Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima, ameisifu Katiba ya mwaka 1977 huku akitoa rai kwa vyama vya upinzani, hususan Chadema, kuheshimu na kushiriki kikamilifu kwenye chaguzi kwa mujibu wa Katiba iliyopo.
Padri Kitima alieleza kuwa, licha ya kuwepo mijadala kuhusu katiba mpya, Katiba ya sasa bado ina uwezo wa kuhakikisha uwazi na ushiriki wa kila mtu katika siasa.
“Katiba hii imerekebishwa mara kadhaa na bado inatosha kutuongoza kushiriki siasa kwa ufanisi. Muhimu ni kuielewa na kuzingatia ili kuimarisha demokrasia yetu,” alisema.
Aidha, alisisitiza kuwa msingi wa Katiba hiyo uliwekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. “Hii ni Katiba nzuri iliyoundwa na Nyerere, mtu wa Mungu. Msisitizo...