JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Hii dunia ina vitu vya ajabu sana na vya kushangaza. Kuna historia baadhi unaweza unaweza kushangazwa nazo mojawapo ikiwa hii niliyopata kusimuliwa. Msitu wa Nyumbanitu una historia nyingi za kushangaza. Msitu huu upo katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoa wa Njombe. Msitu huu nimepata kusimuliwa kuwa endapo mwanamke atakuwa kwenye siku zake basi hatoruhusiwa kuingia katika msitu huo, Ikiwa atakaidi basi akiingia kwenye huo msitu ndio utakuwa mwisho wake wa kuonekana maana atapotea mazima. Nadhani hili jambo mnaona linavyostaajibisha. Najiuliza huu msitu una nguvu na miujiza gani mpaka uweze kuwatendea hivyo dada zetu.
Miaka kadhaa nyuma niliwahi kusikia mwanamke mmoja nchini Uganda kajifungua watoto wawili (mapacha) wenye baba tofauti, hali hii ilinishangaza sana. Hali kama hii iliripotiwa pia Septemba 9, 2022 kwenye jarida la CNBC ambapo mwanamama mmoja kutoka Minerois, Brazil alithibitika kuwa na ujauzito wa mapacha ambao baada ya kupimwa DNA zao ilibainika kuwa walikuwa wa baba tofauti. Kisayansi, ni kweli kuwa jambo hili linaweza kutokea? Kama jibu ni ndio, linatokeaje?
Kijana wa miaka 29 aliushangaza ulimwengu kwa kitendo cha kikatili kisichokuwa na chembe ya utu. Inadaiwa baada ya kumpindua na kumuua Rais aliyekuwa madarakani William Tolbert, Samuel Doe alihakikisha anamaliza mizizi ya mtangulizi wake kwa kuua viongozi wote waandamizi. Inadaiwa Aprili 22, 1980 viongozi 13 walifikishwa ufukweni mwa bahari ya Atlantic nchini humo, wanaume hao 13 walikuwa nusu uchi ambapo walifyatuliwa risasi na vikosi vya Rais Samuel Doe. Kati ya waliouawa ni pamoja na Frank E. Tolbert ambaye alikuwa Kaka yake na rais Tolbert, na Rais wa Bunge la seneti. Picha: hali ilivyokuwa siku ya mauaji Muosha huoshwa, Rais Samuel Doe naye alikuja kupinduliwa na kuuawa kikatili sana na waasi.
Salaam Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo. Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi. Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini: Picha: Dkt Slaa Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi Chanzo: Star TV
Nianze kwa ku-declare interest kuwa mimi ni mzaliwa wa Mkoa wa Kagera Wilaya ya Missenyi. Katika makuzi yangu hasa baada ya kutoka nje ya mipaka ya mkoa wa Kagera, nimekuwa nikishambuliwa na kutaniwa sana kuhusu UKIMWI kuanzia mkoa wa Kagera. Hayati Rais Magufuli kwa nyakati tofauti amewahi kunukuliwa akiusema mkoa huko kwamba kila janga baya huanzia mkoa huo. Rais Magufuli awashangaa Kagera kila jambo baya kuanzia mkoa huo Pia watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakiuponda mkoa huo kuhusu kuwa chanzo cha kuleta UKIMWI Tanzania. Je, ukweli ni upi kuhusu historia ya UKIMWI nchini?
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza anuai mpya ya COVID-19 iitwayo EG.5 - iliyopewa jina lisilo rasmi "Eris" huku likishauri kila nchi kuchukua hatua mahsusi za kufuatilia uwepo wake. Lakini shirika hilo linasema inaleta hatari ndogo kwa afya ya umma, bila ushahidi kwamba husababisha ugonjwa mbaya zaidi kuliko lahaja zingine zinazozunguka kwa sasa.
