JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Huwa navutiwa sana Historia za wanamke shupavu ambao walifanya mambo ya kuacha alama kwenye jamii zao na kukumbukwa mpaka sasa. Katika pitapita zangu kwenye machapisho nikavutiwa na historia ya mtawala kutoka katika kabila la Waha wa Jamii ya Kitutsi, ukanda wa Kasulu sehemu za Heru Juu. Imezoeleka kuwa wanaume ndio huwa machifu katika jamii mbalimbali za Kitanzania kabla na baada ya Uhuru. Sikuwahi kusikia mwanamke yeyote kuwa Chifu wa jamii fulani tofauti na Theresa Ntare. Tukiachana na Chifu Hangaya ambaye ni Chifu wa Heshima wa kabila la Wasukuma, naweza kuhitimisha kwa kusema Chifu Theresa Ntare ni Chifu pekee mwanamke katika historia ya nchi yetu Tanzania. Mwami Theresa Ntare
Nimeona taarifa mtandaoni ikisema watumishi wa Umma na Binafsi ambao wamechangia kwa zaidi ya miezi 108 yaani miaka 9 katika NSSF au PSSSF sasa rukhsa kutumia michango yao kama dhamana ya kuchukulia mkopo wa kujenga, kuboresha au kununua nyumba nchini Tanzania. Kanuni namba 141 za Mwaka 2024 zimeanza kazi tangu Machi 8, 2024. JamiiCheck tusaidieni kujua ukweli wake.
Matumizi ya tumbaku ni moja ya maafa ya afya ya umma yanayojulikana sana. Licha ya ripoti nyingi kuhusu afya ya umma, matumizi ya tumbaku yanazidi kuongezeka katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takriban watu Bilioni 1.3 duniani wanavuta sigara ambapo 80% kati yake wanatoka kwenye nchi zenye uchumi mdogo na uchumi wa kati. Aidha, takriban watu Milioni 7 hupoteza maisha kutokana na athari za moshi wa sigara unaotokana na kuvuta sigara moja kwa moja au pia kuvuta moshi uliotolewa na mvutaji wa Sigara. Tumbaku huathiri karibu kila kiungo na mfumo katika mwili, ikisababisha matatizo mbalimbali kama vile saratani, Magonjwa ya mfumo wa upumuaji, Ugonjwa wa Mishipa ya Moyo, Kiharusi...
Leo nimesoma mtandaoni kuwa Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Naomba kujua kama ni kweli maana siku zote mie najua vidonda vya tumbo huvipata mtu kutokana na mtindo wake wa maisha(kutokula) au kwa kutumia baadhi ya dawa ambazo zinaweza kuchubua utumbo. Sasa hii ya kuambukiza kwangu imekuwa mpya sana, tena mwandishi alifafanua zaidi kuwa eti iwapo mwenza wako ana ulcers basi uwezekano wa wewe kuupata ni mkubwa maana anaweza kukuambukiza.
Baada ya kauli ya CDF wa Tanzania Jenerali Mkunda kusema kuwa 'Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi' imenifikirisha sana nikakumbuka nilishawahi kusikia tetesi kuwa Paul Kagame wakati akiwa mkimbizi nchini Uganda, aliwahi kuhudumu kwenye jeshi la nchi hiyo na mpaka kufikia cheo cha Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda. Mpaka sasa tunaona jinsi Kagame anavyoisumbua Uganda labda kutokana na ukweli kuwa anaijua nje ndani. Je, ni kweli Paul Kagame aliweza kuaminiwa na kupewa cheo nyeti kwenye Jeshi la Uganda?
Kuna dada zetu wanapenda sana urembo hivyo kujiongezea baadhi ya vitu kama matako, kope, lenzi kwenye macho, matiti vimekuwa vitu vya kawaida sana kwao. Ukweli hayo yote wanayojiongea yanakuwa na madhara. Mimi nipende tu kutoa hadhari kuwa kope na lenzi bandia mnavyojiongezea ni hatari kwa afya ya macho yenu. Chonde chonde ridhikeni na mlivyoumbwa navyo. Khadija Omary ni mmoja wa wahanga wa kupofuka baada ya kuwekewa kope bandia. Ni hayo tu.
Salaam wakuu, Wakati mikoa mingi nchini ikiendelea kupata mvua ya kutosha, kwa wengine imekuwa neema kwao kwani sasa wanaweza kuvuna maji ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mifugo na hata mazao. Sasa kwa matumizi ya nyumbani ni pamoja na kuyatumia kwa kunywa bila kuyafanyia treatment yoyote. Tokea nakua kumekuwa na kasumba na kuaminishana kuwa maji ya mvua ni bora kwa kunywa. Mvua ikinyesha tumekuwa tukiyakinga na kunywa moja kwa moja bila kujua madhara yake Pamoja na kubeba vimelea vingi na kila aina ya takataka, pia kuna aina ya madini maji hayo hukosa kwa ajili ya afya ya binadamu. Pia kuna jamii zinaamini kuwa maji ya mvua yanatibu magonjwa mbalimbali. Maji ya mvua yanaweza kuwa safi lakini siyo salama.
Haya mambo yasikie tu, watoto wetu siku za shule huwa wanalazimishwa kulala tu punde wamalizapo kula. Hii ni hatari kwa mujibu wa tafiti za afya. Uelewa mdogo na kutojali kwa wazazi kunaweza kupelekea watoto wetu kupata madhara hapo mbeleni. Kulala mara baada ya kula ni kitendo ambacho hupendelewa kufanywa na mamilioni ya watu japokuwa tabia hii si nzuri kiafya, kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wansayansi wa chuo kikuu cha Loannina Medical watu wanaosubiri kulala kwa muda kidogo mara baada ya kula wana nafasi ndogo ya kupata ugonjwa wa mshtuko na hii ndio sababu inashauriwa kukaa masaa mawili mara baada ya kula ndipo kulala.
Wote mnaweza kufikiria ni namna gani mtu asiye mkazi au mfanyakazi au mwenye appointment kwenye makazi rasmi ya Malkia wa Uingereza angeweza kupenya bila kuonekana, akafanikiwa kuingia ndani ya jumba hilo, akapiga misele kidogo, akaingia ofisi ya Malkia Elizabeth kufyonza mvinyo maalum wa Malkia, na mwisho wa siku akazama ndichi kwenye hiyo room ya Malkia na kumkuta Malkia akiwa katikati ya njozi tamu, akaketi pembeni yake na kumsubiri Malkia aamke ili wayajenge/wapeane maelekezo. Basi kunaye dogo mmoja alileta makwaru na kufankiwa mpaka Malkia mwenye alipomsanukisha. Inadaiwa tukio hilo lilisababisha ulinzi zaidi uimarishwe na baadhi ya walinzi walifukuzwa.
Nimekuwa nikisikia kuwa wabunge wetu hawalipi kodi kwenye mshahara mnono wanaopata. Kuwa walimu wanalipwa Tsh 400,000 lakini kamshahara hako kanaliwa na PAYE. Wabunge wetu wakiwa kwenye vikao, sitting allowance na Perdiem wanakunja 470,000 kwa siku, Mshahara wa mwisho wa mwezi nao mnono hatari. Je, hakuna sababu ya wabunge kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi? Tena napendekeza hata yale marupurupu wanayopata nayo yakatwe kodi.
Back
Top Bottom