JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Hello JamiiCheck, Nimeona mtandaoni ukurasa wa Mtandao wa X wa Watetezi TV ukikanusha madai ya kuwahi huchapisha taarifa ya Rais Samia akisema kuna madini kwenye baadhi ya hifadhi zetu na yanapaswa kuanza kuchimbwa kwakuwa Simba na Tembo hawali Madini. Wao wanasema akaunti iliyoposti ni bandia, siyo yao lakini nakumbuka kama niliwahi kuiona mtandaoni siku za nyuma. JamiiCheck fanyieni uhakiki hili suala.
Nimeona video inasambaa mtandaoni ikimnukuu mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akisema kama unataka kujiunga na chama cha wadhulumaji, wizi wa kura, ulaji wa rasilimali za Taifa, giza na rushwa, ingia CHADEMA. Nimeshituka sana kusikia maneno haya kutoka kwa Mbowe. JamiiCheck tusaidieni kufanya uhakiki. Video inayosambaa Mtandaoni Video halisi
Salaam Wakuu, Nimekutana na maandiko yanadai kuwa Lissu akiwa kwenye mkutano Singida alisema mtoto wa Rais Samia aitwaye Abdul aliwahi kumpelekea rushwa akamfukuza. Je, kauli hii ni kweli? Tunaomba mtusaidie kutafuta uhakika --- Video 1: Lissu akiwa Mkutanoni Singida akielezea kufuatwa na Abdul Video 2: Lissu akieleza kufuatwa na Abdul katika Spaces ya Maria Sarungi
Kamanda Tundu Lissu amekanusha madai yaliyotolewa hapo nyuma kidogo na Lema kwamba Mbowe ndio aliyeshika chupa ya damu wakati akipelekwa Nairobi kwa matibabu. Amesema aliyeshika chupa ya damu aliyokuwa akiongezewa ni Mchungaji Peter Msigwa mwanasiasa nguli asiyeogopa hila na figisu. Wataalam wa mambo ya siasa za kusini mwa jangwa la sahara wanasema hii kauli imebeba maana kubwa sana.
Katika jamii yetu ya kitanzania asilimia kubwa inatumia vyombo vya plastiki kunywea na kulia chakula, lakini nimekuwa nikisikia kuwa plastiki ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu, wapo wanaodai inasababisha saratani, wengine inamaliza nguvu za kiume kwa wanaume na mambo mengi. Je, ni kweli ina madhara? Maana napata mashaka kwani sijawahi kusikia serikali ikisema kuhusu madhara hayo au kukemea matumizi yake wala kutoa elimu ya namna ya kuvitumia.
Kuna wazandiki huwa nawashangaa wanavyoponda pombe. Pombe haina madhara kama wanafiki wanavyotuaminisha. Pombe ni nzuri ukinywa kistaarabu, ina faida lukuki, ukibisha muulize Albert Chalamila. Tafiti zinasema kuwa beer zinasaidia kujilinda na magonjwa ya moyo. Kama mnavyojua magonjwa ya moyo yanaondoa watu kimya kimya hivyo mimi nawashauri tunywe beer kujilinda na magonjwa ya moyo. Hata Biblia inasisitiza tunywe pombe tufurahie, na mkituona tunakunywa pombe msitukwaze. Too much of anything is bad, but too much good whiskey is barely enough
Wakuu, Kuna video nilikutana nayo huko mtandaoni (nimeangalia sijaiona), huyo dada alikuwa anasimulia jinsi rafiki yake alivyokufa baada ya kung'atwa chura. Chura huyo alikuwa ndani ya kiatu chake, wakati anavaa hakumuona, basi huyo chura akamng'ata kwenye kidole baada ya kushtuka (unajua jinsi wadada tunaogopa wadudu) akamtoa kwenye kiatu na kuvaa na kuendelea na kazi zake. Baada ya siku mbili yule dada akaumwa, homa kali ikamshika kumpeleka hospitali ndio ikaonekana ni hiyo sumu ya chura, na imeshambaa mwilini kiasi ambacho hakuna msaada tena. Mwisho dada alikuwa anakoroma kama chura (kama vile inavyotokea mtu aking'atwa na mbwa mwenye kichaa) mwishowe akafa. Sasa wakuu mimi nauliza, hawa chura tunaopishana nao majumbani ndio...
Back
Top Bottom