Kizza Besigye na Yoweri Museveni walikuwa marafiki walioshibana wakati wa Vita ya Msituni Uganda kumuondoa Milton Obote miaka ya 1980, na Dkt. Besigye aliwahi kuwa daktari binafsi wa Museveni na wanajeshi wengine waliokuwa msituni pamoja na Museveni Rais Museveni na Winnie Byanyima walikuwa wachumba kati ya 1981 na 1986, Bi Byanyima alikuwa pamoja na Museveni alipoingia Kampala akiwa mkuu wa jeshi la waasi mwaka 1986. Lakini Museveni hakuwa tayari kumuacha mkewe, Janet, na Bi Byanyima akafukuzwa. Hatimaye aliolewa na Dkt. Besigye 1998. Inadaiwa kitendo kile kilimuuma sana Rais Museveni, kwanza akataifisha ranchi ya babake Winnie Byanyima, Mzee Boniface Byanyima. Pia matukio hayo ya ngono na usaliti yalijenga uadui mkubwa kati ya...
Kuna maeneo fulani nimepita ya mkoa wa dodoma wilayani huko; nimekuta kuna msururu mrefu sana wa vyombo vya moto kwenye moja ya petrol station. Nikajaribu kuuliza kuna shida gani hapa? Wenyeji wanasema mafuta ya petrol hamna kabisa wilayani hapo. Baadhi ya vituo vya mafuta vimesitisha huduma. Pia majuzi nilisikia kuna sehemu hapa tz pia kuna shida ya mafuta.
Licha ya kuwa Mazoezi husaidia kujenga na kulinda Afya, kuna masuala muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanza mazoezi ikiwemo kuchagua eneo la kufanyia mazoezi ambalo litakuwa salama kimiundombinu na kimazingira. Katika siku za hivi karibuni watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi katika maeneo ya jirani au pembezoni mwa Barabara zinazotumiwa na Vyombo vya Moto (Magari, Pikipiki Bajaj na Mitambo mbalimbali) hali inayodaiwa kuwa watu hao huvuta hewa chafu. Je kuna ukweli wowote hapo?
Hoja ya Serikali ya Tanzania kufanya Makubaliano ya awali na kampuni ya DP World ya Dubai kwenye kuendeleza bandari ya Dar Es Salaam imezua mambo mengi yanayojadiliwa sana. Mojawapo ya Mambo hayo ni kuhusisha Bandari kuwa miongoni mwa masuala ya Muungano. Baadhi ya watu wamekuwa wanadai kuwa Bandari ni Suala la Muungano huku wengine wakipinga. Ukweli upoje?
Kuna wakati jengo la Burj Khalifa lilisambaa mtandaoni likiwa na bendera ya Tanzania na Picha ya Rais, lakini kwa siku za hivi karibuni nimeona tena mitandaoni kuna picha za bendera za majirani zetu zikiwa kwenye jengo hilohilo. Mjadala wa bendera za nchi za Afrika mashariki kuwekwa kwenye jengo la Burj Khalifa umeshika kasi zaidi mitandaoni leo 14/07/2023 baada ya Rais Samia kudokeza kuwa ipo nchi jirani bendera yake imewekwa pale baada ya kuwapo kwa malumbano ya mkataba wa bandari nchini. Ukweli wa jambo hili upi? Je, picha za majirani zetu ziliwekwa baada ya Tanzania kuwekwa?
Nimekuwa nikisikia kutoka kwa watu mbalimbali kuwa pindi hutumiapo dawa zozote basi itakupaswa usitumie maziwa aina yoyote kwasababu matumizi ya maziwa hupunguza au kuondoa kabisa ufanisi wa dawa hizo hivyo kupelekea kutotibu ugonjwa uliokusudiwa. Kwa uelewa wangu ni dawa mbili tu ambazo hushauriwi kutumia maziwa pindi ukiwa unazitumia ambazo ni Tetracycline Antacids Je, upi ukweli kuhusu jambo hili? Nawasilisha.
Back
Top Bottom