JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

"Mama kuwa na umri zaidi ya miaka 35 au Baba kuwa na miaka zaidi ya 40 kunaweza kupelekea kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo, kupata infection wakati wa ujauzito, Mama mjamzito kuumia sababu zipo nyingi ambazo zinapeleka mtoto kuzaliwa na mtindio wa ubongo" Dkt. Alvin Miranda. vijana wenye malengo ya kupata watoto, jitahidi uzae ukiwa under 35
Tumefanikiwa kuipata picha hii ambayo inaaminika huyu ndio Gustave. Kuna Mamba katika Ziwa Tanganyika anayeitwa "Gustave" ambaye inadaiwa ameua zaidi ya watu 300 katika miongo kadhaa iliyopita. Kumekuwa na majaribio kadhaa ya kumuua au kumkamata bila mafanikio. Gustave ni mamba wa kiume yupo tangu mwaka 1955 ambaye huzurura katika fukwe ndani ya Ziwa Tanganyika. Inasemekana kuwa Gustave aliua watu 300, amepata hadhi ya kuzungumzwa na anaogopwa sana na watu. Uwezo wake ni mkubwa sana wa kukamata na nguvu zake hazieleziki. Urefu wake ni mita 6.1 ana uzito wa kilo 907 kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika. Ana uwezo wa kukamata mnyama yeyote yule wa nchi kavu na majini ikiwemo Kiboko. tembo n.k. Wazungu wamelichukulia swala hili ni maajabu...
Nimesikia sehemu kuwa binadamu anaweza kupata usugu wa vimelea kutokana na kutumia mazao yatokanayo na wanyama mbalimbali, mfano wa mazao hayo ni nyama nk. Hofu yangu ni kuwa wafugaji wengi siku hizi wamekuwa si waaminifu kabisa, wamekuwa wakitumia madawa hatari kwa ajili ya kukuzia haraka wanyama ili waingize sokoni, au wakati mwingine wamekuwa wakitumia madawa kwa ajili ya kuhifadhi mazao hayo ili yakae muda mrefu bila kuharibika. Kumekuwepo cases nyingi za nguruwe na kuku kuchanganyiwa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI. JamiiCheck.com naomba mniondoe wasiwasi huu maana tunakoelekea huko mbeleni ni hatari.
Nimeona mjadala kuhusu mihula anayoruhusiwa kugombea makamu aliyeshika madaraka ya Urais kutokana na kuchukua kiti katikati ya muhula baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kuendelea aidha kwa kufariki akiwa madarakani, kujiudhuru au sababu za kiafya. Mjadala umechagizwa na kauli ya Sophia Mjema aliyesema Rais Samia ni hadi 2035, huku wanaharakati wakipinga vikali kuwa hana sifa ya kugombea mihula miwili tena. Je, ukweli ni upi?
Back
Top Bottom