JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Tizama hi video kwa makini kabla ya ku-comment. Kiongozi wa Korea kasikazini amelegeza mashariti kwa dini moja tu uko nchini kwake baada ya kushuhudia great miracle en Wisdom katika kitabu cha Qur"an tukufu, wakati anaingia madarakani 2011 Uislamu kama dini zingine zilikua marufuku nchini mwake, mwaka 2015 waislamu kwa kujificha ficha walifika 3000 tu kwasasa waislamu ni 30,000. Adhana ya kila swala kwa kutumia vipaza sauti misikitini imeruhusiwa katika hiyo nchi kali ya kicommunist kuna hofu kubwa kwamba Uislamu ndani ya miaka 10 watagawana hiyo nchi na wa Buddha.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza masikitiko yake na kulaani vitendo vya upendeleo vinavyodaiwa kufanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). TEF limezitaka taasisi zote zinazojihusisha na haki za binadamu, kama LHRC, kulaani vitendo vya ukiukwaji wa haki bila kuegemea upande wowote. TEF imetoa wito kwa LHRC kutoa kauli ya wazi dhidi ya mauaji, utekaji, na vitendo vya ukiukwaji wa haki kwa watu wasio na hatia. Pia, TEF imeshauri LHRC kufanya maboresho ya kimkakati ili kuepuka upendeleo wa aina yoyote unaoweza kudhoofisha lengo lake la kutetea haki kwa uwazi na usawa. TEF inaamini kuwa hatua hii ni muhimu katika kujenga jamii yenye misingi bora ya haki na usawa kwa wote.
Baada ya jana Klabu ya Simba kutoa taarifa kuwa mlinda mlango wao, Aishi Manula alishindwa kusafiri kuelekea Algeria baada ya kupata hitilafu ya kiafya dakika chache kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Haya ndio majibu ya Tanzania One "Siumwi chochote, ila wao ndio wanajua nini kinaendelea. Siwezi kuzungumza chochote, naacha wasimamizi wangu wazungumze." — Aishi Manula
Wanawake wajawazito hupewa tahadhari au hata hukatazwa kabisa kufanya baadhi ya mambo kwa lengo la kuwaepushia madhara yanayoweza kuhatarisha afya zao, pamoja na mtoto aliyeko tumboni. Miongoni mwa mambo yaliyodumu kwa muda mrefu kwenye jamii zetu ni kuzuia wanawake wajawazito kutumia mayai ili kuwalinda watoto wasizaliwe wakiwa na vichwa vikubwa, au wakiwa hawana nywele. Kisayansi, jambo hili lina ukweli kiasi gani?
Nimekutana na taarifa zinadai kuwa Baltasar Ebang Engonga ameachiwa huru na kurudi mtaani baada ya kukutwa hana hatia kwani Wanawake wale aliokuwa akifanya nao ngono kwenye zile video zaidi ya 400 ni watu wazima na walionekana kuwa wameridhia kufanya na kurekodiwa. Aidha vipimo vilionesha hana ugonjwa wowote wa zinaa na hivyo kuwa huru kwani hajasababisha madhara yoyote kwa jamii. Je, ni kweli au watu wanatupiga huku mtaani wakuu?
Wakuu nimekutana na barua mtandaoni inasambaa inaonekana kuwa ya LHRC ina kichwa cha habari, uimarishwaji wa demokrasia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, barua hiyo inaeleza kuwa Tanzania imeonesha hatua kubwa katika kuimarisha demokrasia kutokana na uchaguzi wa serikali za mitaa. wakuu hapa uhalisia ni upi imetolewa na LHRC kweli?
Back
Top Bottom