ndio nikakutana na hili bandiko kuwa aina ya kujamiiana huku mwanamke akiwa amemkalia mwanaume juu ('woman on top' or 'cowgirl' or 'reverse cowgirl'), hatari kwa afya ya mwanaume kwani hupelekea maumivu makali kwani hupekelea fracture ya uume kwa asilimia kubwa wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Inashauriwa mwanaume ndio akae juu ili kupunguza uwezekano wa kupata madhara.
Aprili 27, 2023, akaunti ya Mtandao wa Twitter inayotumia jina la MainLandAfrica iliweka chapisho linalodai kuwa Bilionea wa Marekani Dan Friedkin amekodisha takriban Ekari 6,000,000 za ardhi nchini Tanzania. Chapisho hilo lilienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Friedkin ni mmiliki wa Ekari zingine 25,000 za ardhi zinazounda pori la Akiba la Mwiba. Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
Ingawa ni kama utani na inachekesha ila huwezi amini kuwa ng'ombe akijamba/kutoa ushuzi basi kile kitokacho huambatana na gesi ya methane ambayo huzalisha joto na moto/mwanga. Wanaharakati mbalimbali wa mazingira wamekuwa wakidiscourage ufugaji/uzalishaji wa ng'ombe kwa wingi na kusema wazi kuwa ushuzi wa ng'ombe huleta mabadiliko ya hali ya hewa, kwa sababu ng'ombe hutoa methane, gesi chafu inayohusishwa na ongezeko la joto duniani. Ng'ombe akiwa anajamba, ukiwasha njiti ya kiberiti moto unawaka kutokana na gesi ya methane. Ningependa kujua ukweli wa hili jambo.
Back
Top Bottom