JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Miaka ya hivi karibuni, matumizi ya dawa za uzazi wa mpango (Vidonge na Sindano) yameongezeka sana, hali inayozua wasiwasi wa usalama wake miongoni mwa watumiaji. Baadhi wameonesha wasiwasi wao kuwa dawa hizi husababisha kupata watoto wa kiume wenye homoni nyingi za kike, au hata kupata watoto wa kike wenye kiasi kikubwa cha homoni za kike hivyo kuwafanya wakomae mapema kabla ya umri sahihi. Mathalani, mdau mmoja wa JamiiForums.com amekiri kuwahi kusikia kuwa matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi yanaweza kusababisha mama kupata binti ambaye akifikisha umri wa miaka 8 matiti yake yanaweza kuwa makubwa, yaliyolala. Ukweli kuhusu athari za dawa hizi ukoje?
Kumekuwepo na taarifa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia gazeti la Mwananchi limeandika kuwa Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo wanasiasa wanne wa Kenya pamoja na familia zao akiwemo Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua baada ya kupata taarifa kuwa wanasiasa hao walipanga na kufadhili vurugu wakati wa maandamano ya Jumatatu iliyopita. Wanasiasa wengine katika orodha hiyo ni pamoja na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Moses Kuria, kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichungwa na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro. Ukweli wa taarifa hii upoje?
Mdau wa JamiiForums amedai kuwa jamii za wafugaji ni warefu kwasababu wanakunywa sana maziwa tofauti na jamii za watu wasiotumia maziwa. Amebainisha baadhi ya sababu ni kutokana na maziwa kuwa na madini ya calcium na vitamini D ambavyo husaidia kutengeza na kuimarisha mifupa. Kinyume chake kwa jamii za wakulima ambazo hazitumii sana maziwa huwa wanakuwa wafupi. Jambo hili lina ukweli kiasi gani?
Ushiriki wa mazoezi ni jambo muhimu kwa afya. Husaidia kuongeza utimamu wa mwili pamoja na kuupa kinga ya kutosha dhidi ya magonjwa, hasa yale yasiyoambukizwa kama kisukari, shinikizo kubwa la damu na viribatumbo. Pamoja na faida hizi, watu wengine hushiriki mazoezi mbalimbali ya Gym kwa lengo la kuboresha muonekano wa miili yao, tunaweza kusema kwa sababu za urembo au utanashati. Miongoni mwa mazoezi yanayofanyika sana siku hizi hasa kwa wanawake ni kupiga vibao sehemu ya chini ya tumbo ili kubana misuli. Je, ni kweli kuwa mazoezi haya husaidia kubana misuli ya tumbo?
Taarifa ya kusikitisha kidogo kutoka Kata ya Mwana-Mutombo Kijiji cha Mwasinasi Tarafa ya Nkololo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, Diwani kwa jina la Rambo Kidiga anatuhumiwa kuozesha wanafunzi wawili wa kidato cha pili na pia yeye binafsi kufunga ndoa na mabinti wawili wakisadikika kuwa ni Wanafunzi mmoja wa kidato cha pili na mwingine wa kidato cha tatu (majina yamehifadhiwa). Halikadhalika mtendaji wake wa kijiji alifahamika Kwa jina la Bw. Magobeko mwenye umri wa miaka 50 ameozesha binti wa kidato cha pili na vilevile Mwenyekiti wa kijiji afahamikaye kwa jina la Madereke Ngoro anatuhumiwa kuoa binti wa darasa la nne na kuachishwa masomo yake Katika Hali ya kusikitisha tumepokea malalamiko Kwa mama mzazi (Mama Nkwabi) wa binti...
Matumizi ya muda mrefu ya mafuta ya nywele aina ya body luxe (body luxe hair oil) husababisha mvi kuota kwa kasi katika umri mdogo. Hapa nazungumzia haya mafuta ya nywele ya body luxe yenye kopo la pink lenye picha ya mwanamke ana nywele ndefu. Picha: Muonekano wa chupa za mafuta ya Body Luxe kwa upande wa mbele Picha: Chupa ya mafuta ya Body Luxe ikionesha sehemu ya Viambato (Ingredients) Hii ni kutokana na uzoefu wangu (personal experience) kwangu mwenyewe, kaka yangu na jamaa mwingine ambaye tunaishi naye mtaa mmoja. Wote tumeota mvi katika umri mdogo na tumekuja kugundua shida ni haya mafuta. Mimi nilikuwa sijajua, nimeambiwa na kaka yangu jana kuwa mafuta ya nywele yanasababisha kuota mvi, nilioomuuliza alikuwa anatumia...
Mdau wa JamiiForums ametoa hoja yake kuwa watu wanaokula dagaa hupata faida kubwa zaidi kuliko wale wanaokula samaki wakubwa. Amedai kuwa tofauti na samaki wakubwa, mtu anayekula dagaa anakula hadi mifupa yake yenye madini mengi ya calcium hivyo kuwafanya wawe na mifupa imara kuliko alaye samaki wakubwa, hasa kwa watoto ambao wanakua. Amewashauri watu kutumia dagaa kwa wingi, ikiwezekana wawepo kwenye kila mlo. Madai haya ni sahihi?
Mdau mmoja wa JamiiForums ameelezea kuwa watu wanaokunywa pombe kupita kiasi (Ulevi uliopindukia) wakiacha ghafla matumizi ya pombe wanaweza kufa. Mdau huyu anaeleza kuwa pombe hupunguza utendaji wa akili kama yalivyo madawa mengine ya kulevya, pia huleta uraibu na utegemezi. Amewashauri walevi sugu kuacha pombe taratibu ili wasipatwe na athari kubwa kwenye afya, ikiwemo kifo kutokana na kifafa. Madai haya ni sahihi?
Zipo taarifa zinadai kuwa Jeshi la Tanzania katika wilaya ya Nangade, Cabo Delgado waliingia kwenye mtego wa Magaidi katika kijiji cha Vondanhar, eneo la Palma. Aidha inadaiwa Jeshi la Tanzania lilikuwa likisafiri kwa magari ya kivita sambamba na jeshi la Msumbiji. Magari matatu ya jeshi la Tanzania yamechomwa moto na baadhi ya Silaha kuharibiwa. Taarifa iliyotolewa na kikundi cha Kigaidi cha IS, imedai wamekamata baadhi ya Silaha ikiwemo Chinese Type 81-1 assault rifle pamoja na 12.7x108mm Type 54 HMG ya kwenye gari. Zaidi inaelezwa kuwa haya ni magari ya JWTZ yapo chini ya himaya ya magaidi.
Back
Top Bottom