JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Hapa kijijini mjadala umekuwa ukiendelea kuhusu wanyama jamii ya Punda namna ya ulaji wa mimea, mfano "mhindi" ambao umeng'atwa na punda huwa hauoti tena, tofauti na unapong'atwa na wanyama wengine kama ng'ombe, kondoo au mbuzi, na wanakijiji wamefika mbali zaidi na kusema labda wanyama aina ya punda yamkini watakuwa na sumu, hivyo endapo watang'ata mmea huo basi huathirika na sumu, hivyo kutokuendelea kuchipua tena.
Nyota wa zamani wa Real Madrid, Roberto Carlos anadaiwa kuingia kwenye mgogoro na mkewe hali iliyopelea atumia majengo ya uwanja wa mazoezi wa Real Madrid kama makazi wakati akishughulikia suala lake la talaka na mkewe waliodumu kwa miaka 15 Wenzi hao, waliofunga ndoa mwaka 2009, sasa wanakabiliwa na vita vya kisheria kuhusu utajiri mkubwa wa Carlos, unaoripotiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 133 (Tsh410,091,550,000)
Je, ni kweli kuna Samaki mtu? Maana huku mtaani kuna watu huwa wanatuhadithia namna walikutana na Samaki watu au kuhadithiwa na wengine stori kama waliona mwanamke Mrembo mweupe kama Mwarabu ila amekaa juu ya jiwe au ufukweni au anaogelea kwenye bahara au ziwa. Mwanamke huyo wanaeleza anakuwa na nywele ndefu na chini umbile la samaki wa kawaida ila kuanzia kiunoni ndio binadamu, na wasimuliaji husimulia kuwa ukitaka kumkamata unaona analia na anaomba usimkamate wengine wakidai wana watoto wadogo wananyonyesha, au wana familia hivyo kuomba waachwe huru waondoke. Stori ni nyingi sana huku wakidai samaki watu hao hukamatwa na kuliwa kama samaki wengine huku viwiliwili vyao vikizikwa au kutupwa tena majini. Je, ukweli ni upi JamiiCheck...
Back
Top Bottom