JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Nimekuwa nikisia mara nyingi kuwa kunguru akifa haozi, bali hukauka tu na kadiri siku zinavyozidi kwenda hupukutika mpaka kuisha ila huwezi kuta kaoza wala kutoa harufu. Badhi ya watu huwa wanasema haozi kwa sababu hali chumvi japo sina hakika katika hili maana mara kibao amekula vyakula vyenye chumvi kama nyama na vyakula vingine hapa home. Je kuna ukweli wowote katika hili? Kama ni kweli sababu ni nini?
Wakuu nimekutana na video inayosambaa kwa kasi sana mtandaoni ambapo wanaonekana John Mrema na John Mnyika, na Mrema akisikika kuwa atatoa maoni juu ya usafiri huo mara baada ya safari kukamilika lakini kinachonipa utata ni sauti inayosikika katika video hiyo baada ya Mrema ikisema viongozi hao wamesifia huduma za usafiri wa treni ya mwendokasi (SGR) na filamu ya royal tour wakati Mnyika na Mrema hawaonekani wakitoa maoni hayo, Je kuna ukweli wowote hapa?
Katika pita pita zangu mitandaoni leo nimekutana na "Twit" inayosema kwamba Gavana wa BOT Gilman Rutihinda (1989 - 1993) alifariki kutokana na ajali ya gari mwaka 1993 kama hii tweet inavyojieleza: Hata hivyo kuna article ya Mwaka 2011 hapa katika Forum inayoelezea kifo cha Gavana Rutihinda pamoja na Waziri wa Fedha wa wakati huo Steven Kibona kwamba vilitokana na 'food poisoning' baada ya kurudi kutoka safarini India. - Sababu ya kifo cha Steven Kibona na Gilman Rutihinda Je tunaweza kupata ukweli wa vifo hivi?
"Mama kuwa na umri zaidi ya miaka 35 au Baba kuwa na miaka zaidi ya 40 kunaweza kupelekea kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo, kupata infection wakati wa ujauzito, Mama mjamzito kuumia sababu zipo nyingi ambazo zinapeleka mtoto kuzaliwa na mtindio wa ubongo" Dkt. Alvin Miranda. vijana wenye malengo ya kupata watoto, jitahidi uzae ukiwa under 35
Back
Top Bottom