Na Mwita Mwija
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ameeleza kuwa kutokana na uhaba wa fedha, kwa sasa wagombea wote ngazo za mitaa, vijiji na vitongoji lazima wachangie kukiwezesha chama shilingi Laki nne (400,000) hii itasaidia uwezeshaji katika usimamizi wa chaguzi hizo kwa kuweka mawakala wa kusimamia zoezi hilo.
"Pia chama bado tunaendelea kutafuta wafadhiri wa kutufadhiri katika chaguzi hizi ili tuwe na nguvu kubwa na vigezi vyote watakavyo vitoa ili kutupa msaada huo wa kifedha tutavitimiza na hadi sasa tumemtuma Mhe. Tundu Lissu huko huko duni (nje ya nchi ) azungukie wadau na kutafuta fedha kwa masharti yeyote yale watakao yatoa tupo tiyari kuyatimiza na hadi sasa yuko mbioni kufanikisha hilo," amesema Katibu Mkuu CHADEMA...