Umewahi kunywa sumu yoyote ile kimakosa kisha baadhi ya watu wakakushauri utumie maziwa fresh kama sehemu ya tiba?
Madai ya maziwa fresh kuwa na uwezo wa kuondoa sumu mwilini yamekuwepo wa muda mrefu. Katika kujadili ufanisi wake, mdau mmoja wa JamiiForums amekosoa vikali tiba hii kwa kusema kuwa maziwa hayana uwezo wowote katika kuondoa sumu.
Amewashauri watanzania kuacha kufanya mambo kwa mazoea pasipo kuwa na uhakika kwanza wa jambo husika.
Taarifa za kitabibu zinasemaje kuhusu nadharia ya uwezo wa maziwa katika kudhibiti/kutibu sumu mwilini?
Kwa muda mrefu kumekuwa na imani kwamba pale ambapo mtu amepita kwenye vumbi, au amevuta hewa chafu yenye moshi au vumbi jingi basi atakunywa maziwa kwa imani kwamba anakunguza uwezekano wa...